MANCHESTER, ENGLAND
KLABU ya Molde ya
Ligi Kuu Norway imemtaka kocha wa muda
wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, abaki England kuendelea kuifundisha timu hiyo, baada
ya mafanikio aliyoyapata tangu ateuliwe
kurithi mikoba ya Kocha Jose Mourinho.
Uamuzi huo unatokana na Solskjaer, kuwa msaada tangu
atue Manchester United, ambapo amefikisha
michezo nane bila kufungwa.
Mashabiki wa kocha huyo ambaye aliwahi
kuichezea Manchester United kwa mafanikio wamekuwa na raha tangu kufukuzwa kwa Mourinho Desemba mwaka jana.
Molde ilikubali kumtoa kwa mkopo kocha huyo wakiwa katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Norway msimu
huu, lakini inadaiwa kuwa wanaweza kumwachia moja kwa moja kutokana na
mafanikio anayopata akiwa Manchester
United.
“Nilimpigia simu mmiliki wa Molde, alinieleza Manchester United inanihitaji na ukweli ni kwamba anafahamu hii ndiyo ndoto yangu, alisema: ‘Endelea kuwa na furaha tafadhali usirudi!
“Viongozi wote wananitakia kheri hapa United, wanatambua hapa ndio nyumbani, kama nitarudi pia Molde nitafanya mambo makubwa nikiwa huko lakini itategemea,” alisema Solskjaer.
Solskjaer alikishuhudia kikosi chake
kikifikisha michezo nane bila kufungwa baada ya kupata sare ya kufungana mabao
2-2 na Burnley.
↧