Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live

Zimbabwe's Robert Mugabe accepts disputed election result

$
0
0
"Things have been righted. We can't deny it," he says.

Chemnitz violence: 'No evidence' far-right chased foreigners, says intelligence chief

$
0
0
Germany's domestic intelligence agency says there's "good reason to believe" the reports were deliberate misinformation. A widely shared video showed far-right demonstrators chasing after people who looked non-German.

Diego Maradona: Achaguliwa meneja wa timu ya daraja la pili Mexico

$
0
0
BIngwa wa soka kutoka Argentina Diego Maradona ameteuliwa kuwa meneja wa timu ya daraja la pili nchini Mexico Dorados de Sinaloa.

Magazeti Ya Tanzania Leo Ijumaa, Septemba 7, 2018 - Habari Kubwa Magazetini leo

$
0
0
Nafasi za Kazi leo Ijumaa 7: Nafasi za Kazi zaidi kibao zilizotangazwa leo Ijumaa 7, Septemba 2018

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 7

Profesa Kikula Atoa Mwezi Mmoja Utatuzi Wa Mgogoro Wachimbaji Madini Winza

$
0
0
Na Greyson Mwase, DodomaMwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ametoa mwezi mmoja kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kuhakikisha mgogoro katika machimbo ya madini aina ya rubi yaliyopo katika kijiji cha Winza kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma unamalizika ili wachimbaji hao waendelee na shughuli zao za uchimbaji madini na kujipatika kipato.Profesa Kikula ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea kero za wachimbaji wadogo wa madini katika eneo hilo katika ziara yake katika wilaya ya Mpwapwa yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wadogo wa madini.Katika ziara hiyo Profesa Kikula aliambatana na Makamishna wa Tume, Profesa Abdulkarim Mruma na Haroun Kinega, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya pamoja na waandishi wa habari.Alimtaka Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kushirikiana kwanza kwa kuchukua alama za eneo (coordinates) ili kubaini maeneo yasiyo na leseni na kuwapatia wachimbaji hao ili wafanye uchimbaji bora wenye kufuata sheria na kanuni za madini.Aliendelea kufafanua kuwa, kwa maeneo yenye leseni wachimbaji wadogo wa madini wanaweza kuangalia namna ya kushirikiana na wamiliki wa leseni kwa kuingia ubia na kujipatia kipato pasipo migogoro isiyo ya lazima.Profesa Kikula alisisitiza kuwa lengo la Serikali kupitia Tume ya Madini ni kuona wachimbaji wadogo wa madini wanafanya shughuli zao katika mazingira mazuri kwa kufuata kanuni na sheria za madini.Katika hatua nyingine, Profesa Kikula aliwataka wachimbaji hao kuunda vikundi vidogo na kuomba leseni na kusisitiza kuwa Tume ya Madini ipo tayari  kuwasaidia kwa njia zote kupitia wataalam wake ikiwa ni pamoja na namna ya kuomba leseni za madini, elimu kuhusu kanuni na sheria za madini.Wakiwasilisha kero zao kwa Mwenyekiti Kikula kwa nyakati tofauti, wachimbaji hao walisema kuwa wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa muda mrefu pasipokuwa na leseni huku kukiwepo na watu wanaojitokeza na kudai kuwa ni wamiliki halali wa leseni za madini.Awali akielezea historia ya ugunduzi wa madini aina ya rubi katika eneo hilo, mgunduzi ambaye ni mwenyeji wa kijiji hicho,  Shabani Kigelulye alisema kuwa, kati ya mwaka 2005 na 2006 akiwa shambani kwake katika eneo hilo aligundua mawe aliyohisi kuwa ni madini ya rubi.Alieleza kuwa, katika harakati za utafiti wa  madini hayo mwaka 2007 alipeleka sampuli za mawe hayo aliyohisi kuwa ni madini ya rubi kwa ndugu wake walioko Dodoma Mjini na Arusha na kuelezwa kuwa yalikuwa ni madini ya rubi.Aliendelea kueleza kuwa kwa kushirikiana na ndugu zake alipeleka sampuli hizo za mawe kwenye Ofisi za Madini na kushauriwa kuomba leseni na kupata.Aliongeza kuwa  mwaka 2008 aliingia ubia na  wenzake Roja Sezinga, Johnson Kamara na Perfect Shayo na kuanza uchimbaji wa madini, na kusisitiza