Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

WANASOKA WETU WAJIFUNZE KWA KINA NDIKUMANA, NONDA SHABANI

$
0
0
NA JUMA KASESA, BUJUMBURA WAKO wapi Emmanuel Gabriel, Nico Nyagawa, Mussa Hassan Mgosi, Victor Costa ‘Nyumba’ na wengineo ambao walicheza na straika Mrundi Selemani Ndikumana wakati ule wa kikosi cha Simba mwaka 2007. Ni kipa Juma Kaseja pekee ndiye aliyebaki anacheza soka mpaka sasa ambaye alicheza na Ndikumana pamoja Simba lakini wengi wa wachezaji hao sasa wako hoi kisoka na kiuchumi. Hawa ni baadhi tu ya wachezaji waliocheza na Ndikumana ambaye kwa sasa anawika nchini Qatar na klabu ya Almisamiry inayoshiriki Ligi Daraja la pili, akiwa anashika nafasi ya pili  katika mbio za kuwania ufungaji bora. Rekodi zinaonyesha kuwa robo tatu ya wachezaji aliokipiga nao Simba wakati ule tayari walishastaafu soka muda mrefu lakini yeye bado anawika katika soka la kulipwa lakini pia na timu ya Taifa ya Burundi ambako anaendelea kuvaa kitambaa cha unahodha. Kwanini Ndikumana awe bado wamo katika soka huku nyota wazawa aliocheza nao Simba katika umri mmoja wawe wameshastaafu? Hapa ndipo kwenye maswali mengi yasiyokuwa na majibu. Moja ya maswali hayo ni nani aliyewaroga wanasoka wa Tanzania? Kwanini Warundi wanaendelea kuifanya Tanzania kama daraja la kupita na kisha kwenda kuvuna mafanikio ilhali wachezaji wazawa wakiwa bado wapo katika usingizi mzito. Nani aliyewahi kujiuliza kwanini Burundi ina wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa kuliko Tanzania wakati nchi hiyo kwa muda mrefu inakabiliwa na matatizo ya kisiasa na vita vya kikabila. Ukiitazama safari ya soka ya Ndikumana baada ya kuachana na Simba mwaka huo ni ndefu, kwani ni mtu ambaye alionyesha kuwa mwenye kiu ya mafanikio na hakuridhika na mafanikio ya muda mfupi aliyoyapata akiwa na klabu hiyo. Hili la kutoridhika na kulewa sifa za kuichezea Simba moja ya klabu kubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki lilitosha kumfanya nyota huyo kuendelea kuwa mpambanaji na kujikuta akitua barani ulaya. Takwimu zinaonyesha nyota huyo amecheza soka katika nchi mbalimbali barani ulaya na amepata mafanikio makubwa ya kiuchumi kiasi cha kuwa miongoni mwa wachezaji matajiri nchini Burundi. Huyo ni Ndikumana tu lakini wapo wachezaji wengine wa kimataifa ambao wameitumia Tanzania kama njia ya kwenda kuogelea mafanikio ya kiuchumi kupitia soka na kuwaacha nyota wazawa waking’aa macho. Mtazame Emmanuel Okwi alivyokwishapiga pesa kupitia klabu za Tanzania kabla ya kutimkia nchini Sweden ambako yuko mpaka sasa. Kumbuka safari ya straika Mcongoman Nonda Shaban Papii alivyoitumia Yanga kama daraja kabla kutimkia barani ulaya na kufanya mambo makubwa katika soka akiwa nchini Ufaransa. Nani asiyefahamu yaliyofanywa na Nonda akiwa na klabu kama Vaal Professionals, FC Zürich Rennes, Monaco, Roma, Blackburn Rovers na Galatasaray  ambapo straika huyo alifanikiwa kupiga pesa kujenga vitega uchumi vya kutosha na sasa ni mmoja ya wafanyabiashara wakubwa jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo -DR, waliovuna mafanikio kupitia soka. Ukitazama kipindi kifupi Nonda alichoichezea Yanga wakati ule utagundua baada ya kuondoka kwake wachezaji aliokipiga nao soka katika umri mmoja waliachana na mpira na kugeuka maveteran. Kupitia wachezaji hao kwa uchache kipo cha kujifunza kwa nyota wa sasa wa Tanzania katika safari ya maisha ya soka waliyonayo. Bila ya wachezaji hao kubadilika na kutamani mafanikio ya wenzao safari ya maisha ya soka siku za usoni itaendelea ngumu kwao. The post WANASOKA WETU WAJIFUNZE KWA KINA NDIKUMANA, NONDA SHABANI appeared first on Dimba.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>