Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Mkutano Simba wasogezwa mbele

$
0
0
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM MKUTANO Mkuu wa wanachama wa klabu ya soka ya Simba uliopangwa kufanyika Julai 10, mwaka huu katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Masaki, jijini Dar es Salaam, umesogezwa mbele hadi Julai 31, mwaka huu. Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, ilieleza kwamba  uamuzi wa kuahirishwa kwa mkutano huo umetokana na sababu kubwa ya uongozi kutaka kuwajibika zaidi kwa upande wa timu inayojiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Alisema uongozi umefanya mabadiliko hayo uweze kuelekeza nguvu zake kukiandaa kikosi kwa ajili ya mazoezi. “Tunaomba radhi kwa wanachama kutokana na usumbufu uliojitokeza, lakini tunakiri kwamba mambo haya yanafanywa ili kuongeza ufanisi ndani ya klabu yetu,” ilieleza taarifa hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>