Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live

Mbunge ataja mali mpya za Paul Makonda

$
0
0
Sakata la mali zinazodaiwa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeendelea kulitikisa bunge baada ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) kuongeza nyingine.

Klopp na mastaa wake wanacheka tu mtaani

$
0
0
KOCHA, Jurgen Klopp anakula bata tu la kikosi chake cha Liverpool.

Wanyama azuia ubingwa Chelsea

$
0
0
REKODI zinaibeba Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspur watakapomenyana nao leo Jumamosi huko Anfield.

Rescuers Save Some Stranded Whales in New Zealand; New Pod Runs Aground

$
0
0
A new pod of 240 whales swam aground at a remote New Zealand beach Saturday just hours after weary volunteers managed to refloat a different group of whales from an earlier mass stranding.   In total, more than 650 pilot whales have beached themselves along a 5 kilometer (3 mile) stretch of coastline over two days on Farewell Spit at the tip of the South Island. About 335 of the whales are dead, 220 remain stranded, and 100 are back at sea.   Department of Conservation Golden Bay Operations Manager Andrew Lamason said they are sure they’re dealing with a new pod because they had tagged all the refloated whales from the first group and none of the new group had tags.   The news was devastating for hundreds of volunteers who had come from around the country to help with the initial group of 416 stranded whales that was found early Friday, many of them already dead.  Volunteers not giving up Volunteers are planning to return Sunday to help refloat as many healthy whales as they can.   Lamason said about 20 of the new group were euthanized by conservation workers because they were in poor condition and more would likely need to be killed Sunday.   Rescuers had been hopeful earlier Saturday after efforts to refloat the initial group of whales had gone well, following a frustrating day Friday. Lamason said improved weather and crystal clear water helped with the latest rescue attempt. He said all the surviving whales were refloated, and about 100 volunteers formed a human chain in the water to prevent them from beaching again.   He said volunteers were warned about the possibility of stingrays and sharks, after one of the dead whales appeared to have bite marks consistent with a shark. He said there had been no shark sightings. Carcass disposal  With the rescue effort now paused, officials are beginning to turn their attention to the grim task of disposing of hundreds of carcasses.   Lamason said one option was to tether the carcasses to stakes or a boat in the shallow tidal waters and let them decompose. The problem with towing them out to sea or leaving them was that they could become gaseous and buoyant, and end up causing problems by floating into populated bays.   Farewell Spit, a sliver of sand that arches like a hook into the Tasman Sea, has been the site of previous mass strandings. Sometimes described as a whale trap, the spit’s long coastline and gently sloping beaches seem to make it difficult for whales to navigate away from once they get close.   There are different theories as to why whales strand themselves, from chasing prey too far inshore to trying to protect a sick member of the group or escaping a predator.   New Zealand has one of the highest rates of whale strandings in the world, and Friday’s event is the nation’s third-biggest in recorded history. The largest was in 1918, when about 1,000 pilot whales came ashore on the Chatham Islands. In 1985, about 450 whales stranded in Auckland.   Pilot whales grow to about 7.5 meters (25 feet) and are common around New Zealand’s waters. 

Ukame nchini Kenya sasa ni janga la kitaifa

$
0
0
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nchi yake inakabiliwa na janga la ukame na kulitangaza sasa ni tatizo la kitaifa.

