Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Kino Base Music watamba kuwapoteza B.O.B

$
0
0
NA MWANDISHI WETU KUNDI la muziki wa Bongo Fleva, lenye maskani yake Kinondoni, Dar es Salaam, Kino Base Music, limetamba kuwa kwa sasa ndilo linalowakilisha nyema wilaya hiyo kuliko kundi la B.O.B linalomilikiwa na staa wa Hip Hop, Nyandu Tozzy. Akizungumza na Papaso la Burudani jana, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo aliyeomba kuhifadhiwa jina lake, alisema kundi la B.O.B limepoteza umaarufu na asilimia kubwa ya mashabiki wao wanaunga mkono harakati za Kino Base Music. “Uliza mtu yeyote hapa Kinondoni utaambiwa Kino Base Music ndiyo kundi bora kwa sasa, tayari kumeshawafunika B.O.B, mashabiki wao wamehamia kwetu kutokana na harakati zetu kuwavutia,” alisema msanii huyo. Kundi la Kino Base Music linaundwa na wasanii kama Side Gaidi, Rapper Tino, Murph Killer, Chill Byser na Vado.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Latest Images

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>