Serikali imewataka wananchi wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi waliokuwa wamefungua kesi na baadaye kushindwa waendelee kuheshimu mipaka ya Msitu huo huku Chama cha Mapinduzi kikiangangalia namna bora ya kuwasaidia.Hatua hiyo inakuja kufuatia Wananchi hao waliokuwa na mgogoro wa Ardhi ndani ya Msitu huo kufungua kesi mwaka 2017, kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na maamuzi ya shauri la madai hayo yaliipa serikali ushindi, baada ya wananchi hao kushindwa kuonyesha ushahidi wa umiliki wa ardhi ikiwa ni ushahidi wa manunuzi na urithi wa ardhi hiyo katika Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi, Akizungumza kwenye mkutano na wananchi hao katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi amewaambia wananchi hao kuwa hawana haki kwenye ardhi hiyo kwa mujibu wa hukumu iliyotoka, Aliongeza kuwa mipaka ya msitu huo ipo sahihi na si vinginevyo hali iliyopelekea wananchi hao kushindwa kukata rufaa. Hata hivyo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amejipa siku 30 kuangalia namna ya kuwasaidia wakazi hao walioshindwa kesi. Ameongeza kuwa tayari ameshaunda kamati iliyopewa muda wa miezi miwili na tayari imeshamaliza mwezi mmoja na hivyo itatoa majibu ndani ya siku 30 lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi hao ambao kisheria walishindwa kesi."Mgogoro huu ulishafika mahakamani na uamuzi ukatolewa kuwa mmevamia hilo lipo wazi na sisi hatupingani na uamuzi wa mahakama."Ila kwa kuwa nyie ni wananchi wetu, CCM imeamua kununua kesi, sio kwa maana ya kupinga mahakama Bali ni kwa kuangalia tunawasaidia vipi," alisema Mhe. LukuviKwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amesema wizara yake haina tatizo na wakazi hao zaidi ya kuhakikisha msitu huo uko salama.Amesema katika kipindi ambacho msitu huo ulivamiwa athari kubwa zilijitokeza."Msitu huu tunaweza kusema ndio mapafu ya Dar, sasa ukivamiwa kwa kuwekwa Makazi au shughuli za kibinadamu mambo yanakuwa mabaya,”Tunategemea tupate hewa nzuri kutoka huku lakini wao walivamia na kutengeneza hewa chafu. Sisi tunachosimamia ni kuhakikisha msitu unatunzwa na kubaki kuwa msitu,"amesema.Baadhi ya wawakilishi wa kundi hilo la wananchi waliokuwa wamevamia msitu huo wameeleza kuwa wanachotaka ni kuonyeshwa mipaka ya kitaalam ya unapoanzia msitu huo."Hatupingani na mahakama wala wizara sisi tunataka wataalam wa wizara ya ardhi waje wafanye vipimo na kutuonyesha kitaalam ilipo mipaka," amesema Jackson Rwehumbiza.Akizungumza kuhusu msitu huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo alisema, Mwaka 1954 serikali ilianzisha Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi wenye ukubwa wa hekta 4,860, kwa Tangazo la Serikali Na. 306 la mwaka 1954 na ramani Jb 196 ya mwaka 1954 kwa kutambua umuhimu wake.Profesa Silayo anasema licha ya umuhimu wake Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na wananchi wanaoishi kuzunguka msitu huo na serikali ilifanya zoezi la kuwaondoa mwaka 1998,2003,3007,2011 na 2014.Msitu huu upo katika Wilaya ya Kisarawe na upande wa mashariki ndiyo mpaka kati ya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani na wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es Salaam. MWISHO
↧
Waziri Lukuvi Na Waziri Hasunga Wazidi Kusisitiza Wananchi Kuheshimu Mipaka Ya Msitu Wa Kazimzumbwi ....Ni Baada ya Kushindwa Kesi Mahakamani
↧
Gigy Money Afichua Siri ya Kutoka Kimapenzi na Mwambaji wa WCB Lava Lava
Msanii wa muziki kutoka Tanzania, hitmaker wa wimbo 'Nampa Papa', Gift Stanford a.k.a Gigy Money amefichua kuwa amekuwa kwenye mahusiano na msanii wa muziki kutoka Lebo ya WCB Wasafi, @iamlavalava.Katika video waliyoonekana katika ishara za uwepo wa mahaba kati yao, Gigy aliandika ujumbe kwenye post ya video hiyo kuwa "Tumeamua kuweka wazi tumechoka kujificha". Je, unahisi Lava Lava sasa hana Gundu tena? >Soma na hii ➤Africa Initiative for Governance (AIG) Scholarships 2019/2020 for Study in the University of Oxford, UK (Fully Funded)
↧
↧
Bondia wa Kenya Fatuma Zarika ahifadhi ubingwa wa dunia wa WBC uzani wa super-bantam
Bondia wa Kenya Fatuma Zarika ahifadhi ubingwa wa dunia wa WBC uzani wa super-bantam
↧
Several injured in Paris knife attack
Police have launched an investigation into a stabbing in Paris's 19th district. The attack left at least four people in critical condition.