SERENGETI BOYS ISAIDIWE KWA NGUVU ZOTE

$
0
0
TIMU ya soka ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, imefanikiwa kupata nafasi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Gabon, Aprili mwaka huu. Serengeti imepata nafasi ya kushiriki fainali  hizo baada ya Tanzania kushinda rufaa yake dhidi ya nchi ya Congo Brazzaville ambayo ilimtumia mchezaji aliyezidi umri, Langa Lesse Bercy, katika mchezo dhidi yao wa kufuzu kucheza fainali hizo. Watanzania tuna kila sababu ya kuhakikisha timu ya Serengeti Boys inapata maandalizi ili kufanya vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa wa Afrika katika mashindano hayo makubwa ya Afrika. Tayari Shirikisho la Soka Tanzania TFF, limeshatangaza kiasi cha fedha kinachohitajika  kuwa ni Sh bilioni moja kwa ajili ya maandalizi ya fainali hizo, ambapo ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki fainali hizo tangu kupata uhuru. Tanzania tuna haja ya kujivunia kupata nafasi ya kushiriki fainali hizo lakini vile vile inatupasa kuhakikisha timu hiyo inapata maandalizi mazuri, ili iweze kushiriki nichuano hiyo bila wasiwasi na kuweza kurudi nyumbani na kikombe hicho kwa kuwa naamini kwa uwezo waliouonyesha kwenye mechi za kufuzu hilo linawezekana. Sisi BINGWA tunaamini kwamba endapo Watanzania wote tutashirikiana katika maandalizi ya timu yetu, tuna kila sababu ya Tanzania kurudi na kombe la ubingwa wa Afrika na kuliletea sifa taifa letu, hivyo basi imefika wakati kwa watu wote kushirikiana pamoja kufanikisha mchakato huu. Tunafahamu soka la Tanzania linakabiliwa na mizengwe, hasa katika kipindi hiki cha  kukaribia uchaguzi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), lakini  uchaguzi huo usifanye tushindwe  kuisapoti  timu yetu ya Taifa ya Vijana, Serengeti Boys. BINGWA tunaamini kwamba kuisapoti si kwa fedha tu, michezo ipo mingi ambayo inaweza  kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri katika fainali hizo za Afrika, shime Watanzania, tushirikiane katika jukumu hili. Mungu ibariki Tanzania, Serengeti Boys   The post SERENGETI BOYS ISAIDIWE KWA NGUVU ZOTE appeared first on Bingwa.

LWANDAMINA AKOMAA NA PENALTI YANGA

$
0
0
NA SALMA MPELI KOCHA wa Yanga, George Lwandamina, anafahamu udhaifu wa kikosi chake hicho linapokuja suala la mikwaju ya penalti, kwa kutambua hilo ameamua kutafuta ufumbuzi kwa kuwapika wachezaji wake kwa ajili ya kuhakikisha hawarudii makosa endapo  watalazimika kufika hatua hiyo. Yanga ambayo inaondoka nchini leo kwenda Comoro ambako itavaana na Ngaya FC katika pambano la raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, haina rekodi nzuri inapofika kwenye hatua ya mikwaju ya penalti. Tukio la hivi  karibuni ni pale Yanga ilipoondolewa na Simba katika nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi iliyofanyika Januari mwaka huu visiwani Zanzibar baada ya kuchapwa penalti 4-2. Pia Yanga iliondolewa kwa mikwaju ya penalti  raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mabingwa wa Misri, timu ya Al Ahly ya Misri. Janga hilo limeendelea hata katika  baadhi ya  mechi zake za  Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakikosa penalti kadhaa ambazo kama wangefunga zingeweza kuisaidia kuibuka na ushindi mnono. Rekodi hizo mbaya zinaonekana kumtisha kocha huyo wa zamani wa Zesco na Zambia na sasa ameamua kukomaa na wachezaji wake kuhakikisha wanakuwa tayari kwa mazingira yoyote  ikiwamo penalti. Katika mazoezi ya timu yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, BINGWA lilishuhudia wachezaji wote wa Yanga wakipiga mikwaju ya penalti huku kocha huyo akiwataka wale waliokosa kurudia zoezi hilo. The post LWANDAMINA AKOMAA NA PENALTI YANGA appeared first on Bingwa.

YANGA KUWAKABILI WACOMORO KWA TAHADHARI KUBWA

$
0
0
NA SAADA SALIM BENCHI la ufundi la Yanga limesema  timu hiyo inasafiri kwenda Comoro ikiwa na tahadhari kubwa ya kutowadharau wapinzani wao Ngaya FC. Yanga inasafiri leo kuelekea Comoro kwa ajili ya mchezo wao huo utakaochezwa kesho (Jumapili) Uwanja wa Moroni nchini humo. Akizungumza na BINGWA jijini jana, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema wamejizatiti kuhakikisha wanapambana kwa nguvu ili kuibuka na ushindi na kamwe hawawezi kuwadharau wapinzani wao hao. Alisema rekodi walizonazo zinaonyesha  wapinzani wao hao wamefanikiwa kutwaa vikombe vitatu katika kipindi kifupi kilichopita ambazo ni  Kombe la Ngazija, Super Cup na Champion Ship. “Hatujawahi kupata mikanda yao ya video (CD) kwa ajili ya kuwaangalia, kwa hiyo hatujajua mifumo wanayotumia lakini tunaenda na historia yao kwamba wamefanya vizuri kwa msimu uliopita na kushinda vikombe vinne huko kwao,” alisema. Mwambusi alisema kulingana na historia hiyo waliyopewa juu ya wapinzani wao, wameshtuka na kuhakikisha wako kamili na kuhitaji ushindi mkubwa katika mchezo huo. The post YANGA KUWAKABILI WACOMORO KWA TAHADHARI KUBWA appeared first on Bingwa.

