Serikali imesema haitakua tayari kuona Jeshi la Polisi linachafuliwa na baadhi ya Askari Polisi wasiofuta maadili huku ikisisitiza haitosita kumchukulia hatua askari atakaebanika kukiuka maadiliHayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifunga mafunzo kwa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi Visiwani Zanzibar ambapo jumla wa walinzi 681 walihitimu mafunzo hayoAkizungumza na wahitimu pamoja na askari katika hafla hiyo Naibu Waziri Masauni alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na askari polisi waadilifu huku akiweka wazi kuwepo kwa askari wasio waadilifu“Jeshi letu la Polisi lina miiko yake katika utendaji wa kazi zake,lakini wapo askari wachache wanaovujisha taarifa kwa wahalifu, wanasaidia wahalifu kutenda makosa sambamba na kupokea rushwa,hali hiyo haikubaliki na atakebainika hatutosita kumchukukia hatua kwa mujibu wa taratibu za jeshi,” alisema MasauniAkizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Saleh Mohamed Saleh, aliwataka wananchi kufichua wahalifu wanaowafahamu katika makazi yao ili matendo ya uhalifu yaweze kupungua“Polisi Jamii ni dhana pana,tunawategemea wananchi mtusaidie kufichua wahalifu katika maeneo mnayoishi maana uhalifu ukifanyika nyie ndio mnaathirika hivyo basi ni bora mkawa mabalozi wazuri katika maeneo yenu kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi,” alisema Kamishna SalehKatika mafunzo hayo jumla ya Walinzi Shirikishi 681 walihitimu ambapo walipitishwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukamataji salama,namna ya kuendesha doria,jinsi ya kumfikisha mtuhumiwa kituo cha polisi na elimu jinsi ya kujikinga na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto.
↧
Serikali Kuendelea Kusimamia Maadili ya Askari Polisi
↧
Mwili wa Ruge Kuwasili Nchini Ijumaa ya March 1, 2019
Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa ya Machi 1,2019 na utazikwa Bukoba, mkoani Kagera wiki ijayo.Annik Kashasha ambaye ni msemaji wa Familia ya Mutahaba amesema Leo Jumatano February 27 kuwa kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga Ruge siku ya Jumamosi,March 2.Baada ya hapo Familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya Jumatatu ya March 4, 2019.
↧
↧
CAMILLA PARKER BOWLES: Alimbomoa Princess Diana, akafeli kwa Princess Kate, sasa aujaribu umalkia Uingereza
JOSEPH HIZA
MTAWALA wa
Kike wa Cornwall nchini Uingereza, Camilla Parker Bowles amekuwa haishiwi na kashfa
hasa zinazomtazama kama mwanamke mbinafsi mwenye roho ya korosho, chuki, wivu
na husda.
Analaumiwa si
tu kuisambaratisha ndoa ya kwanza ya mumewe, Prince Charles na aliyekuwa
kipenzi cha wengi, Princess Diana bali pia kifo cha mtawala huyo wa kike wa
Wales mwaka 1997.
Uhusiano
wake na Prince Charles ulianza tangu mwaka 1972 na uliendelea kwa siri hata
pale walipoingia ndoa na watu tofauti; Camilla akiwa na mjeshi mmoja hivi,
Charles na Diana.
Licha ya kufanikiwa
kumpata Prince Charles aliendeleza chuki kwa mke wa mwanae wa kambo Prince
Williams, Mtawala wa Kike wa Cambridge, Kate Middleton, tangu alipomtupia jicho
kwa mara ya kwanza miaka 15 iliyopita.
Wakati Parker
Bowles (68), alipokutana mara ya kwanza na Middleton (36) wakati urafiki wake
na Prince Williams wakati wa enzi zao katika Chuo Kikuu cha St. Andrews, alimpa
uzito maalumu.
Middleton alishukuru
kwa wema na ukarimu aliofanyiwa naye na alimsimulia mama yake Carole namna
alivyokirimiwa na Camilla katika moja ya shughuli za ukoo wa kifalme.
“Ni mcheshi
mno na aina ya mama mwema,” Middleton anasemekana kuwaambia wazazi wake, pasipo
kujua nini kinaendelea moyoni mwa Camilla.