kuwa mwaka 2009 wakazi wengi wa kijiji hicho waliingia na kuanza kuchimba kiholela pasipokuwa na leseni hali iliyopelekea mgogoro.Katika hatua nyingine Profesa Kikula alitembelea eneo lililopangwa kujengwa mtambo wa kuyeyushia shaba na kukuta jengo lililotelekezwa tangu mwaka 2004Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto alimweleza Profesa Kikula na timu yake kuwa, kampuni ya Igozomo kutoka China ilipanga kujenga mtambo wa kuyeyushia shaba lakini baadaye walisitisha uwekaji wa mtambo huo baada ya kutoelewana na wazawa.Profesa Kikula alishauri wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza kwenye shughuli za madini nchini kukutana na wenyeviti wa vyama vya wachimbaji madini ambao wanaweza kuwapa taratibu sahihi za uwekezaji nchini hivyo kuepuka kuingia kwenye mikono ya matapeli.Wakati huohuo akiwa katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa, Sarah Komba, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alisema kuwa suala ushiriki wa huduma za jamii (corporate social responsibility) kwa makampuni ya madini nchini si la hiari bali ni moja ya sheria.Aliendelea kufafanua kuwa ni vyema kukawepo  mikataba kati ya wakuu wa wilaya na kampuni za madini kuhusu maeneo yanayohitaji katika uboreshaji wa huduma za jamii na kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na huduma zilizoainishwa kwenye mikataba na kupunguza migogoro.“ Serikali kupitia Tume ya Madini imeweka  mikakati ya kuhakikisha wananchi wote wananufaika na rasilimali za madini kupitia ushirikishwaji wananchi kwenye utoaji wa huduma kwenye kampuni za madini (local content) na kupata huduma bora za jamii kutokana na uwekezaji unaofanywa na kampuni za madini,” alisisitiza Profesa Kikula.Akielezea mikakati ya kumaliza migogoro kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji madini nchini, Profesa Kikula alisema kuwa Tume ya Madini inaandaa rasimu ya mfumo wa utatuzi wa migogoro  kuanzia kwenye ngazi ya kijiji, kata na wilaya kabla ya kufikia ngazi ya tume.Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa, Sarah Komba alimpongeza na kumshukuru Profesa Kikula pamoja na timu yake kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutatua changamoto kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini na kutoa elimu kuhusu sheria na kanuni za madiniAidha Komba aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kutoa taarifa za wavamizi wasiokuwa na leseni za madini ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akizungumza katika mahojiano maalum na vyombo vya habari aliwataka wananchi wanaogundua madini kwenye maeneo yao kutoa taarifa kwenye ofisi za vijiji na vyama vyama vya wachimbaji madini na kufika kwenye Ofisi za Madini  kwa ajili ya utambuzi wa madini na kuelekezwa namna ya kuomba leseni.Alisema kutokana na wagunduzi wengi kuchimba bila kushirikisha uongozi wa kijiji, wilaya na vyama vya wachimbaji madini wamejikuta wakitoa mwanya kwa wajanja kuomba leseni hivyo kuzalisha migogoro isiyokwisha.Alisema kuwa Serikali kupitia Tume ya  Madini imeweka utaratibu mzuri sana wa kumlinda mgunduzi wa madini tangu anapogundua madini hayo hadi kupata leseni.

Viwanja Vinauzwa....Surveyed plots for sale: Bunju na Mapinga (Baobab sec)

$
0
0
Viwanja viko Kimele Mapinga, umbali wa km 3 kutoka Baobab secondary. Vipo viwanja kuanzia ukubwa wa 20/20 (sqm 400) kwa bei ya tsh 4 milioni, ukubwa wa 20/30 (sqm 600) kwa bei ya tsh 6 milioni, ukubwa wa 20/40 (sqm 800) kwa bei ya tsh 8 milioni, ukubwa wa 35/40 (sqm 1400) kwa bei ya tsh 18 milioni, ukubwa wa sqm 2386 kwa bei ya tsh 31 milioni, ukubwa wa sqm 3018 kwa bei ya tsh 39 milioni.Pia Bunju B viko viwanja 2 vya sqm 1700 kila kimoja na luksa kuviunganisha ukapata kiwanja kikubwa cha sqm 3400, bei ya kila sqm ni 30,000Luksa kulipa kwa awamu 2 ndani ya miezi 3, kianzio ni 50%.Hakuna dalali. Mhusika: call 0758603077, whatsap 0757489709