↧
AICT church speaks on killing of choir member
The African Inland Church of Tanzania (AICT) hopes that justice will be served in the death of its choir member, Ms Miriam Charles, 26, stressing they will leave the matter to police.
↧
↧
Minister: Arrest ill-fated lorry driver
The deputy minister for Home Affairs, Mr Hamad Masauni, has ordered the arrest of the owner of a lorry, which was involved in a tragic accident, which left 15 people dead and 15 other injured.
↧
Government to form task force to curb invasive species
The government will form a task force to lay down strategies on how to address the problem of invasive plant and animal species.
↧
JULIO AJITOSA UCHAGUZI MSIMBAZI
NA ZAITUNI KIBWANA
KOCHA na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amedhamiria kuchukua fomu ili kuwania moja ya nafasi katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Novemba 3, mwaka huu.
Akizungumza na BINGWA jana, Julio alisema baadhi ya wanachama wa Simba wamekuwa wakimshawishi kugombea nafasi yoyote kwenye uchaguzi huo kutokana na uzoefu alionayo.
“Nitachukua fomu kama nitaona waliojitosa kwanza, kuna baadhi ya wanachama wamejitokeza kunishawishi kufanya hivyo, bado naendelea kuvuta kasi kuona kama msukumo utakuwa mkubwa nitajitosa kuchukua fomu.
“Si lazima kuchukua fomu kuwania nafasi za juu kama urais japo nina kigezo cha kugombea nafasi hiyo, ninachoamini ni kuwa naweza kuiletea Simba mafanikio hata nikitumikia nafasi ya ujumbe,” alisema.
Wakati Julio akiyasema hayo, naye mjumbe wa zamani wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, Swedi Mkwabi, amesema atachukua fomu kuwania nafasi katika uchaguzi huo.
“Bado siku zipo ila nitachukua fomu kuwania nafasi katika uchaguzi huu ambao wanatafutwa wajumbe sita pekee wa kuingia kwenye bodi ya wakurugenzi,” alisema.
Mpaka jana wanachama 10 ndio wamejitosa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.
Akizungumza na BINGWA jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Stephen Ally, alisema kesho ndio siku ya mwisho ya kutolewa kwa fomu hizo.
“Mchakato unaenda vizuri mpaka sasa wanachama 10 tu ndio waliochukua fomu, japo siwezi kuwataja majina kwa kuwa tulikubaliana kutaja majina yote baada ya mchakato mzima kumalizika siku ya kesho,” alisema Ally.
Licha ya kugoma kutaja majina hayo, taarifa kutoka Simba zinadai kuwa Kaimu Rais, Salum Abdallah ‘Try Again’ huenda akajitosa kuwania nafasi hiyo huku Makamu wake, Iddi Kajuna, akiwa tayari kachukua fomu ya kutaka ujumbe kwenye uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unatafuta wajumbe sita watakaoingia kwenye bodi ya wakurugenzi inayosimamiwa na mfadhili, Mohammed Dewji ‘Mo’.
The post JULIO AJITOSA UCHAGUZI MSIMBAZI appeared first on Bingwa.
↧
SIRI NZITO MO IBRA, MBELGIJI SIMBA
NA WINFRIDA MTOI
KUNA siri nzito imejificha nyuma ya kiwango cha juu kilichoonyeshwa na Mohammed Ibrahim ‘Mo Ibra’ wa Simba katika mchezo wao wa juzi wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Simba ilishinda mabao 4-2, huku Mo Ibra akifunga moja na kwamba kiwango chake kiliwakosha mno mashabiki wa Simba.
Lakini kiwango cha Mo Ibra aliyekuwa akiwatoa udenda Yanga, kilichangiwa kwa kiasi kikubwa na Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems.
Unajua ni vipi? Siku chache kabla ya mchezo huo wa juzi, BINGWA lilimshuhudia Mbelgiji huyo akimfuatilia kwa karibu mno Mo Ibra wakati wa mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.
