Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783
↧

BABU TALE AENDELEA KUSOTA MAHABUSU

$
0
0
NA KULWA MZEE   MENEJA wa staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamis Shaban Taletale (Babu Tale), ataendelea kusota mahabusu hadi msajili aliyetoa amri ya kukamatwa kwake atakapokuja kwa ajili ya maelekezo mengine   Uamuzi huo ulifikiwa jana na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, baada ya Babu Tale kufikishwa akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi saa sita mchana, baada ya kutiwa mbaroni juzi kwa amri ya mahakama.   Babu Tale alitiwa mbaroni juzi na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kutokana na amri iliyotolewa na Msajili wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri na kupelekwa Gereza la Ukonga, kutumikia kifungo kama mfungwa wa madai.   Mahakama hiyo iliamuru hivyo kutokana na Babu Tale ambaye ni mmoja ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tiptop Connection Ltd, kushindwa kulipa shilingi milioni 250 kwa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, kwa kutumia kibiashara mahubiri yake bila ridhaa wala makubaliano.   Baada ya kufikishwa mahakamani jana, Babu Tale, alifikishwa mbele ya Naibu Msajili Ruth Massam, ambaye aliwapa dakika 10 pande zote wajadiliane namna ya kulimaliza lakini walishindwana kwenye kiwango.   Kutokana na kushindwa kufikia mwafaka, Naibu Msajili Ruth alisema Msajili Mashauri yuko Dodoma na kuamuru Babu Tale arudishwe mahabusu mpaka Msajili atakapokuja kwa ajili ya maelekezo mengine ya kimahakama.   Februari 16, mwaka huu Mahakama Kuu kupitia Naibu Msajili, Wilbard Mashauri, ilitoa amri ya kukamatwa Babu Tale na ndugu yake, Idd Shaban Taletale na kupelekwa gerezani kuwa wafungwa wa madai baada ya kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama hiyo.   Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Augustine Shangwa Februari 18, 2016, iliwaamuru Babu Tale na nduguye ambao ni Wakurugenzi wa Kampuni ya Toptop, kumlipa fidia ya Sh milioni 250, Sheikh Mbonde baada ya kuwafungulia kesi.   Katika kesi ya msingi, Sheikh Mbonde, alikuwa akidai kuwa aliingia mkataba na Kampuni ya kina Babu Tale (Tiptop Connection) ili wamrekodi mahubiri yake kisha wayauze na kugawana mapato.   Baada ya kurekodi masomo saba, walimkatia mawasiliano na alipowatafuta na kukutana nao wakamweleza kuwa wameamua kuachana na mpango huo.   Sheikh Mbonde anadai akiwa kwenye mahubiri Dodoma, akakutana na mikanda ya video katika mfumo wa DVD yenye mahubiri yake huku kukiwa na namba za simu za viongozi hao wa Tiptop.   Sheikh Mbonde akadai baada ya kufanya uchunguzi alibaini kuwa DVD hizo zilikuwa zikiuzwa katika mikoa mbalimbali, ndipo akawafungulia kesi ya madai. The post BABU TALE AENDELEA KUSOTA MAHABUSU appeared first on Bingwa.
↧

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Latest Images

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>