AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM
PACHA waliougana Anisia na Melnes Bernard, wamewasili jana katika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea nchini Saudi Arabia baada ya kutenganishwa, matibabu
yaliyogharimu dola za Marekani 500,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.1)
Mapacha hao
walikuwa wameungana kifua, tumbo na nyonga walianza kufanyiwa upasuaji wa
kutenganishwa Disemba 23 katika hospitali ya King Abdallah.
Baada ya
kutenganishwa, pacha hao ambao walizaliwa wakiwa na miguu mitatu, sasa kila
mmoja amebaki na mmguu mmoja.
Wakizungumza
wakati walipowasili, madaktari bingwa wa upasuaji kwa watoto walisema
waliungana na madaktari 35 wa Saudi Arabia na nchi zingine ili kufanikisha upasuaji huo ambao ulifanyika
ndani ya sasa 14.
Mmoja wa
Madaktari hao Dk Petronia Ngiroi, alisema madktari bingwa wa sehemu mbalimbali
wa watoto walifanya uchunguzi na kuhakikisha kuwa upasuaji huo utafanikiwa.
“Tangu
wakiwa Muhimbili tuliwafanyia vipimo na tukawasiliana na madktari wa Saudi
Arabia na tukawatumia vipimo wakatuambia inawezekana kufanyiwa upasuaji baada
ya hapo tukaanza safari Julai 8 mwaka jana.
“Tuliposafiri
tulipokelewa vizuri na watoto wakaanza kupatiwa vipimo mbalimbali kwani umbali
wa kutoka huku mpaka kule uliwafanya wawe na infection hivyo wakawafanyia consultation
kwa madaktari wa mifupa, kibofu cha mkojo, madktari wa upasuaji kwahiyo
wataalamu karibia wote waliwaona watoto,”alieleza Dk Ngiroi.
Daktari mwingine Dk Zainab Bohari, alisema
pamoja na kuwa watoto hao waliungana, kila mmoja anaweza kuwa na tabia yake na
wanauwezo wa kuishi muda mrefu kama watu wengine .
“Kutenganishwa
kwa kutawapa uhuru kwani tulipenda wote wawili watoke salama, walikuwa na miguu
mitatu lakini kila mmoja amerudi na mguu mmoja na mguu wa tatu ulitumika kuziba
vidonda vya upasuaji.
“Hawa watoto
wamenufaika kupitia ushirikiano mzuri na
Saudi Arabia, tukumbuke watoto hawa walitokea Bukoba hivyo tutafatilia hali zao
mpaka wawe watu wazima hasa afya zao,”alisema Dk Bohari.
Kwa upande
wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Elias Kwesi, alisema anashukuru ubalozi wa Saudi
Arabia kwa ushirikiano waliouonesha hadi
kuwarudisha watoto hao kuwa salama.
Naye Katibu
Mkuu wa Waizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mwinyi, alisema Serikali ya Tanzania
inashirikiana kikamilifu na Serikali ya Saudi Arabia ambapo walitoa mashine na
vifaa tiba 64.
“Walitupa
mashine na vifaa ambavyo viligawavywa bara walipata mashine 45 na Zanzibar
walipewa 17 na pia msaada huu ambao tumepata kwa watoto hawa ni mkubwa
pia,”alisema Mwinyi.
Kwa upande
wake mama wa watoto hao, Jonensia Jovitus, aliwashukuru watu wote walioshiriki
katika kufanikisha matibabu ya watoto wake.
“Napenda kuwashukuru
wote kwani tokea ninamimba ya hawa watoto nilipata shida sana lakini kwa uwezo
wa Mungu nikafanikiwa kujifungua salama, nawashukuru pia hospitali ya muhimbili
kwa jitihada walizofanya kufanikisha jambo hilo,”alisema Jonensia.
↧