MADRID, Hispania
AKIWA tayari na mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kiungo wa Real Madrid, Isco, amedai kuwa nia yake ni kuhakikisha anaongeza taji hilo kwenye kabati lake msimu huu.
Kiungo huyo anatarajia kuwepo kwenye kikosi cha Madrid kitakachoivaa Liverpool kwenye fainali ya michuano hiyo, wikiendi hii.
“Nilikuwa nikiuguza bega langu kwa wiki tatu, sasa nimepona na ninafanya mazoezi kama mbogo aliyejeruhiwa.
“Natamani kutwaa taji la nne la ligi ya mabingwa. Nafurahia namna tunavyopambana kila mwaka kwa sababu sikuwahi kuwaza kama nitacheza fainali nyingi hivi katika miaka michache.
“Hivyo, sijaridhika. Nahitaji kombe jingine. Nataka niitimize ndoto ya kutwaa taji la nne,” alisema Isco.
The post ISCO APANIA KUNYAKUA MEDALI YA NNE ULAYA appeared first on Bingwa.
↧