Star wa BongoFleva na mshambuliaji wa Coastal Union Ali Kiba amesema waamuzi waliochezesha #CoastalVsYanga timu yao ilionewa na waamuzi.
“Uonevu ulikuwa LIVE yani”-Ali Kiba.
Kocha wa Yanga ZAHERA MWINYI
“Waamuzi wa hovyo wanachezesha mpira wanavyopenda, mnacheza na waamuzi, mnacheza na timu pinzani. Kwa aina hii ya marefa unafikiri mpira wa Tanzania utakuwa? Ligi haiwezi kuendelea kwa mpira huu wa hovyo.”
“Watu wanatumia gharama kubwa kuendesha timu, walipa mishahara, gharama za usafiri, chakula na malazi lakini mtu mmoja anaharibu kila kitu.”
“TFF na bodi ya ligi kwa nini wanaruhusu mambo haya? Mpira wenu hauwezi kuendelea kwa mambo ya namna hii.”
Kocha wa Coasta Union JUMA MGUNDA
“Nachelea sana kuwazungumza hawa (waamuzi) sijui wanafanya kusudi, bahati mbaya au ni vipi lakini mwisho wa yote mechi ilikuwa nzuri na ngumu tunashukuru.”
↧