Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live

Iran Yasema Mashambulizi ya Kimtandao Yaliyofanywa na Marekani Dhidi Yake Yamefeli na Hayajaleta Madhara Yoyote

$
0
0
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya kompyuta ya Marekani dhidi ya mfumo wa makombora wa Iran yameshindwa kuleta madhara na kwamba mwaka jana pekee Tehran ilifanikiwa kuvunja makumi ya mamilioni ya mashambulizi ya kompyuta dhidi yake.Waziri wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano wa Iran, Bw. Mohammad Javad Azari Jahromi ameandika leo Jumatatu katika mtandao wake wa Twitter kwamba vyombo vya habari vimeuliza iwapo mashambulizi ya kompyuta yanayodaiwa kufanywa na Marekani dhidi ya Iran yamefanyika au la? "(Napenda kujibu kwamba) wamejaribu sana lakini hadi hivi sasa hakuna shambulio lao lolote lililofanikiwa." AmesemaSiku ya Alkhamisi, vyombo vya habari vya Marekani vilidai kuwa nchi hiyo imeshambulia mifumo ya kompyuta inayoendesha maroketi na makombora ya Iran.Mashambulizi hayo ya kompyuta ya Marekani yalianza mara baada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kutungua ndege kubwa na ya kisasa kabisa ya kijasusi ya Marekani ya RQ-4A global Hawk, iliyoingia katika anga ya Iran kinyume cha sheria. Mfumo wa kujilinda na mashambulizi ya anga wa Khordad 3 wa Iran ndio uliotungua ndege hiyo ya Marekani katika anga ya Ghuba ya Uajemi, kusini mwa Iran.Waziri huyo amesema kuwa; "kwa muda mrefu sana tumekuwa tukikabiliana na ugaidi wa mashambulizi ya kompyuta kutoka kwa adui… mwaka jana tulifelisha mashambulizi milioni 33 kwa kutumia mfumo wetu maalumu wa kitaifa wa kujilinda na mashambulizi ya kompyuta."

Tanzanian woman kills Kenyan neighbour over a beer bottle

$
0
0
A 24-year-old Tanzanian woman was arrested over the weekend for allegedly killing a Kenyan woman, who was her neighbour, in south Delhi's Chhattarpur area after an argument between the two over lending a bottle of beer, police said.

AhadI Ya Rais Magufuli Ujenzi wa Barabara Geita Kutimizwa

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.Serikali imesema ahadi  ya  Rais Magufuli ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami  ya kutoka Kahama ,Bulyang’hulu   hadi Geita  yenye urefu wa  km   120 ipo palepale   na wakati wowote ujenzi unaweza kuanza.Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Elias Kwandikwa amesema hayo leo bungeni  jijini  Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Busanda ,Mkoani Geita Lolensia Bukwimba aliyehoji juu ya ahadi mbalimbali za serikali juu  ya ujenzi wa  barabara  kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Kahama hadi Geita ,ni lini Serikali  itaanza kutekeleza ahadi hizo.Katika majibu yake,Naibu waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe,Elias Kwandikwa  amesema ahadi ya Rais  John Pombe Magufuli katika ujenzi wa Barabara mbalimbali hapa nchini ikiwemo barabara ya Kutoka  Kahama,Bulyangh’ulu,Bukoli hadi Geita  ipo palepale na ujenzi unaweza kuanza muda wowote kuanzia sasa.Ikumbukwe  kuwa ,taratibu za kuomba kupandishwa  hadhi barabara zimeainishwa kwenye kanuni Na.43 na 44 za  mwaka   2009 za sheria ya barabara Na.13 Ya  mwaka  2007  ambapo  bodi ya mkoa  ya barabara  [Regional   Roads Boards] huwasilisha  maombi  kwa Waziri anayehusika na Barabara tajwa  kama itakuwa imekidhi vigezo  vya kupandishwa hadhi.

Cambodia building collapse: minister sacked, governor quits

$
0
0
The governor of Cambodia's Preah Sihanouk province has stepped down after a seven-floor building collapsed. Cambodian Prime Minister Hun Sen has also fired a top safety official for "lack of responsibility."

Mbunge CCM aivimbia serikali

$
0
0
JOSEPH Kasheku (Msukuma), Mbunge wa Geita (CCM), amevutana na serikali kuhusu utaratibu wa Jeshi la Polisi kutumia wanaume kukagua wanawake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Amelalamika kuwa, jeshi hilo limekuwa likitumia askari wa kiume na utaratibu unaotumika kwenye vituo vingine vya polisi kwenye majimbo mengine. Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo tarehe 24 Juni 2019, Msukuma amepinga ...

Uwanja wa ndege Saudi Arabia washambuliwa

$
0
0
Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wameushambulia uwanja wa ndege wa Abha ulioko Kusini Magharibi mwa Saudi Arabia.