Mara nyingi, Aussems alionekana kumwita Mo Ibra pembeni na kuzungumza naye na kuna wakati alilazimika kusimamisha mazoezi na kumwelewesha baadhi ya vitu.
Na hatimaye jitihada za Mbelgiji huyo zimejibu kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na Mo Ibra juzi.
Lakini mbali ya kiungo mshambuliaji huyo, pia kuna kijana aliyetua Msimbazi msimu huu akitokea Majimaji ya Songea ambaye naye ‘treni limewaka’.
Huyo si mwingine, bali ni mshambuliaji, Marcel Kaheza, ambaye juzi naye alionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards, akifunga bonge la bao dakika chache baada ya kuingia uwanjani kipindi cha pili.
Kwa kiasi kikubwa, kung’ara kwa wawili hao, hasa Mo Ibrahim, kumeanza kuzua maswali kuwa ni nani atampisha fundi huyo katika kikosi cha kwanza cha Aussems? Ni John Bocco aliyefunga mabao mawili juzi, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi au Shiza Kichuya?
Tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mo Ibra na Kaheza, walikuwa wakikaa jukwaani kutokana na kukosa namba.
Baada ya mchezo wa juzi na AFC Leopards, Aussems aliweka wazi jinsi alivyofurahishwa na viwango vizuri vilivyoonyeshwa na wachezaji wake ambao walikuwa hawapati nafasi.
“Wachezaji wangu leo (juzi) wamejitahidi kuonyesha kiwango kizuri, makosa kwenye mpira hayaishi, lakini walichokifanya ni kitu kizuri, walikuwa hawapati nafasi ila uwezo wao umeonekana ni mkubwa,” alisema.
Alisema kwa sasa akili yake ameielekeza katika mechi yao ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC na kwamba wachezaji wake waliokuwa kwenye timu za taifa wanatarajia kurejea kikosini ili kuendelea na programu zao.
Nyota wa Simba waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa ni Okwi (Uganda), Cletus Chama (Zambia), Aishi Manula (Tanzania) na Kagere (Rwanda).
Hadi sasa Simba wameshacheza mechi mbili za ligi, wakijikusanyia pointi sita baada ya kushinda zote dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.
The post SIRI NZITO MO IBRA, MBELGIJI SIMBA appeared first on Bingwa.
↧
↧
ZAHERA BONGE LA MAFIA
NA MWANDISHI WETU
*Awavuta Yanga mastraika wawili, beki hatari wa DR Congo
*Asema akiwapata, hakuna ‘paka’ yeyote wa kuisumbua Yanga 2018/19
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amekiangalia kikosi chake na kubaini kinahitaji kuongezewa nguvu na hivyo kupiga hodi ndani ya timu ya Taifa lake, DR Congo na kufanikiwa kupata vifaa vya maana.
Zahera alikuwa na kikosi cha DR Congo tangu wiki iliyopita kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Liberia kwenye Uwanja wa Samuel Kanyon Doe Sports, mjini Monrovia jana.
Mchezo huo uliopangwa kuanza saa 1:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ulikuwa ni muhimu mno kwa DR Congo kwani ushindi ungeiwezesha kuongoza Kundi D kwa kufikisha pointi sita.
Akizungumza na BINGWA juzi, Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa DR Congo, alisema kuna wachezaji waliopo katika kikosi hicho cha nchi yake ambao anaamini wakitua Yanga, hakuna timu itakayowasumbua Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Katika timu ya Taifa ya DRC, kuna starika wazuri sana na hata mabeki, lakini wote wanacheza nje ya Congo, wapo wanaotoka Ulaya na timu nyinginezo za Afrika.
“Nimezungumza na wachezaji wengi tu ili waje Yanga, lakini tatizo ni mishahara yao, wapo wanaolipwa zaidi ya euro 50,000 (Sh mil 130) na wengine wanaocheza TP Mazembe au Vita Club ni kati ya USD 5,000 (Sh mil 11) na 8,000 (Sh mil 18) au chini ya hapo. Sasa kwa mishahara hiyo ni vigumu kukubali kuja Yanga,” alisema Zahera.
Alisema iwapo atajitokeza mtu Yanga kuwa tayari kutoa fedha, ana uwezo wa kuiletea timu hiyo wachezaji wa kiwango cha juu wa idara zote, kuanzia mabeki, viungo na hata washambuliaji.
Aliwataja wachezaji waliopo DR Congo ambao wapo tayari kutua Yanga iwapo Wanajangwani hao watafika bei kuwa ni washambuliaji, Ben Malango na Elia Meschak (TP Mazembe), Cedric Kilua (SM Sanga Balende) na beki Ngonda Muzinga (Vita Club) na wengineo wengi.
