RIO, Brazil
FOWADI wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar, ameanza rasmi mazoezi ya kikosi hicho, kwa maana kwamba yuko tayari kukiwasha nchini Urusi.
Neymar alikuwa nje tangu Februari alipoumia vibaya mguu wake wa kushoto na kuhatarisha ndoto za kucheza fainali hizo.
Nyota huyo aliungana na wenzake akiwamo Gabriel Jesus na Danilo katika kambi ya timu hiyo nchini Brazil.
Wakati huo huo, mkongwe wa Brazil, Rivaldo, alimtabiria kuwa na nafasi ya kung’ara Urusi na hata kuibeba tuzo ya Ballon d’Or.
Aidha, alimtaka kujiunga na Real Madrid au timu kutoka England ili kulifanikisha hilo la Ballon d’Or.
“Ligi ya Ufaransa (Ligue 1) si kama ya Hispania na England, hizo ni ngumu zaidi,” aliongeza.
The post NEYMAR AREJEA MAZOEZINI BRAZIL appeared first on Bingwa.
↧