NA WINFRIDA MTOI
KIUNGO wa Yanga, Mohammed Issa ‘Mo Banka’, anaonekana
kuwapa presha wapinzani wao Lipuli FC baada ya kocha wa kikosi hicho, Samwel
Moja, kukiri yeye ndiye mchezaji atakayewasumbua.
Lipuli na Yanga wanatarajia kukutana Mei 6, mwaka
huu katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), utakaopigwa
kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.
Akizungumza na BINGWA jana, Moja ambaye aliushuhudia
mchezo kati ya Yanga na Tanzania Prisons juzi, alisema Mo Banka amerejea katika kiwango chake hivyo kuifanya
timu yake kuwa na mabadiliko makubwa.
Alisema uwezo wa kiungo huyo umesaidia kuimarisha
eneo la katikati la kikosi cha Yanga hivyo kuwafanya waweze kumiliki mpira muda
mrefu na kupeleka mashambulizi mbele, tofauti na alivyowaona kipindi cha nyuma.
“Nimeangalia mechi za Yanga za hivi karibuni nikabaini
wameimarika sana eneo la katikati, hii
imesababishwa na uwepo wa Mo Banka kulingana na
uchezaji wake,” alisema Moja.
Hata hivyo, alieleza kwamba kutokana na hali
hiyo wanatakiwa kufanya kazi ya ziada wakati wa maandalizi ya mchezo huo, wakitambua
wanakutana na Yanga ya tofauti kabisa na ile waliyoifunga katika mechi ya Ligi
Kuu Tanzania Bara
↧