Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

MAGULI NJIANI KUIKACHA STAND, KUJIUNGA NA WAKALI WENGINE VPL

$
0
0
Elius Maguli, mshambuliaji wa timu ya taifa ya ‘Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu ya Stand United Mshambuliaji wa Stand United Elias Maguli ambaye amekuwa hana mwendelezo mzuri kwenye klabu yake tangu alipohitilafiana na kocha wa timu hiyo, huenda akajiunga na wapinzani wao wa mjini Shinyanga Mwadui FC. Mwadui ambayo ipo chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ inajaribu kuimarisha kikosi chake hasa katika nafasi ya ushambuliaji hasa kutokana na kufunga magoli 29 katika msimu huu baada ya kucheza mechi zote 30. Maguli aliingia kwenye mgogoro na kocha wake Patrick Liewig baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Tanzania Prisons, Ruvu Shooting na Simba kwenda kufanya majaribio nchini Misri huku kocha wake akiwa hana taarifa hizo. Baada ya Maguli kurejea Stand, hakupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza licha ya kuwa ndiye mshambuliaji aliyekuwa akiongoza kupasia nyavu katika ligi kwa wakati huo hadi baadaye alipoomba radhi. Endapo Maguli ataihama Stand United, inatajwa kuwa maelewano madogo kati yake na Liewig ndiyo sababu kubwa ya nyota huyo wa taifa stars kuikacha Stand ambayo ameifungia magoli 14 katika msimu wake wa kwanza kwenye klabu hiyo akishikilia nafasi ya nne katika orodha ya wafungaji bora wa VPL msimu uliomalizika hivi karibuni. Idd Ubwa na Haruna Chanongo ni wachezaji wengine ambao waliingia kwenye marumbano na kocha huyo mfaransa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>