Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Walcott: Vita ya namba inaibeba Arsenal

$
0
0
LONDON, England Theo Walcott anaamini kugombania namba ndiyo sababu kubwa inayowafanya Arsenal  kung’ara Ligi Kuu England, ambapo kwa kikosi hicho cha Arsene Wenger kina pointi sawa na vinara wa ligi hiyo, Manchester City. Arsenal ilikuwa kwenye wakati mgumu katika mchezo wao wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Swansea City, walioshinda mabao 3-2, baada ya kiungo Granit Xhaka kutolewa kwa kadi nyekundu  kipindi cha pili. Lakini Arsenal walipambana na kuulinda ushindi huo, ambao mabao mawili yalifungwa na Walcott, huku Mesut Ozil, aliyekuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, akifunga moja. “Ni mafanikio makubwa kwetu, baada ya kuanza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu England,” alisema Walcott. “Msimu huu kuna mambo tumeongeza na ndiyo maana tumeanza kuwa na mafanikio, tumefanya kazi timu nzima kufika tulipofika sasa.” “Kwa sasa timu yetu ina ushindani mkubwa wa namba, hili ndilo linatufanya tucheze kwenye kiwango cha juu.” Mechi inayofuata Arsenal watakutana na Ludogorets katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo watakuwa nyumbani, kabla ya kuikaribisha Middlesbrough kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. The post Walcott: Vita ya namba inaibeba Arsenal appeared first on Bingwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>