Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Mahrez aitakia mafanikio Leicester

$
0
0
LONDON, England STAA Riyad Mahrez ameitaka Leicester City kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa kama ilivyofanya msimu uliopita, ikiwa ni baada ya kusaini mkataba mpya. Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Algeria alizima tetesi kuhusu hatima  yake kwenye klabu hiyo baada ya wiki hii kusaini mkataba mpya na kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Claudio Ranieri. Kwa kujitia kitanzi hicho, Mahrez,  ambaye alitangazwa  kuwa mchezaji bora wa Chama cha Wanasoka  wa Kulipwa baada ya kuisaidia timu yake msimu uliopita kutwaa ubingwa, atakuwa ameungana na nyota wenzake, Jamie Vardy, Kasper Schmeichel, Wes Morgan  na  Andy King, ambao tayari walishajifunga kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya King Power. Wakati Danny Drinkwater akijiandaa kufuata nyayo za wenzake na huku  N’Golo Kante akiwa mchezaji pekee aliyeondoka na kwenda kujiunga na Chelsea, Mahrez anaamini Leicester wana kikosi ambacho kinaweza kutetea taji hilo tena msimu huu. “Nina furaha kuendelea kufanya kazi na Leicester City. Itakuwa ni presha kuwa mahali hapa na nitaendelea kufanya hivyo,” staa  huyo alikiambia kituo cha televisheni TV channel. “Msimu uliopita tulipata mafanikio ya kitu kimoja kizuri nchini England. Tulikuwa na msimu mzuri, hivyo ni vizuri kuendelea kufanya hivyo,” aliongeza staa huyo. The post Mahrez aitakia mafanikio Leicester appeared first on Bingwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>