Ndivyo
ilivyokuwa, kwani nyuma ya pazia, Parker Bowles alikuwa anakula njama za kuwatenganisha
na kumchagulia mwanae huyo aina ya mwanamke kama alivyodai ‘mrembo na wa hadhi
zaidi’.
Hivyo, tangu
hapo Camilla alifuatilia kwa karibu nyendo za penzi hilo changa ikiwamo kutuma mashushushu
kufuatilia na hata kuangalia uwezekano wa kuingiza sumu kulivuruga.
Alitoa
sababu kadhaa za kumkataa Middleton, mbali ya malezi kutoka familia ya kawaida,
hakupendezwa na tabia ya mama yake, Carole ya uvutaji sigara na nyinginezo.
Kuhusu haiba
ya Middleton alikiri yu ‘mzuri’ lakini ‘aliyefifia’
au kutokuwa ‘mwanamke wa maarifa,” anaripotiwa kumtoa dosari.
Lakini
ukweli ni kwamba yote hayo ni chuki tu zinazotokana na wivu. Camilla hakutaka
awepo ‘mtu baki’ ampiku umaarufu na hata uwezekano kuchuana naye katika kiti
cha umalkia.
Na hivyo
haikushangaza alipompiga marufuku Middleton kuhudhuria arusi yake na Prince
Charles mwaka 2005, kwa mujibu wa habari za ndani.
Baada ya
kufanikiwa kuingia katika ndoa na kipenzi chake hicho cha tangu ujanani,
ukizingatia wote walishatengana na wenzi wao wa awali, Camilla aliongeza
mashambulizi kuhakikisha Kate haingii katika ukoo wao huo.
Kama mama wa
kambo, anatuhumiwa kumshawishi William kumtosa rafikiye huyo aliyedumu naye miaka
sita mwaka 2007 akiukosoa ukoo wake kutoendana na wa kifalme.
Wakati
kashfa ya familia ya akina Middleton ilipovuja— mjomba wake Gary akituhumiwa kutumia
dawa za kulevya — Parker Bowles alipata nguvu zaidi na kumshikia sikio mumewe Charles.
Ikumbukwe Charles
hakuwa na sauti mbele ya mkewe huyo na wakati
huo huo hakuona ubaya wa uhusiano baina ya mwanae na akina Middletons.
Lakini kutokana
na ushawishi wa mkewe, Charles alitimiza matakwa ya mkewe na hivyo William
akatengana na Kate mwaka 2007.
Haikuchukua
muda baada ya mtengano huo, magazeti ya udaku yakajaa na picha na habari chafu
kumhusu Kate, nyingine zikimwonesha akicheza katika vilabu vya usiku akiwa na
dada yake Pippa huku wakiwa wamevaa viwalo kama vile sketi fupi na za kubana.
Inasemekana
Camilla alikuwa nyuma ya mikakati yote hiyo na vyombo hivyo vya habari.
Lakini katika
kuonesha kuwa walishibana, wiki sita baadaye Will na Kate wakarudiana na umma
wa Uingereza ukavutiwa na msichana huyo kutoka familia ya kawaida.
Wakati huo
huo, Camilla aliendelea kutumia saa nyingi kufanya mikakati huku akivujisha
taarifa za kweli na uongo kwa vyombo vya habari.
Licha ya
hayo, Camilla si tu hakufanikiwa katika azma yake hiyo bali pia amebakia kutopendwa
na watu wa kawaida pamoja na Malkia Elizabeth II mwenyewe hadi leo hii.
Prince
William akamuoa Middleton April 29, 2011 na sasa wawili hao wana watoto wawili:
Prince George (miaka 2) na Princess Charlotte, miezi 11.
Licha ya
roho mbaya Camilla aliyomfanyia Kate, yeye mwenyewe alipambana mno kuweza kuolewa
na Charles kutokana na kupingwa kwa nguvu si tu na umma wa Waingereza bali pia ukoo
wa kifalme kutokana na nyendo zake zisizofurahisha, kukosa mvuto na ‘alichomfanyia’
si tu Prince Diana bali pia mumewe wa kwanza.
