NA
WINFRIDA MTOI
KUELEKEA
ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili dhidi ya Zesco, Mkurugenzi mpya wa
ufundi wa klabu ya Yanga ambaye ataokea nchini Uingereza, anatarajia kuanza
kazi rasmi leo.
Mkurugenzi
huyo, aliyekuwa anafanya shughuli za soka nchini Uingereza ni Mtanzania,
aliyezaliwa visiwani Zanzibar akiwa amebobea katika masuala ya ufundi na
program za vijana.
Akizungumza na BINGWA, mmoja wa viongozi wa Kamati
ya Utendaji wa Yanga ambaye hakutaka
jina lake liandikwe gazetini, alisema tofauti na ufundi, wakurugenzi wengine
watakaonza kazi leo ni wa masoko, fedha na sheria.
Kiongozi
huyo alisema hawajaweka majina ya watu
hao hadharani kutokana na kuwa walikuwa
bado katika ajira na waliakubaliana leo ndiyo wanaweza kuwaweka wazi wakati
wanapoanza majukumu yao rasmi.
“Rasmi
kesho (leo), Mkurugenzi wa Ufundi ataanza kazi, anatokea Uingereza lakini ni
Mtanzania aliyezaliwa Zanzibar, mkurugenzi wa masoko, sheria na fedha.
Kamati
ya Utendaji ya Yanga, inatarajia kukutana leo na hao waajiriwa, baada ya hapo
majina na CV zao zitawekwa wazi, tulishindwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa
walikuwa bado katika ajira,” kilisema
chanzo.
Alieleza
kuwa nafasi nyingine ikiwamo ya katibu, ofisa mtendaji mkuu na ofisa habari,
zinaendelea kushughulikiwa na kamati husika.
↧