KOCHA SIMBA ATAMBA KUITINGISHA GHANA

$
0
0
NA EZEKIEL TENDWA WAKATI Ligi Kuu nchini Ghana ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi  kesho, kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema atahakikisha anakipa ubingwa kikosi chake kipya cha Asante Kotoko. Loga ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili na kikosi hicho baada ya kugoma kuingia mkataba mpya na timu ya Inter Club ya nchini Angola aliyokuwa akiifundisha, amesema atahakikisha Kotoko inatisha nchini Ghana. Akizungumza na BINGWA kwa njia ya mtandao, Loga alisema kwa sasa anakisuka vilivyo kikosi chake hicho na kwamba anayo matarajio makubwa wachezaji wake watafanya kile anachowafundisha. “Matarajio yangu ni makubwa ndani ya timu yangu hii mpya, ninachoweza kusema ni kwamba, nataka kuona tukibeba ubingwa hapa Ghana na hilo linawezekana kabisa kutokana na maandalizi tunayoyafanya,” alisema. Alisema ataonyesha uwezo wake wa kufundisha katika kikosi hicho na ana uhakika msimu ujao kikosi hicho kitashiriki michuano mikubwa barani Afrika. The post KOCHA SIMBA ATAMBA KUITINGISHA GHANA appeared first on Bingwa.

Ujenzi wa vituo vya ‘Polisi Mobile’ mwendo wa kinyonga

$
0
0
Mpango wa Usalama wa Jamii (Polisi Mobile) uliozinduliwa na Rais John Magufuli, unasuasua kuwekwa katika maeneo mengine kutokana wadau wachache kujitokeza kuufadhili.

Ian Wright: Wenger aliniambia muda wake unakaribia kikomo Arsenal

$
0
0
Arsene Wenger amemwambia Ian Wright kwamba muda wake kama mkufunzi wa Arsenla unakaribia kikomo kulingana na mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal.

Mexico yawaonya raia wake US baada mwanamke kufurushwa

$
0
0
Serikali ya Mexico imewataka raia wake wanaoishi Marekani kuchukua tahadhari zaidi mbali na kuwasiliana kwa karibu na ubalozi wao kutokana na kauli za utawala mpya wa Bw. Trum

Polish Prime Minister Suffers Minor Injuries in Car Crash

$
0
0
Prime Minister Beata Szydlo suffered injuries in a car crash in southern Poland Friday and was flown by helicopter to Warsaw for medical tests, even though doctors and her spokesman said that she was not badly hurt.   The accident occurred shortly before 7 p.m. in the southern town of Oswiecim, which is Szydlo’s hometown. Szydlo, 53, was traveling in a convoy along the town’s main road when another car drove into her black Audi limousine, causing it to hit a tree.   The state broadcaster TVP published an image of the limousine with the front of the car bashed in. Prognosis good  Government spokesman Rafal Bochenek said Szydlo was in “good condition” but had been flown 350 kilometers (215 miles) by helicopter to a government hospital in Warsaw for further monitoring and tests.   The car that hit the prime minister’s vehicle was a small Fiat driven by a 21-year-old man who was sober, said Sebastian Glen, a police spokesman. Two security officers, one of whom was the car’s driver, were also taken to a hospital with injuries.   Dr. Andrzej Jakubowski, who examined Szydlo in the hospital in Oswiecim, a town of 40,000, said she was stable and conscious all the time and was talking and “very strong” given the trauma. Jakubowski said Szydlo suffered some injuries but that the prognosis is good.   Oswiecim is best known to the world by its German name, Auschwitz. It is the town where Nazi Germany ran the death camp in occupied Poland during World War II and today is the site of a memorial and museum that draws large numbers of visitors.   Poland’s interior minister called an emergency meeting with the leadership of the Government Protection Office, which protects and drives Szydlo and other top figures. Meanwhile, prosecutors also opened an investigation. String of accidents  It was the latest in a string of road incidents involving top state officials.   In November, several vehicles in a Polish government convoy collided during a state visit to Israel. Szydlo was not in one of those that collided, but two other Polish officials had minor injuries.   Separately, Defense Minister Antoni Macierewicz escaped uninjured from an eight-car collision in January.   In March 2016, a limousine carrying President Andrzej Duda skidded into a grassy ditch because of a punctured tire. Duda was unhurt. 

