Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Red Monday… Mourinho ataendelea kuwa mteja wa Klopp?

$
0
0
MERSEYSIDE, England KIU ya kuuona mtanange wa mahasimu wawili wa Kaskazini Magharibi (North West derby) kati ya Liverpool na Manchester United, kuona kama Jose Mourinho atafuta uteja wake kwa Jurgen Klopp itamalizwa leo. Leo haitakuwa tena ‘Blue Monday’ kama watu walivyozoea kuiita siku hii ya Jumatatu, baada ya uchovu na ‘mning’inio’ wa wikiendi, bali itakuwa ni ‘Red Monday’, pale miamba hiyo inayotumia jezi zenye rangi nyekundu itakapoumana. Mechi za Liverpool na Man United ni moja ya mechi zenye uhasimu mkubwa kuliko nyingine, kutokana na kuhusisha klabu ambazo zimenyakua mataji makubwa 87, kati yao (Liverpool 44, Man Utd 43). Kwa sasa Liverpool wako kwenye kiwango cha juu, wakiwa wameshinda mechi zao nne za mwisho za Ligi Kuu England, ikiwa ni moja ya mafanikio kwao wakiwa chini ya Klopp, wakati United tayari wamekwishapoteza mechi mbili za ligi msimu huu na wako nyuma kwa pointi tano dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Manchester City. Lakini, rekodi ya hivi karibuni ya United dhidi ya Liverpool ni nzuri, ambapo wameshinda mechi zao nne za ligi walizokutana kati yao. Ikiwemo mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu England kushinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Anfield, Januari mwaka huu. Liverpool wameshinda mabao 2-0 mechi yao ya mwisho kukutana na Man United katika Uwanja wa Anfield, kwenye mechi ya mtoano ya Ligi ya Europa msimu uliopita. Hali za wachezaji Kiungo Adam Lallana ndiye anamtia shaka Klopp, kutokana na nyota huyo wa England kupata majeraha ya nyonga katika mchezo uliopita dhidi ya Swansea. Kiungo mwenzake, Georginio Wijnaldum, amerejea kutoka timu yake ya Taifa ya Uholanzi, akiwa na majeraha ya paja, lakini wote wawili hawajawekwa wazi kwenye uwezekano wa kuukosa mchezo wa leo, huku mabeki Nathaniel Clyne na Dejan Lovren, ambao walipata majeraha kwenye timu zao za taifa wako vizuri. Kwa upande wa Mourinho, wachezaji wake wawili, Luke Shaw na Henrikh Mkhitaryan watakuwa wamerejea kutoka majeruhi kuucheza mchezo huo. Beki wa kushoto, Shaw alikosa mechi nne za United kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyonga na majeraha ya nyama za paja yalimweka benchi kwa muda Mkhitaryan tangu mchezo wa ‘Manchester derby’ Septemba 10, mwaka huu. Beki Phil Jones, anayesumbuliwa na majeraha ya goti ndiye pekee atakosekana, huku nahodha wa England, Wayne Rooney, ambaye alianzia bechi kwenye mechi tatu za ‘Three Lions’, huenda akaendelea kuwekwa benchi kwenye kikosi hicho cha United. Takwimu za mechi Liverpool wamepoteza mechi nyingi za Ligi Kuu England ambazo ni 27, huku wakipoteza mechi 67 dhidi ya United kuliko wapinzani wengine. Liverpool wamepoteza mechi zao nne za Ligi Kuu England za mwisho kukutana na United, ikiwa ni rekodi yao mbaya dhidi ya Red Devils tangu Machi 2008 (walifungwa mechi tano mfululizo za Ligi Kuu England). Mechi za mahasimu hawa wawili zimeshuhudia kadi nyekundu 16 kwenye Ligi Kuu England; Everton na Liverpool wao pekee ndio wameshuhudia kadi nyekundu 21. Klopp amepoteza mechi moja kati ya tano ambazo amekutana na Mourinho (kashinda tatu, sare moja), mechi hiyo aliyofungwa ilikuwa ni mwaka 2013, wakati Borussia Dortmund wakichapwa mabao 2-0 na kuitoa Real Madrid kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa mara ya kwanza Klopp na Mourinho kukutana ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi miaka minne iliyopita, Borussia Dortmund iliichapa Real Madrid mabao 2-1 katika mchezo huo wa Kundi D (Oktoba 2012). Haikuchukua muda mrefu makocha hao wawili kukutana tena, wakati Madrid walipoikaribisha Dortmund kwenye mechi ya marudiano ya Kundi D kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, Novemba 2012, ambapo mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2. Miezi mitano baada ya mechi hiyo ya sare (Aprili 2013), makocha hao maarufu walikutana tena msimu huo ambao fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja Wembley. Borussia Dortmund walishinda mabao 4-1 kwenye mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wakati wa maandalizi ya mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, mechi hiyo ndiyo ilikuwa ikiamua hatima ya Mourinho kwenye klabu hiyo ya Real, hofu ilionekana kuwa juu kati ya makocha hao wawili. Hiyo ndiyo ilikuwa mechi pekee Mourinho kumfunga Klopp, ambapo Real Madrid waliichapa Borussia Dortmund mabao 2-0. Oktoba mwaka jana, Klopp akiwa Liverpool alishinda mechi yake ya tatu kati ya tano walizokutana na Mourinho, ambaye wakati huo alikuwa akiinoa Chelsea. Walishinda mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England. Tangu Klopp atue Liverpool Oktoba mwaka 2015, wamefunga mabao mengi kuliko timu yoyote ya Ligi Kuu England ambayo ni mabao 73 na kuwa na wastani mkubwa wa kumiliki mchezo ambao ni asilimia 58.8. Juan Mata amehusika kwenye mabao matano katika mechi nne alizokutana na Liverpool kwenye Ligi Kuu England, akifunga matatu, akitoa pasi mbili za mabao. Mkongwe Steven Gerrard ndiye amefunga mabao mengi kwenye mechi za Ligi Kuu England zinazowakutanisha mahasimu hawa wawili, ambapo amefunga mabao nane zaidi ya Rooney mwenye mabao sita, sawa na mkongwe Robbie Fowler. Hadi sasa Rooney ana mabao 87 ya ugenini kwenye mechi za Ligi Kuu England, akikaribiana kabisa na Alan Shearer. Manchester United wamekusanya pointi tatu zaidi msimu huu, tofauti na msimu uliopita chini ya kocha Louis Van Gaal wakati kama huu. Zlatan Ibrahimovic hajafunga mechi tatu za ligi, ikiwa ni rekodi mbaya kwake tangu Januari mwaka 2015, ambapo alicheza mechi nne mfululizo bila kufunga akiwa Paris Saint-Germain. Marcus Rashford amefunga mabao 12 tangu ameanza kuchezea United, Februari mwaka huu kwenye michuano yote, mabao manne zaidi ya wachezaji wengine wa United kwa kipindi hiki. The post Red Monday… Mourinho ataendelea kuwa mteja wa Klopp? appeared first on Bingwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>