Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Maseneta wa Republican wawasilisha muswada kuhamisha ubalozi wa Marekani kwenda Jerusalem

$
0
0
Ted Cruz, Seneta kutoka Texas.WASHINGTON D.C., MAREKANI (CNN) Wabunge wa Baraza la Seneti kutoka chama cha Republican wamewasilisha muswada wa kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli na kutaka kuhamisha ubalozi wan chi hiyo kwenda mji mkuu wa Israel Jerusalem. Mpango huo tata, ambao Rais Mteule Donald Trump alikuwa akiusema sana wakati wa kampeni, una unaweza kusababisha misuguano zaidi baina ya Wapalestina na Wasraeli. Muswada huo uliwasilishwa katika siku ya kwanza ya Bunge la Congress na Seneta Dean Heller, akiwa pamoja na Marco Rubio wa Florida na Ted Cruz wa Texas – maseneta wawili ambao walizidiwa kete na Trump katika mbio za kupata tiketi ya Republican mwaka jana. “Jerusalem ni mji mkuu wa milele wa taifa la Kiyahudi la Israel, na huko ndipo ubalozi wa Marekani unapaswa kuwepo,” Rubio alisema katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari kuutangaza muswada huo. “Ni wakati sasa kwa bunge la Congress na Rais Mteule kuondoa mwanya ambao ulikuwa unawaruhusu marais kutoka vyama vyote viwili kudharau sheria za Marekani na kuchelewesha ubalozi wetu kuhamia sehemu sahihi huko Jerusalem kwa zaidi ya miongo miwili.” Cruz aliongeza, “Kwa bahati mbaya, utawala wa Obama ulikuwa na ajenda dhidi ya taifa la Kiyahudi na umekuwa katili hata kutamka ukweli huu rahisi – hata ule ukweli kwamba Jerusalem ni sehemu sahihi kwa ubalozi wa Marekani huko Israel – inatisha katika baadhi ya maeneo.” Muswada, unaofahamika kama “Jerusalem Embassy and Recognition Act," unaitaka Marekani kufanyia kazi pendekezo la mwaka 1995 kuitaka nchi hiyo kuhamisha ujumbe wake wa kidiplomasia kutoka Tel Aviv. Tangu muswada huo upite mwaka 1995, kila rais – kutoka Republican na Democratic – amekuwa akikwepa matakwa ya kuhama, kwa madai ya masuala ya usalama wa taifa. Suala la Jerusalem Jerusalem siku zote imekuwa miongoni mwa masuala magumu katika mgogoro baina ya Wapalestina na Waisraeli. Hata baada ya dunia kulitambua Taifa la Israel mwaka 1948, iliacha hadhi ya mwisho ya Jerusalem – nyumbani kwa maeneo matakatifu zaidi Wayahudi, Waislamu, na Wakristo – wazi kwa ajili ya mazungumzo ya siku za usoni. Waisraeli wanaiona Jerusalem yote kama mji wao mkuu. Wapalestina wanaiona Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wa taifa la baadae la Palestina. Trump amesema kwamba angependa kujaribu kufanya amani baina ya Waisraeli na Wapalestina, lakini pia ameapa kuhamisha ubalozi wa nchi yake na kutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel – kitu ambacho viongozi wa Wapalestina wanapinga kama chanzo cha kufa kwa ndoto ya taifa la Palestina. David Friedman – mteule wa Trump kama balozi wa nchi hiyo huko Israel, ni mwanasheria huko New York na Myahudi wa madhehebu ya Orthodox – ni ishara nyingine kwamba Rais Mteule anapania kunadili sera za miongo kadhaa za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati. Friedman, anayefahamika kwa misimamo yake mikali, ameziita jitihada za kuwa kwa mataifa mawili kama “ndoto” na akaongeza anakaribisha suala la kuhamisha ubalozi kwenda Jerusalem. Friedman pia amesema kwamba ujenzi wa makazi ya Waisrael katika maeneo ya Wapalestina haipaswi kuwa kinyume cha sheria – msimamo ambao unamuweka kinyume na utawala wa Obama na sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa. Hali ya wasiwasi juu ya makazi Marekani na mataifa mengine yanaona ujenzi wa makazi mapya unaofanya na Israel huko Ukanda wa Magharibi na Jerusalem Mashariki – ardhi ambazo Wapalestina wanaziona kama sehemu za taifa lao la baadae – kama kikwazo kwa matumaini ya mataifa mawili ya Israel na Palestina. Kwa miaka kadhaa sasa Marekani imekuwa ikiomba bila mafanikio kwa Israel kuacha ujenzi wa makazi mapya. Lakini mwezi Desemba, uhusiano baina ya mataifa hayo mawili ulizidi kudorora baada ya Marekani kuruhusu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa upitisha azimio linaloshutumu ujenzi wa makazi mapya kupita. Azimio – ambalo lilipita kwa sababu ya Marekani, ambayo ina nguvu ya kura ya veto, kujitoa kwenye kupiga kura – linasema kwamba ujenzi wa makazi “hauna haki kisheria na unakiuka sheria za kimataifa.” Kujizuia kwa Marekani kupiga kura ni hitimisho la miaka minane ya uadui baina ya Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Ilizua mashambulizi makali kutoka kwa Israel dhidi ya Marekani kuwa imemtua rafiki yake wa karibu zaidi. Rais Mteule Donald Trump alitumia Twittwe kuonyesha kutofurahishwa na kura hiyo, na kuonyesha kwamba kuingia kwake madarakani itakuwa ni mwanzo wa ukurasa mpya wa kirafiki zaidi baina ya nchi hizo mbili. “Hatuwezi kuendelea kukaa kimya wakati Israel inaangaliwa kwa dharau na kutoheshimika,” Trump aliandika kwenye Twitter. “Walikuwa na rafiki mkubwa kwa Marekani, lakini si hivyo tena.” Aliongeza, “Kuweni imara Israel, Januari 20 inakuja haraka!”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>