Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Karia kufunga ushahidi kesi ya akina Malinzi

$
0
0
NA KULWA MZEE RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, anatarajiwa kuwa shahidi wa mwisho katika kesi ya kutakatisha fedha inayomkabili aliyekuwa anashikilia wadhifa huo, Jamal Malinzi na wenzake. Hayo yalibainika jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, wakati kesi hiyo ilipotakiwa kuendelea, lakini ilikwama kwa sababu Jamhuri hawakuwa na shahidi. Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai, alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, lakini hawana shahidi kwa sababu alikuwa anaumwa. Swai aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa tarehe ya karibu kwa kuendelea na shahidi wa mwisho. Mahakama ilikubali kuahirisha hadi Julai 5, mwaka huu, ambapo Jamhuri wanatarajiwa kufunga ushahidi, baada ya shahidi wa mwisho, Karia kumaliza kutoa ushahidi wake. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba na Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa. Mwingine ni Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017. Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335. Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wanaendelea kusota rumande kwa sababu wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Trending Articles