Waziri Kigwangalla Aipokea Gold Ya Barnaba

$
0
0
Na Andrew Chale, DarWaziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla amempongeza msanii nyota wa kizazi kipya nchini Bongo flava Elias Barnaba maarufu kama kwa Barnaba Classic kwa hatua yake ya kutoa albam ya Gold ambayo itasaidia kukumtangaza zaidi kwenye medani za muziki ndani na nje ya nchi.Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo jana Septemba 6,2018 wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajali Agosti 4, na kumkabidhi rasmi CD ya album yake ya GOLD ambayo imeingia sokoni 31 August mwaka huu.Katika hatua hiyo Waziri alimshukuru kwa kumtembelea ambapo pia alimpatia ushauri namna bora ya kuiuza albam hiyo ya GOLD ikiwemo soko la kimataifa.“Nilipata mwaliko wako wa uzinduzi wa albam ya Gold. Bahati mbaya sikuweza kufika kutokana na ajari. Lakini naendelea vizuri na nashukuru kwa kufika kuja kuniona na kunikabidhi rasmi..natambua wasanii pia ni nguzo katika kukuza Utalii wetu ikiwemo kuutangaza kupitia ala na mashahiri yenu na ndio maana mwezi huu wa Septemba tunakuja na tamasha la Urithi ambalo Wasanii wamepewa nafasi ya kipekee” alieleza Waziri Dkt.Kigwangalla.Kwa upande wake Barnaba alimshukuru Waziri Dkt Kigwangalla kwa kuipokea Album hiyo ambayo imezingatia vigezo vyote na ubora wa hali ya juu.“Kwanza nikupe pole kwa ajali. Naamini wasanii na wadau wote tunakuombea upone haraka na urejee kwenye majukumu yako ya kila siku ya kukuza Maliasili zetu na Utalii kwa ujumla na upokee albam hii ya Gold ikuburudishe unapoendelea kuuguza majeraha, Asante Sana” alisema Msanii huyo wakati wa kumkabidhi Albam hiyo.Kwa upande wake Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa Mxcater amesema albam hiyo iliyosheheni nyimbo Bora na kali zikiwemo Chausiku, Lover Boy na nyingine nyingi inapatikana katika maduka ya mtandao yaani (Online) kupitia Boomplay Music.“Kwa watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia App ya BoomplayMusic_tz na wataipata moja kwa moja” alisema Mxcater.

Wanajeshi wa Sudan Kusini wafungwa kwa ubakaji na mauaji

$
0
0
Uhalifu huo ulitokea wakati wa shambulizi lililofanywa katika hoteli ya Terrain kwenye mji mkuu Juba mwaka 2016.

Linah: Mwili Nilionao Haunifanyi Nishindwe Kujiachia Jukwaani

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga amesema kuongezeka kwa mwili wake baada ya kujifungua haujamuathiri chochote kwenye kazi yake ya usanii na kwamba anafanya kazi zake kama kawaida. ‘’Mazoezi nafanya ya kawaida tu, naupenda sana mwili wangu, mimi naona kawaida tu kuongezeka kwangu hakujaniathiri chochote nafanya kazi zangu kama kawaida, napiga shoo jukwaani na najiona ni mwepesi kama kawaida, unajua kuwa watu wembaba lakini wazito, lakini mimi unene nilionao haunipi changamoto zozote ninapokuwa jukwaani nawaburudisha mashabiki wangu kama kawaida, halafu ujue kwamba mimi sio dansa mimi ni mwanamuziki naimba nitakavyo sio lazima niruke ruke’ Alisema Linnah Sanga akizungumza na mtandao wa www.cloudsfm.co.tz

Amber VIDEO: Rutty Afunguka Ukweli Kuhusu Video ya Ngono Akishiriki Mapenzi na Wanaume Wawili

