Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

YONDANI AMSIKITISHA MKWASA

$
0
0
Wakati kikosi cha Taifa Stars kikisafiri kuelekea Nigeria, Kelvin Yondani si miongoni mwa wachezaji 18 walioondoka kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo wa mwisho katika hatua ya makundi kuwania kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 2017. Taarifa ambazo shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linazo ni kwamba Yondani anamatatizo ya kifamilia ambapo hajayaweka sawa hadi wakati timu hiyo inaondoka kwenda Nigeria. Kocha mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwasa amesikitishwa na kitendo hicho lakini TFF itasubiri ripoti ya kocha huyo mara baada ya kurejea kutoka Nigeria. “Amepigiwa simu hakupokea, ametumiwa ujumbe mfupi wa maandishi lakini pia akatumiwa ujumbe kwa mfumbo wa whatsapp lakini hakujibu. Tukazungumza na viongozi wa Yanga Katibu Mkuu Baraka Deus Dedit akatuambia Yondani hayupo kambini kwao na sababu ya kutokuwepo ni kwamba ametoa taarifa kwamba anamatatizo ya kifamilia”, amesema afisa habari wa TFF Alfred Lucas ambaye alizungumza na Mkwasa muda mfupi kabla ya safari. “Jambo hilo limemsikitisha sana mwalimu (Charles Boniface Mkwasa)kwasababu ni mchezaji ambaye alimtegemea, lakini sisi kwa upande wetu  (TFF) tunasubiri ripoti ya mwalimu ndipo tuweze kuzungumza jambo au kutenda jambo.” Stars imeondoka Dar ikiundwa na wachezaji 18 huku nahodha wake Mbwana Samatta akitarajiwa kuungana na kikosi hicho nchini Nigeria.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>