Kikosi cha Yanga cha sasa kina mshambuliaji mmoja tu wa kiwango cha juu ambaye ni Herieter Makambo kutoka DRC, huku Matheo Anthony akiwa bado hajawateka mashabiki wa timu hiyo kama ilivyo kwa kinda Yusuph Mhilu, Pius Buswita na Emmanuel Martin.
Kwa upande wa viungo washambuliaji, kuna Ibrahim Ajib, Mrisho Ngassa na Deus Kaseke, huku viungo wakiwa ni Feisal Salum ‘Fei Toto’, Pappy Tshishimbi (DRC), Said Juma Makapu, Rafael Daudi, Said Mussa na Maka Edward.
Katika safu ya ulinzi, Yanga ipo vizuri katikati japo nako kunahitaji kuongezewa nguvu kama ilivyo upande wa kulia na kushoto.
Yanga ilishindwa kufanya usajili wa kishindo baada ya kumalizika kwa msimu uliopita kutokana na wimbi la ukata linalowakabili ambapo kwa sasa mashabiki na wanachama wamekuwa wakisubiri kwa hamu Uchaguzi Mkuu kuona iwapo watapata viongozi watakaokuwa na ushawishi wa kuyavuta mataji zaidi Jangwani.
The post ZAHERA BONGE LA MAFIA appeared first on Bingwa.
↧
Muswada uliokwama kwa kukosa akidi kupitishwa leo bungeni
Muswada wa Sheria Mbalimbali namba 2 wa Mwaka 2018 ambao uliachwa Ijumaa wiki iliyopita kutokana na kukosekana kwa akidi inayohitajika kikanuni, leo utarudishwa kwa ajili ya kupigiwa kura ya uamuzi.
↧
Kinachotekelezwa ni mpango wa Taifa sio ilani ya CCM - Chadema
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema kitendo cha CCM kujinadi kuwa kinatekeleza miradi ya maendeleo kupitia ilani yake wakati ni mpango wa maendeleo wa Taifa ni upotoshaji.
↧
Mabasi yaendayo mikoani kuanza safari saa 11 alfajiri
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditye amesema baada ya wiki mbili mabasi yanayoenda mikoa mbalimbali nchini yataanza safari zake saa kumi na moja alfajiri.
↧
↧
Ajali yawapeleka mawaziri Mbeya
Siku mbili baada ya kutokea kwa ajali iliyosababisha vifo vya watu 15 na majeruhi 15 jijini Mbeya Ijumaa iliyopita, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusuph Massauni ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa Lori lililosababisha ajali na ili athibitishe kama gari lake lilistahili kuwapo barabarani na kama dereva wake alikuwa na ujuzi unaokubalika kisheria kuendesha gari.
↧
Magufuli: Hii ndiyo sababu ya kumteua Mpina
Rais John Magufuli ametaja sababu ya kumteua Luhaga Mpina kuwa waziri wa Mifugo na Uvuvi, kwamba ni kwa kuwa anatoka kwenye jamii ya wafugaji.
↧
Dili tamu zilizogoma kutiki klabu za Big Six ligi kuu England
KWENYE Big Six ya Ligi Kuu England upinzani haupo tu kwenye kusaka ubingwa wa taji hilo, bali hata kwenye kufungua pochi kunasa wachezaji mahiri kwenye vikosi vyao limekuwa ni jambo linalofanyika kwa ushindani mkali.
↧
Zidane ataja wachezaji wake akitua Man United
HABARI ndio hiyo. Zinedine Zidane ameshaorodhesha majina ya wachezaji ambao atawasajili atakapotua Manchester United kama atapewa kibarua hicho kinachoshikiliwa na Jose Mourinho kwa sasa.
↧
↧
Hata Rudiger naye kanogewa na Sarri
BEKI wa kati wa Chelsea, Antonia Rudiger amekiri wachezaji wote wa kikosi hicho cha Stamford Bridge wamepagawa na soka la kupiga mpira mwingi linalofundishwa na Kocha Maurizio Sarri klabu hapo kwa sasa.
↧
Kane amnunia refa kisa England kupigwa
STRAIKA wa England, Harry Kane amekuwa mkali na kudai refa amechangia kuwafanya wachapwe na Hispania katika michuano mipya kabisa huko Ulaya, inayofahamika kama Uefa Nations League.
↧
Dybala mwili upo Juve, moyo upo Madrid
STAA wa Juventus, Paulo Dybala ameripotiwa kutamani sana kujiunga na Real Madrid kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi kama sio Januari.
↧