$
0
0
Amber Rutty Afunguka Ukweli Kuhusu Video Yao Ya Ngono Na Mabantu Video imesambaa akiwa kitandani na wanaume wawili wakifanya yaoBreaking News: Form Five Second Selection 2018/2019SPOTI TV SEPTEMBER 06, 2018Breaking News: Form Five Second Selection 2018/2019 Form Five Second Selection 2018 is out. Use the links below to read the anno...APPLY NOW

Dah!!! Hamisa Mobetto hadi USA kwa ex wa Rick Ross

$
0
0
Mwanamitindo Hamisa Mobetto amechukua tena headlines baada ya kupostiwa na mpenzi wa zamani wa rappa Rick Ross kutokea Marekani Lira Mercer na kuandika maneno yanayoashiria kuwa wanauhusiano wa karibu na watakutana hivi karibuni Marekani.Hamisa Mobetto ameonekana kupata dili mbalimbali hivi karibuni ikiwemo na kuwa balozi na nyingine nyingi , kupostiwa na mwanadada huyo wengi wamehoji na kujiuliza kuhusu ukaribu wao? na je ataenda Marekani kupata dili nyingine au kukutana kirafiki?Kupitia ukurasa wa instagram wa Lira ameandika “Mwanangu Hamisa  Mobetto anakuja kutembea Marekani hivi karibuni #AfrikaMashariki” Baada ya muda Hamisa Mobetto alimjibu na kusema “Nina shahuku mpenzi “Hamisa Mobetto na yeye alimpost mwanadada huyo kupitia ukurasa wake wa instagram na kuandika “Siwezi kusubiri kukuona “

Ujumbe wa Zari Waibua Hisia Tofauti Sakala la Hamissa Mobetto

$
0
0
Mashabiki wengi wameupokea kwa furaha ujumbe wa Zari the Bosslady kwa kile wanachoamini ujumbe huo unamlenga Hamisa Mobetto.Zari The Bosslady ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza kuwa; 'Usimpe mtu yeyote nguvu ya kuchagua kati yako na mtu mwingine... kama hukubaliki, ondoka na usiangalie nyuma na wala usimweleze mtu. Situmi chochote zaidi ya upendo kwako , Sasa futa machozi na urekebishe,'."Never give anyone the power to 'choose' between you and someone else. If they can't decide, decide for them. Walk it away and never look back. Go where your celebrated. Don't even explain i to anyone, your journey is yours. NOBODY has to understand it but YOU. Sending nothing but love you sis in TZ, Now wipe those tears and fix that.Ujumbe huo wa Zari unakuja ikiwa ni hivi karibuni Hamisa Mobetto ameingia kwenye shutuma nzito kwa kile kinachodaiwa kuwa alikuwa akipanga njama za kumloga Diamond Platnumz na familia yake.Zari the Bosslady aliwahi kuingia kwenye vita  kali ya maneno na Hamisa Mobetto baada ya Hamisa kuzaa na Diamond wakati akijua kwa wakati huo alikuwa kwenye mahusiano na Zari na tayari walikuwa wameshapata watoto wawili.

Sam Ikwae: Afuga ndege wenye thamani kama kivutio Mombasa Kenya

$
0
0
Sam Ikwae kutoka Mombasa Kenya ameanzisha mradi wa kuwafuga ndege wakiwemo kuku kutokanana umaridadi wao wenye thamani ya hadi $700

Kocha Simba ampa agizo moja tu Salamba

$
0
0
Kocha wa Simba Patrick Aussems amekaririwa akisifu kiwango cha Salamba lakini akamtaka ajibidiishe zaidi.

Boban ampagawisha mzungu Lyon

$
0
0
Boban alionekana akijituma uwanjani huku Lionel akionekana kushangazwa na kiwango cha kiungo huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars.

Key quotes from Woodward book, NYT op-ed assailing Trump

$
0
0
Woodward describes Trump regularly insulting key members of his team.

What Lissu misses one year after ‘assassination’ attempt

$
0
0
Recuperating Singida East MP (Chadema) Tundu Lissu said yesterday that he was homesick as he marks one year since surviving an “assassination” attempt in Dodoma.