Tens of Thousands Rally in Jakarta Ahead of Election 

$
0
0
Tens of thousands of Indonesians descended on the capital Saturday to hear clerics urge them to vote for Muslim politicians in the city and district elections being held across the country next week. The crowd at Jakarta’s Istiqlal Mosque spilled over into the surrounding streets. The clerics in Jakarta want Muslims to vote out Basuki Tjahaja Purnama, the city’s Chinese Christian governor, who is on trial for blasphemy. Basuki’s political drama began in October when he dismissed his opponents who had cited a Quranic verse that warns against Muslims supporting nonbelievers. The embattled governor said Jakartans had “been lied to” by the verse in question and remarked, “If you feel you can’t vote for me because you fear you’ll go to hell ... no worries. That’s your personal right.” Basuki has since apologized and said he never intended to cause offense, but it has done little to placate many Muslims who are enraged that a Muslim-majority city is administered by a Christian. Saturday is the last day politicians can campaign before Wednesday’s vote. Indonesia is the world’s most populous majority Muslim nation and has a large Christian minority.  

RC Iringa Mwalimu Amina Masenza Aonya Watumishi Wanaokwepa Mazoezi.

$
0
0
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  mwalimu  Amina Masenza (wa tatu kushoto) akiongoza  mazoezi ya viungo katika  uwanja wa  samora  Leo wa  pili kushoto ni katibu  tawala wa mkoa  wa Iringa wamoja Ayubu DC  Iringa  Richard  Kasesela wa kwanza  kulia  akishiriki mazoezi ya  riadha kutoka  uwanja  wa Samora Washiriki wa  mazoezi  wakiwasili  ufisi ya  RC Iringa wakitokea  uwanja  wa  Samora Afisa  michezo mkoa wa Iringa Kenedy Komba  akiorodhesha  majina  ya wakuu wa Idara  walioshiriki mazoezi leo ni  kuwabana wamnaokwepa mazoezi Wanamazoezi  wakitoka  uwanja wa  samora Mkazi  wa Iringa  akiwa amebeba  pombe aina ya  komoni asubuhi ya  leo pombe  hii inatengenezwa kwa mahindi jambo  ambalo  serikali  ya  mkoa imepigamarufuku matumizi mabaya ya  chakula Mkazi  wa Iringa  akipishana na washiriki wa mazoezi huku  akiwa amebeba pombe ya  komoni inayotengenezwa  kwa mahindi RAS  Iringa na RC Masenza kulia  wakiwa katika mazoezi RC Iringa Amina Masenza  kulia  akiongoza mazoezi saa 12 asubuhi ya  leo Afisa  habari Manispaa ya  Iringa  Sima Bingilengi kushoto  akiwajibika Mwanahabari Manispaa ya  Iringa Janeth Matondo kulia pia  akishiriki mazoezi DC  Kasesela katikati wa  pili  kulia akiwa na wadau  wa  kwanza  kulia ni Geofrey  Mungai Mzee Vitus Mushi  akiwajibika mazoezini DC  Iringa  Richard Kasesela  wa  tatu katikati  kulia akiwa na mkurugenzi Manispaa ya  Iringa Dr  Wiliam na mwanasheria  wa  Iringa wa  pili kuliaNa MatukiodaimaBlog MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa mwalimu  Amina Masenza amewaonya  watumishi  wa serikali ambao wanakwepa  kushiriki mazoezi ya  pamoja katika  uwanja  wa  Samora  na  kuwa kuanzia sasa mtumishi atakayekwepa kushiriki  kubanwa .Alisema pamoja na kuwa mazoezi  hayo ni kwa ajili ya afya za kila mmoja kujikinga na maradhi  yanayosababishwa na  kutofanya mazoezi ila  bado mazoezi hiyo  ni  utekelezaji wa agizo la makamu  wa Rais kwa  kila mtanzania .Hivyo  alisema kutokana na baadhi ya  watumishi hasa  wanawake  kukwepa mazoezi hayo anaandaa mkakati wa kuwabana  watumishi  wote  wanaokwepa mazoezi kwa  kuitisha mazoezi  siku ya kazi ili wale  ambao  watashindwa  kufika watawajibishwa ."Naangalia  ni  siku gani  ambayo  itakuwa ni  siku ya kazi kama ijumaa ama siku  nyingine  yeyote  ambayo  nitaitisha mazoezi kuanzia ofisi  yangu  hadi  Samora kwa  kila mtumishi kushiriki na siku hiyo hata ofisini  watumishi  wakichelewa ni  sawa lengo  kuweza  kufanya mazoezi na kutekeleza agizo la  serikali ......nashangazwa  sana  awali  wanawake  ndio  ambao  walikuwa  wakifika kwa  wingi mazoezini  ila leo  hii idadi ya  wanawake  imepungua ukilinganisha na  wanaume ....nawashangaa sana wanawake  wanaokwepa mazoezi  wakati  ndio ambao  wanakula vitu  vyenye mafuta "Hivyo  alisema  kuanza sasa  kila mtumishi  wa serikali  lazima  kufika katika mazoezi na  utawekwa  utaratibu  wa  kuorodhesha majina kila idara  ya  watu  wanaoshiriki mazoezi .