Ukoo wa
kifalme ulikuwa ukimshinikiza Charles kutomuoa Camilla, ambaye ameweza
kujipenyeza katika ukoo huo kutokana na uhusiano wa nyuma wa babu yake na ukoo
huo.
Iliwahi kufikia
hatua ya kuwapiga marufuku watoto wa Camilla wapenda matanuzi Laura Lopes na
Tom Parker Bowles kumkaribia kijana Prince William kwa hofu ya ‘kumwambukiza’
tabia mbaya.
Lakini
mwishowe, malkia akasalimu amri kutokana na msimamo wa mwanae. Ilikuwaje?
Ili
kuhakikisha ndoto yake ya kumuoa Camilla inatimia, Charles alimuahidi mama yake
kuwa Camilla hatokuwa malkia wakati atakapotawazwa ufalme. Hilo la umalkia
lilikuwa moja ya hofu iliyoujaa ukoo huo.
“Camilla
hana mpango wala nia ya kuwa Mtawala wa Kike wa Wales sasa wala kuwa malkia
hapo baadaye, Charles alisisitiza. “Wote mimi na Camilla tunahisi kuwa ni vyema
nitakapokuwa mfalme, yeye abaki kama mtawala wa kike mfariji tu,” alimwambia
mama yake.
Hivyo ukoo
wa Kifalme ukatangaza kuwa licha ya ndoa hiyo, Camilla hatakuwa malkia. Hivyo wawili
hao wakaoana mwaka 2005
Iwapo kweli
Princes Charles atabakia na ahadi hiyo ya kutomfanya mkewe kuwa malkia, ni kitu
cha kusubiri na kuona ukizingatia udhaifu wake kwa mkewe pamoja na nyendo
zinavyojionesha sasa.
Camilla
amekuwa akionesha kujipamba hadharani
kama mke na mtumishi mwema, akionekana katika matukio yasiyo na idadi ya hisani
na kuvaa mithili ya malkia. Na anapoulizwa swala la umalkia mara nyingi,
Camilla hutabasamu na kusema; “Huwezi jua.”
Hata hivyo,
ukweli ni kwamba ni sheria ya Bunge pekee ndiyo itakayozuia Camilla asitawazwe umalkia
siku ile inakuja!.
↧
Vurugu za wafugaji, wakulima zafukuta Kongwa
WAKULIMA zaidi ya 70 wakiwemo watoto, wanafunzi pamoja na wanawake wamefanya maandamano ya amani kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili wamuelezee kilio chao cha kuporwa maeneo yao ya kilimo. Anaripoti Danson Kaijage, Kongwa … (endelea). Wakulima hao wakiongozwa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Nalau kijiji cha Kiteto, kata ya Lenjulu, Daimon ...
↧
Serikali za Mitaa zaonywa matumizi ya fedha
MAMLAKA za Serikali za Mitaa nchini zimetakiwa kuhakikisha kuwa fedha zote zinazokusanywa katika mapato zinawekwa benki na fedha hizo zitumike katika kutekeleza matumizi husika. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanga katika hafla ya upokeaji wa mashine ...
↧
↧
Wasemaji ANC kuachia ngazi kwa kashfa za ngono
Chama kinachoongoza Afrika Kusini cha ANC jana kimesema kuwa wasemaji wake wawili wataachia ngazi, ikiwa ni miezi mitatu tu kabla ya uchaguzi kutokana na makosa tofauti ya tuhuma za ngono.
↧
Malaysia kutengeneza magari yanayopaa
Malaysia inapanga kuzindua magari yanayopaa, waziri amesema leo na kusababisha kuibuka kwa kejeli katika nchi hiyo ambayo ina historia tofauti katika masuala ya miradi ya magari.
↧
Facebook yafuta ukurasa wa mwanasiasa wa siasa kali
kampuni inayoendesha mtandao wa Facebook jana iliiondoa akaunti ya mwanasiasa wa Uingereza mwenye mrengo wa kulia, Tommy Robinsonkwa kwa kukiuka viwango vilivyowekwa kwa mitandao ya wengi na kuonyeha tabia nyingine ambazo zimezuiwa.
