Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

JIJI LA LOS ANGELES LAAMUA TAREHE 23 AGOSTI KUWA KOBE BRYANT DAY.

$
0
0
Kitendo cha kuamua kustaafu kucheza mchezo wa mpira wa kikapu kwa Kobe Bryant imekuwa kama hatua nzuri kwake kwani neema kadhaa zimeanza kufunguka kwake ambazo ni za kipekee. Staa huyu wa zamani wa klabu ya Los Angeles Lakers hivi karibuni alizindua mfuko wa uwekezaji wenye thamani ya paundi milioni 100 na huku pia akitumika kuendesha gari ya majaribio yenye thamani ya dola za kimarekani 490,000 katika makao makuu  ya Ferrari, na sasa atakuwa na siku yake mwenyewe. Siku ya Jumatatu, Halmashauri ya Jiji za Los Angeles walitangaza kuwa Jumatano hii itakuwa inajulikana kama tarehe ya Kobe Bryant ikiwa ni kuadhimisha namba za jezi mbili alizowahi kuzivaa mchezaji huyu akiwa  na klabu ya Los Angeles Lakers, 8 na 24 . “Miongoni mafanikio yake, kitendo cha Kobe Bryant kucheza kwa miaka 20 katika klabu moja ya Los Angeles Lakers inamfanya kuwa mchezaji aliyecheza kwa miaka mingi na klabu moja ndani ya na katika historia ya muda wote ya NBA. Kobe Bryant Day ‘ katika jiji la Los Angeles Lakers ‘ imeonekana kama njia sahihi ya kumshukuru kwa kujitolea kwake kuwa nao kwa kipindi chote hiki , hii ikiwa ni kutoka kwa mashabiki na jiji zima la Los Angeles, ” alisema Councillor wa jiji hilo Huizar. Bryant pia anaheshimika kwa kazi yake uhisani pamoja na mke wake, Vanessa , wakiwa na kampuni ya hisani inayofahamika kama Kobe and Vanessa Bryant Family Foundation ( KVBFF ). Msingi wa mfuko huu ni kujitolea na kuboresha maisha ya vijana na familia wenye uhitaji, wote wa ndani na wale wakimataifa, na kuhamasisha vijana kukaa kujishughulisha na kuwa salama kwa njia ya michezo . “Kwa miaka 20 , tulinufaika kwa pmoja na uwezo wa kujitolea kimichezo kwa Kobe Bryant katika jiji hili, na sasa kupitia 8-24 kwa pamoja tunaunganika na kusema, ‘ Asante, Black Mamba ,'” alisema Huizar . Bryant pia alisherekea miaka yake 38 ya kuzaliwa siku ya jana Jumanne tarehe 23 mwezi huu. Ameshinda ubingwa wa NBA mara 5, mchezaji bora mwenye thamani wa msimu mara moja, na pia akishiriki NBA ALL STAR mara 18.        

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>