Balozi Seif Awataka Mabalozi wa Tanzania Ubalozi Unahitaji Uadilifu na Ueledi Mkubwa Kuzingatia Heshima na Matakwa ya Taifa.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi akizungumza na kuwaaga Mabalozi Sita wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kuwakilisha Taifa Nchini Mbali mbali Duniani Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo {DRC} Balozi Paul Mella kwa niaba ya wenzake akimuahidi Balozi Seif  kwenda kutekeleza majukumu yao kwa bidii za kizalendo.Balozi Seif  akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania nchi za Nje mara baada ya kuzungumza nao na  kuwaaga rasmi kwenda kutekjeleza jukumu lao la Kidiplomasia.Kushoto ya Balozi Seif ni Balozi wa Tanzania Nchini Uswiss Dr. James Nsekela na kulia yake ni Balozi wa Tnaznia Nchini Uturuki Balozi Elizabeth  Kiondo.Picha na – OMPR – ZNZ.Na Othman Khamis OMPR.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema suala la kusimamia uhusiano wa Kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Mataifa Rafiki   Duniani ndio kazi ya msingi kwa Mabalozi wote katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.Alisema Kazi ya Ubalozi inahitaji uadilifu na ueledi mkubwa unaohitaji kuzingatia zaidi heshima na Matakwa ya Taifa yatakayopelekea kuimarika kwa huhusiano uliotukuka wa pande zote husika.Balozi Seif Ali Iddi alitoa angalizo hilo wakati akiwaaga Mabalozi Sita  walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kuiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani.Alisema Serikali  ya  Awamu zilizopita nyuma  iliwahi kulazimika kuwajeresha nyumbani  na wengine kuwafukuza kazi baaadhi ya Mabalozi  wa Tanzania baada ya kushindwa kuuheshimu Utumishi wao wa Kidiplomasia.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea matarajio yake ya mafanikio kwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamuhuri ya MKuungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wa kufanya upembuzi wa kina uliyoibuwa Watumishi hao wa Kidiplomasia watakaokuwa kioo chema cha Tanzania katika Mataifa waliyopangiwa kufanya kazi.Akigusia suala la Maendeleo ya Uchumi Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi aliwataka Balozi hao wanaoiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani kuvitangaza Visiwa vya Zanzibar  ambavyo kwa kiasi kikubwa vitaendelea kuzitegemea  Ofisi za  Mabalozi hao.Balozi Seif alisema Zanzibar hivi sasa inategemea kupata zaidi mapato yake kupitia sekta ya Utalii inayopata msukumo kutoka kwa Taasisi na Makampuni mengi ya nje hasa Taifa ya Italy.Alimuomba Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Balozi Samuel Shelukindo kuandaa mazingira ya kukutana na Uongozi wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni { UNESCO } lenye Makao Makuu yake Nchini humo kujadili na Wataalamu wake kuangalia mazingira ya kuyahami Majengo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao kwa kipindi kirefu uko chini ya hifadhi  ya Urithi wa Dunia.Balozi Seif alisema majengo mengi ndani ya Mji Mkongwe  hivi sasa hayako katika mazingira mazuri jambo ambalo Unesco ina wajibu wa kusaidia sambamba na kutoa ushauri badala ya kuwa wakali katika kuelekeza pekee.