↧
Kolo Toure joins Brendan Rodgers' staff at Leicester City
Ivory Coast legend Kolo Toure has been confirmed as first team coach at Leicester City under new manager Brendan Rodgers
↧
↧
Sone Aluko: Reading forward joins Beijing Renhe in Chinese Super League on loan
Reading and Nigeria forward Sone Aluko moves to Chinese Super League side Beijing Renhe on loan for the rest of 2019.
↧
Uzinduzi wa Barabara ya Kiyuni Hadi Ngomeni Wilaya ya Chakechake Kisiwani Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali.Mohamed Shein.Mama Mwanamwema Shein kulia na Waziri wa Ujenzi Miundombini na Usafirishaji Zanzibar Mhe,Dr.Sira Ubwa. wakiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Barabara ya Kiyuni hadi Ngomeni iliyojengwa kwa kiwango cha lami, uzinduzi huo umefanya wiki hii 25-2-2019, wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mikoa ya Kusini nas Kaskazini Pemba. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasikiliza Watoto walioandaliwa katika hafla ya ukataji wa Utepe wa Uzinduzi wa Barabara ya Kiyuni hadi Ngomeni Wilaya ya Chakechake Kisiwani Pemba akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr, Sira Ubwa, wakishuhudiac ukataji wa Utepe wa kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Kiyuni hadi Ngomeni Kisiwani Pemba iliyojengwa kwa kiwango cha lami. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr, Sira Ubwa, wakishuhudiac ukataji wa Utepe wa kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Kiyuni hadi Ngomeni Kisiwani Pemba iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
↧
Vatican to open internal probe into Cardinal George Pell
The Vatican will launch an internal probe into Cardinal George Pell after he was found guilty of abusing two boys. The investigation could see Pell expelled from the priesthood.
↧
Waziri Ummy awaita wadau sekta ya afya
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameishauri jamii kuwa na utaratibu na utamaduni wa kuchangiana kwenye matibabu pindi mtu anapofikwa na matatizo. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea). Kauli hiyo ameitoa leo wakati akikabidhi kadi ya bima ya afya kwa watoto 105 ambazo zilizotolewa na benki ya Stanbic, jijini Mwanza. Waziri ...
↧
↧
Dk Kigwangalla anavyomkumbuka Ruge kwa Tanzania Unforgettable
Leo Jumatano, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema licha ya kwamba Ruge Mutahaba alikuwa mgonjwa lakini alishiriki kikamilifu kuiandaa ‘Tanzania Unforgettable.
↧
VIDEO: Mwakyembe aagiza Dudu Baya akamatwe, mwenyewe asema hajali
Ni kwa makosa ya kumkashifu marehemu Ruge Mutahaba
↧
Rooney azitabiria Man City, Barca Ligi ya Mabingwa Ulaya
Nyota Wyne Rooney ametabiri Manchester City kukutana na Barcelona kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
↧
Matumla: Daah! Ruge jeshi la mtu mmoja
Bingwa ngumi wa zamani wa dunia wa WBU, Rashid Matumla amesema kifo cha Ruge Mutahaba ni pigo katika familia ya ngumi za kulipwa nchini, kwani ni miongoni mwa watu walioshiriki kikamilifu katika kuwaandalia mabondia mapambano.
↧
↧
‘Mtoto wa Pepe Kale’ afunguka wanaomponda, afiwa na mama yake
Mwimbaji wa bendi ya Akudo Impact, Alain Kabasele, amefunguka kuhusu wanaosema yeye sio mtoto wa aliyekuwa mwanamuziki wa Kinshasa, Joseph Kabasele Yampanya 'Pepe Kale' ambaye kwa sasa ni marehemu.
↧
Nyota 20 Serengeti Boys kwenda Uturuki
Wachezaji 20 wameteuliwa kuunda kikosi cha Serengeti Boys watakaoshiriki mashindano maalum ya shirikisho la soka barani Ulaya 'UEFA Assist' yanayotarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Mach 4 mwaka huu.
↧
Wachezaji Tottenham wamchefua kocha wao
Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema kuirudisha timu hiyo kwenye mbio za ubingwa lingekuwa jambo la miaka kumi.
↧