Kulwa Mzee, Dar es Salaam
Meneja Ukaguzi na Udhibiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Sadiki Erimsu ameitaka Kampuni ya Tech Hub kuendesha mchezo wa bahati nasibu wa ‘Daka Pesa Chap Chap’ kwa weledi.
Sadiki amesema hayo leo Alhamisi Septemba 27, wakati wa uzinduzi wa mchezo mpya wa kubahatisha wa Daka Pesa chapchap na kuongeza kuwa mchezo huo utasaidia kuingia kwa teknolojia mpya, utaongeza fursa za ajira, utaliongezea taifa mapato yataokanayo na kodi na inatoa fursa ya uwekezaji.
“Michezo ifanyike kwa weledi, isiwe michezo ya laana, hii ni kampuni halali imekidhi vigezo vyote,” amesema.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Seles Mapunda amesema mchezo huo unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi kutoka kwenye simu ya mchezaji husika na kutumwa kwenda kwenye namba 727272.
“Mitandao inayoweza kufanya miamala ni Tigopesa, M pesa na Airtel Money, kupitia kumbukumbu namba teule ambayo ni Sh 500 au 1,000,” amesema.
Aidha, Mapunda alitumia nafasi hiyo kutambulisha mabalozi wa mchezo huo akiwamo nyota wa filamu nchini, Jacob Steven maarufu JB ambaye amesema kazi yake ni kuhamasisha watu wacheze kwa wingi na wapewe zawadi zao.
The post Waendesha bahati nasibu ya ‘Daka Pesa chapchap’ wafundwa appeared first on Bingwa.
↧