MAGUFULI ATOA SABABU TANO ZA KUMUENZI NYERERE

$
0
0
  Na Andrew Msechu RAIS Dk. John Magufuli ametaja sababu tano za kumfanya amuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, huku akitaka pia wake za viongozi kujifunza kwa mama Maria Nyerere, ambaye amedai amekuwa mfano wa kuigwa kwa kutojikweza. Akizungumza na wananchi wa Butiama, Rais Magufuli alisema mji huo una historia ya pekee kwa kuwa Nyerere alizaliwa hapo na kukulia hapo, kisha kusomea hapo kabla hajaenda mikoa mingine na hata baada ya kufariki dunia alizikwa hapo.   SABABU ZA KUMUENZI NYERERE Rais Magufuli alisema Nyerere anastahili sifa kwa kuwa hakuwa mtu wa kujikweza na aliyependa kusuluhisha migogoro ya ndani na nje. Alisema Nyerere anastahili kuenziwa kwa sababu mbali na kuleta uhuru wa nchi, alisaidia kwa kiasi kikubwa kuasisi na kusababisha muungamo wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania ambayo sasa inaheshimika duniani hadi leo. “Lakini zaidi Mwalimu Nyerere alishiriki kusaidia kupatikana uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika ambazo leo zinajivunia kazi yake aliyoifanya. Huyu ni shujaa aliyewatumikia Watanzania na hatimaye akaamua kupumzika Butiama. “Watu wa Butiama wanaweza kuliona hilo ni jepesi na inawezekana wengine wakabeza, lakini wana bahati kuzaliwa hapa na wakumbuke kwamba historia ya kweli ya taifa la Tanzania ndipo ilipoanzia,” alisema. Rais Magufuli alisema kutokana na heshima ya Baba wa Taifa, atahakikisha ndoto yake (Nyerere) ya ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Stigler’s Gorge iliyokuwepo tangu mwaka 1975, ataitimiza na mradi huo utakapokamilika utaitwa Nyerere Gorge lengo likiwa ni kumuenzi mwasisi huyo wa taifa.   AMZUNGUMZIA MAMA MARIA Akimzungumzia mama Maria Nyerere, alisema mjane huyo wa Mwalimu ni mama tofauti ambaye tabia yake haijabadilika tangu alipokuwa na Nyerere hadi leo, tofauti na baadhi ya wake wa viongozi wengine ambao alisema wakati mwingine hata kuwasogelea unaogopa. Alisema ni matumaini yake kwamba akina mama wengi watajifunza tabia yake, kwa kuwa kuna wengine hata akiolewa tu na mwendesha daladala anabadilika, mwingine akipata mtu mwenye duka tu hasalimu majirani, lakini mama Nyerere amekuwa mama wa taifa. “Wake wa viongozi wengi wanatakiwa wajifunze kwako. Nimeona wake wa viongozi wengi, wengine hata huwezi kuwagusa ila wewe uko hivyo hivyo, kama ulivyoletwa na Mungu duniani na ni kwa sababu ya malezi mazuri, ndiyo maana ninajivunia kuzungumza kwa heshima kubwa nikiwa hapa Butiama,” alisema. Awali, Rais Magufuli alieleza kushangazwa na mji huo wa Butiama kwamba pamoja na sifa zote za kuwa kitovu cha historia ya taifa, bado hakuna maji ya uhakika. Alisema kwa kujali na kuheshimu historia ya Butiama, atahakikisha kunakuwa na maji ya uhakika na barabara za uhakika. Alikumbushia agizo lake la kuhakikisha Shule ya Msingi Mwisenge ambayo alisoma Mwalimu Nyerere inakarabatiwa na kujengewa uzio. Alimwagiza Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo kuhakikisha anafanya kila liwezekanalo, hata kama ikiwa ni kuhamisha fedha kutoka maeneo mengine ili shule hiyo ikarabatiwe. Alimweleza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha anamaliza matumizi ya Sh milioni 400 kabla ya kuomba nyingine.   MIGOGORO YA ARDHI Akizungumzia migogoro ya ardhi katika eneo hilo, Rais Magufuli alieleza kusikitishwa nayo akisema Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa kusuluhisha matatizo kama hayo na kwamba akifufuka leo atawashangaa watu wa Mara. Alisema katika Wilaya za Butiama, Bunda na Serengeti kuna vijiji vinagombania mipaka wakati viko katika mkoa mmoja wa Mara, pia ipo migogoro baina ya vijiji vilivyo katika wilaya moja na migogoro ya mtu na mtu. “Mambo mengine yanashangaza, kuna migogoro baina ya vijiji vilivyo katika wilaya na mkoa mmoja, kwanini wananchi wenyewe wasizuie kutokea kwa migogoro hii, mbona Baba wa Taifa alizuia migogoro mingi na hadi sasa taifa linaheshimika kwa kazi yake ya kusuluhisha na kumaliza migogoro ndani na nje?” alihoji. Aliwaagiza viongozi wakiwamo wakuu wa wilaya wakae na maofisa ardhi na kuhakikisha migogoro hiyo inamalizika kabla haijafika kwake na kwamba iwapo kiongozi ataendelea kuwapo katika eneo lenye migogoro maana yake ameshindwa kutawala. Alisema kwa kuwa wamepewa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, sheria ya ardhi na madaraka kwa mujibu wa katiba, hivyo wasikubali kukaa mahali ambako migogoro inaedelea kuwapo na kuwafanya watu washindwe kufanya shughuli zao.