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Mabalozi hao wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani kwamba maeneo mengi ya Kihistoria  yaliyopo katika Visiwa vya Zanzibar ukiwemo Mji Mkongwe  ni chem  Chem ya kuimarika kwa mapato yake kupitia sekta ya Utalii.Balozi Seif Ali Iddi alimuagiza Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki Balozi Elizabeth Kiondo kufuatilia mahusiano na Mikataba iliyopo ya muda mrefu kati  Uturuki na Tanzania na Zanzibar kwa Ujumla.Alisema ipo mikataba mingi iliyokwishatiwa saini kati ya Uturuki na Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo ile kubwa ya Utalii ambayo inastahiki kufuatiliwa muelekeo na utekelezaji wake.Naye kwa niaba ya Mabalozi hao wa Tanzania Nchi mbali mbali Ulimwenguni, Balozi wa Paul Mella anayekwenda nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo { DRC } alimuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba watazingatia jukumu walilopewa na Taifa katika kutekeleza wajibu wao.Balozi Paul alisema Watanzania  wana haki ya kujenga matumaini makubwa kutoka kwa Kikosi hicho mahiri kinachoelekea katika eneo lake la uwajibikaji kuisimamia na kuitangaza Diplomasia ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kinana Aongoza Mazishi ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Hai Arnold Swai leo Katika Wilaya Hiyo Mkoani Kilimanjaro.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimfariji Baba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, Jonathan Swai, baada ya kumkabidhi rambirambi za CCM na Jumuia zake, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.  Arnold alifariki dunia katika ajali ya gari wakati akitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, Februari 5, 2017.Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimfariji Baba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, Jonathan Swai, baada ya kumkabidhi rambirambi za CCM na Jumuia zake, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo. Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimfariji Baba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, Jonathan Swai, baada ya kumkabidhi rambirambi za CCM na Jumuia zake, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiifariji familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kutoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimshukuru Nchungaji Andrew Munishi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya kuendesha misa ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kabla ya mazishi yaliyofanyka leo katika kijiji cha Mbweere, Kata ya Miasama wilayani humo.Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. JohnMagufuli, wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kutoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.Mwakilishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya TSN,  Isaya Mwaisembe atoa maneno ya rambirambi wakati wa kuagwa mwili wa marehemu Arnold Swai katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Hai mkoani Kilimanjaro. Arnold alikuwa Mwandishi wa habari wa TSN. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro,  Bahati Nyakiraria.Nchungaji Andrew Munishi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, akitoa neno la kiroho,baada ya kuendesha misa ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kabla ya mazishi yaliyofanyka leo katika kijiji cha Mbweere, Kata ya Miasama wilayani humo.Muombolezaji akionyesha huzuniWaziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Magembe akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wa misa hiyoMwenyekiti wa zamani wa CCM mkoawa Kilimanjaro, Vick Nsilo Swai, akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wa misa hiyo. TAFADHALI ENDELEA KUTAZAMA PICHA ZAIDI ZA MSIBA HUUKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na Waziri Magemebe wakati wa misa hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, na kutokakulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Deogratius Rutta, Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Iddi Juma na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick

‘WANAUME’ SITA VING’ANG’ANIZI LIGI KUU BARA

$
0
0
NA SALMA MPELI LIGI Kuu soka Tanzania Bara tunayoishuhudia imepitia katika vipindi tofauti na majina tofauti. Ligi hiyo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Ligi ya Taifa mara tu baada ya kuanzishwa mwaka 1965 kabla ya kubadilishwa na kuitwa Ligi Daraja la Kwanza na baadaye mwaka 1997 kubadilishwa tena na kuitwa Ligi Kuu Tanzania Bara. Simba na Yanga, ndizo timu kongwe zaidi katika ligi hiyo zikiwa zimefanikiwa kutwaa taji la ubingwa mara nyingi zaidi. Yanga ndiyo inaongoza ikiwa imefanikiwa kutwaa taji hilo mara 25, huku Simba ikifanikiwa kulibeba mara 18. Timu hizi hazijawahi kushuka daraja tangu zilipoanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965. BINGWA kupitia makaya haya linakuletea orodha ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambazo tangu zilipofanikiwa kupanda daraja hazijawahi kushuka licha ya changamoto  kadhaa zilizowahi kukutana nazo. Yanga SC Yanga ndiyo timu kongwe zaidi nchini, ilianzishwa mwaka 1935. Ilipoanzishwa ilikuwa ikijulikana kama New Youngs, ilipofika mwaka 1936 baadhi ya wachezaji wa timu hiyo walijiengua na kwenda kuanzisha timu nyingine iliyojulikana kama  Sunderland ambayo baadaye ilikuja kubadilishwa na kuitwa Simba ambayo wengi wetu tunaifahamu sasa ambayo ni mpinzani mkuu wa Yanga. Wachezaji waliobaki waliamua kubadili jina na kuitwa Young Africans. Tangu ilipoanza kushiriki Ligi Kuu Bara mwaka 1965, Yanga haijawahi kushuka daraja. Simba SC Timu hiyo ambayo awali ilikuwa ikiitwa Sunderland ilianzishwa mwaka 1936. Timu hiyo ilianzishwa na wale baadhi ya waliojitenga kutoka New Young ambao wengi wao walikuwa wasomi ambao walisisitiza wanataka mambo yao yaendeshwe kisomi. Waliungana na timu iliyokuwa inaitwa Eagle Night na katika miaka ya 1940 kabla ya kuibadilisha jina na kujiita Sunderland. Hapo ndiyo chimbuko la kuvaa jezi za rangi nyekundu kama ilivyo kwa timu ya  Sunderland ya England lilipoanzia kabla ya mwaka 1971 kubadilishwa tena na kuamua kuiita Simba. Simba imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara 18 na haijawaji kushuka tangu ilipoanzishwa na kuwa ni miongoni mwa timu zilizodumu. Azam FC Timu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara, Said Salim Bakhressa, ilipanda daraja na kuanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2007 ikiwa ni miaka mitatu tangu ilipoanzishwa na wafanyakazi wa viwanda vinavyomilikiwa na tajiri huyo mwaka 2004. Kabla ya kubadilishwa jina na kuanza kutumia Azam FC, timu hiyo ilikuwa ikifahamika kama Mzizima FC. Lengo la kuanzishwa kwa timu hiyo ni kuimarisha afya za wafanyakazi. Tangu ilipofanikiwa kupanda daraja  timu hiyo imekuwa ikishiriki mfululizo Ligi Kuu Tanzania Bara huku ikifanikiwa kutwaa mataji mbalimbali yakiwemo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Kombe la Kagame na Kombe la Mapinduzi. JKT Ruvu Ni miongoni mwa timu zilizofanikiwa kulinda hadhi yake kwa kuhakikisha haishuki daraja tangu ilipoanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Haijawahi kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini imekuwa ikifanya vizuri na mara kadhaa imemaliza msimu ikiwa kwenye nafasi tano za juu, ukiondoa misimu miwili iliyopita ambayo imeyumba. Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutoka kikosi cha 832, ilianza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2002. Kagera Sugar Timu hiyo ilianzishwa katikati ya miaka ya 80 wakati huo ikiitwa RTC Kagera ikimilikiwa na kampuni ya biashara ya Mkoa wa Kagera. Kutokana na kushuka kwa uchumi, wamiliki walishindwa kuiendesha timu hiyo na kuchukuliwa na wadau wa soka wa mkoa huo ambao waliamua kuibadili jina na kuiita Kagera Shooting Stars. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 timu hiyo ilichukuliwa rasmi na kampuni ya sukari na kufanikiwa kupanda Ligi Kuu mwaka 2004. Kagera Sugar ni miongoni mwa timu ambazo hazijawahi kushuka daraja tangu ilipoanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, pia ni miongoni mwa timu zenye ushindani mkubwa katika ligi hiyo ikiwa tishio kwa vigogo, Simba na Yanga. Mtibwa Sugar           Mtibwa ni miongoni mwa timu zenye historia nchini kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara hiyo ilikuwa mwaka 1999 na mwaka 2000. Kama ilivyo kwa Kagera Sugar, Mtibwa Sugar pia inamilikiwa na Kampuni ya Sukari ya Mtibwa Estates ya mkoani Morogoro. Mtibwa ilianzishwa mwaka 1988 na wafanyakazi wa kiwanda hicho kabla ya kupanda Ligi Kuu mwaka 1997. Ni miongoni mwa timu bora na zenye ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara ikifahamika kwa kuwa na upinzani wa hali ya juu dhidi ya timu vigogo za Simba na Yanga. Pia Mtibwa Sugar inasifika kwa kuibua vipaji ambavyo vimepata kuwika katika klabu za Simba, Yanga na Taifa Stars. The post ‘WANAUME’ SITA VING’ANG’ANIZI LIGI KUU BARA appeared first on Bingwa.

