NA BRIGHITER MASAKI
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika onyesho la Siku ya Urembo wa Asili Tanzania, linaloanza leo na kuendelea kesho katika ukumbi wa Life Park, Mwenge, Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA jana, mwandaaji wa onyesho hilo, Antu Mandoza, alisema yatatolewa mafunzo ya kutengeneza vipodozi vya asili visivyo na kemikali bure na kutakuwa na upimaji saratani ya matiti na elimu ya saratani mbalimbali bila malipo.
“Kutakuwa na kipaumbele kwa wanawake wajasiriamali wa kundi maalumu kama vile walemavu kushiriki katika maonyesho haya ambapo watapewa banda bure la kuonyesha kazi zao pamoja na wajasiriamali vijana,” alisema Antu.
Katika burudani, wasanii kama Khadija Kopa, Aneth Kushaba, Mwasiti, Grace Matata, huku Rose Ndauka, mchekeshaji Jaymond na mtangazaji Dina Marious watazungumza na watu.
↧