Mwalimu afariki akisimamia mtihani

$
0
0
MWALIMU wa Shule ya Msingi Kisumba, Kalambo mkoani Rukwa, Lusekelo Mwakyesa (47), amefariki dunia akiwa darasani wakati akisimamia mtihani wa darasa la saba.Tukio hilo lilitokea juzi saa 9:30 alasiri katika Shule ya Msingi Mkapa iliyoko katika kijiji cha Kateka, kata ya Matai wilayani Kalambo.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alisema Septemba 3 majira ya asubuhi, mwalimu huyo alikwenda katika kituo chake cha kazi na kuomba ruhusa kwa Mwalimu Mkuu, Athuman Rashid, kuwa anahisi anaumwa malaria, hivyo anataka kwenda kununua dawa.Alisema siku iliyofuata, mwalimu mkuu huyo alimuuliza mwalimu huyo kama ataweza kwenda kusimamia mitihani ya darasa la saba katika kituo alichopangiwa na kusema anaweza.Aidha, alisema siku hiyo mwalimu huyo  alifika katika eneo ambalo wasimamizi wote walielekezwa kufika ili wapewe maelekezo na waliulizwa kama kuna msimamizi ambaye ana matatizo ya kiafya na hakuna aliyejitokeza, hivyo walipelekwa katika vituo vyao.Kamanda Kyando alisema juzi Mwakyesa alifika katika chumba cha mtihani na kuendelea kusimamia wanafunzi. Alisema asubuhi alimaliza mtihani wa kwanza na kupumzika kwa ajili ya mtihani wa mchana.Aliporudi katika chumba cha mtihani, alisema mwalimu huyo alitoa maelekezo yote kwa wanafunzi na kugawa karatasi za mitihani na za kujibia maswali na alipomaliza alikwenda kukaa katika kiti alichoandaliwa ili apumzike huku akiendelea kuwasimamia wanafunzi hao.“Baada ya kukaa, aliinama kama amejilaza katika meza iliyokuwa mbele yake kwa muda mrefu bila kuinua kichwa ndipo mmoja wa wanafunzi, Joel Mwajungwa, aliona maji yakitiririka kutokea miguuni kwa msimamizi huyo kitendo kilicho mshtua na kutoka nje kumwita mgambo aliyekuwa akilinda usalama katika maeneo ya shule,” alisema Kamanda Kyando.Alisema baada ya mgambo huyo kuingia darasani na kumtingisha, msimamizi huyo hakuamka na alipoangalia yale maji alibaini kuwa ni haja ndogo na kutoa taarifa kwa msimamizi mkuu aliyefika na gari na kumpeleka katika kituo cha afya cha Matai kwa ajili ya matibabu.Kwa mujibu wa Kamanda Kyando, walipofika kituo cha afya walipokewa na mganga wa zamu, Chapanga Chapanga na alimfanyia uchunguzi na kubaini kuwa alikwishafariki dunia.Alisema walipokagua katika begi lake walikuta dawa aina tano ambazo ni Aluu, Panadol, Piriton, NTZ na Tsonizide na inasadikika kuwa mwalimu huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>