NI WAKATI WA WANARIADHA KUJITOKEZA

$
0
0
NA ZAINAB IDDY MASHINDANO ya Mbio za Nyika za Dunia (World Cross Country), yanatarajiwa kufanyika katika Jiji la Kampala, Uganda,  Machi 26 mwaka huu, Tanzania ikiwa moja ya nchi zitakazoshiriki. Tanzania tunategemea kupeleka washiriki 28 idadi ambayo ndiyo inayotakiwa, kutakuwa na timu tano za Wanawake Seniors Km 10, Wanawake Juniors Km 6 na Wanaume Juniors Km 8, Wanaume Senior Km 10 na pia Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF), limeanzisha mashindano mapya ya “Relay” ambayo yatakuwa na idadi ya wanariadha wanne, wawili ni wanawake na wengine wanaume. Kwa kutambua umuhimu wa mashindano hayo, Tanzania chini cha Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), wameanza  mchakato wa maandalizi tangu Desemba mwaka jana lengo ni kutaka kupata wawakilishi watakaokwenda kushindana kupata medali na si kushiriki kama ilivyozoeleka. RT ilianzisha mpango wa kuandaa mashindano katika baadhi ya mikoa kwa kuzingatia kanda mbalimbali wakianza na mikoa ya Singida, Manyara, Mara, Zanzibar na Ruvuma huku wachezaji waliofanya vizuri wakipewa nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Taifa yatakayofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kuanzia Febuari 18, mwaka huu. Kizuri zaidi katika mashindano hayo pamoja na yale ya Arusha ya wanariadha wanaojitegemea, ndiyo yatakayotoa wawakilishi 28 watakaoingia katika kambi ya Taifa kuanza maandalizi kuelekea katika michuano hiyo Uganda. Pamoja na nafasi ya ushiriki wa  mashindano ya Uganda, lakini pia RT imejipanga kutoa zawadi mbalimbali ikiwamo fedha taslimu kwa washiriki watakaoibuka washindi katika mbio tofauti.. Taarifa ya RT iliyotolewa hivi karibuni juu ya mashindano hayo ya Taifa, atakayeshika namba moja kwa kila mbio ataondoka na Sh 400,000, wa pili 300,000, watatu 200,000, wanne 100,000, watano 90,000, sita 80,000, saba 70,000, wa nane 60,000, wa tisa 50,000 na wa kumi 40,000 hayo yote  ni katika kuhakikisha wanaongeza hamasa kwa washiriki. Katika hili hakuna budi kuwapongeza RT ambao kwa mara ya kwanza wameonekana kuwa na mipango thabiti ya kuifanya Tanzania inaondokana na tabia ya kuwa wasindikizaji  katika mashindano ya kimataifa. Mara kwa mara Tanzania imekuwa wasindikizaji kimataifa, huku sababu kubwa zikitajwa kuwa ni maandalizi mabovu lakini hivi sasa RT chini ya Rais wake, Anthony Mtaka na katibu wake mkuu, Wilherm Gidabudai, aliyevaa viatu vya Seleman Nyambui. Viongozi hao na kamati pamoja na wajumbe wake katika kipindi kifupi tangu walipoingia madarakani, wameonyesha nia ya dhati ya kuipeleka mbele riadha ya Tanzania tofauti na kipindi kilichopita ambacho kilitawaliwa na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe. Kulingana na maandalizi yanayofanywa na RT kuelekea mashindano ya Uganda, ni wakati sasa kwa vijana  na wanariadha kujitokeaza katika mashindano ya Taifa   ambayo yametoa nafasi kwa kila mmoja mwenye uwezo na anayekidhi vigezo kushiriki. Ninaimani ili Tanzania tupige hatua katika mchezo huu, ni lazima sisi wenyewe tuwe tayari kujitoa katika kushiriki mashindano mbalimbali kwa nguvu zote ili tuweze kupata nafasi kimataifa. Ni wakati wa kuondokana na dhana kuwa mchezo wa riadha ni wa watu wachache kama Alfonce Simbu, Sara Ramadhan na wengine ambao kila wakati ndio wanaoonekana kujitoa katika kuhakikisha Tanzania inapata wawakilishi kimataifa. The post NI WAKATI WA WANARIADHA KUJITOKEZA appeared first on Bingwa.

Jecha akabidhi ripoti ya uchaguzi

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha amemkabidhi Rais Ali Mohamed Shein ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015 na ule wa marudio wa Machi 20, 2016.
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>