Kiungo Kenny Ally aitosa Yanga kutua KMC

$
0
0
Yanga wamegonga mwamba kuinasa saini ya kiungo Kenny Ally yuko mbioni kujiunga na KMC kwa mkataba wa miaka miwili Juni 30.

Tatizo sio hawa kina Kagere, Wazawa ndo hawajielewi tu!

$
0
0
TAIFA Stars imeyumba kwa miaka kadhaa. Ni mwaka huu ndio tumeweza kufuzu fainali za Afcon 2019 na usiku wa leo itatupa karata yao ya kwanza dhidi ya Senegal katika mechi za Kundi C ambalo pia lina Algeria na Kenya zitakazovaana pia usiku wa leo.

Mastaa waitumie leo kuikumbuka kesho yao

$
0
0
TASNIA ya soka kwa wiki moja na ushei imekuwa na majanga ya kupoteza nyota wake wakiwamo wa zama hizo na wale waliopita. Said Mrisho ‘Zico wa Kilosa’, Barnabas Sekelo na juzi tu Said Mtupa wote wametangulia mbele ya haki.

Kesi ya Uchochezi Inayomkabili Tundu Lissu Yapigwa Kalenda

$
0
0
Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na wenzake watatu imeahirishwa baada ya mbunge huyo kuendelea na matibabu nje ya nchi.Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni Mhariri wa Gazeti la Mawio Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi..Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde amedai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 24,2019 kuwa shauri lilikuja kwa ya kutajwa na aliomba ipangwe tarehe nyingine.Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema washtakiwa wote wataendelea na dhamana yao na  shauri hilo limeahirishwa hadi Julai 24, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Ghazouani ashinda urais Mauritania

$
0
0
Tume ya Uchaguzi nchini Mauritania, imemtangaza mgombea wa chama tawala cha Mauritania, Mohamed Ould Ghazouani kuwa mshindi wa nafasi ya uras wa nchi hiyo.

Pierre Bemba arejea rasmi Congo

$
0
0
Mwanasisa maarufu wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Jean pierre Bemba, amerejea nchini humo akitokea uhamishoni mjini Brussels, Ubelgiji na kutangaza maandamano makubwa ya kudai haki.

Dk Tulia awakana wabunge walioshiriki semina ya NGO

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amesema Bunge la Tanzania halina taarifa ya mkutano wa taasisi zisizo za kiserikali (NGO) uliowahusisha wabunge 40  kwa ajili ya kupewa uelewa kuhusu muswada namba tatu wa marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2019 uliowasilishwa bungeni na Serikali ya Tanzania.

Schoolkids' phones are targets for fake news

$
0
0
Can teens be vaccinated against online disinformation? DW's Teri Schultz reports on creative educational efforts to help young media consumers fend off viral lies.

Ethiopia: Amhara attorney general dies from injuries after coup

$
0
0
The top prosecutor of Ethiopia's Amhara region has died from wounds he sustained during a coup attempt, media and medics report. The country is marking a day of mourning for four other officials slain amid the attack.

Stakeholders chat ways to improve central corridor performance

$
0
0
Trade, transport and logistics stakeholders are chatting possible ways to improve performance of the central corridor by reducing both time and cost.

Women's World Cup: African football boss seeks to investigate Cameroon behaviour against England

$
0
0
African football chief is calling for an investigation into Cameroon's behaviour against England, saying the issue "will be addressed".

Ethiopia Hunts for Plotter of Failed Coup in Amhara Region

$
0
0
Ethiopian security is hunting for the leader of the failed coup in the northern Amhara region where security is tight, as well as in the capital, Addis Ababa.   An internet shutdown remains in force across the country, following the assassinations of Amhara's governor and an adviser in the regional capital, Bahir Dar, Saturday. Later in Addis Ababa, Ethiopia's military chief was shot dead by his own bodyguard who also killed a visiting retired general.   Prime Minister Abiy Ahmed said that Brig. Gen. Asamnew Tsige masterminded the plot. Ethiopian officials said that Asamnew has not yet been arrested.   Ethiopian military have set up checkpoints in the capital and in the Amhara region.   Flags are flying at half-mast Monday which has been declared a day of national mourning following the four killings.  

Card B ang’ara tuzo za BET

$
0
0
Los Angeles, Marekani Wasanii mbalimbali na wanamichezo walijawa na furaha baada ya kutajwa wao ndiyo washindi katika vipengele mbalimbali katika tuzo za BET, mwanadada Card B akiongoza kwa kuchukua tuzo mbili kwa mpigo. Tuzo hizo amabazo hutolewa kila mwaka huwatunuku pia tuzo za heshima wasanii ikiwa ni kuheshimu na kutambua mchango wao katika sanaa ya muziki duniani na mwaka huu tuzo ya heshima ilienda kwa Mary J Blige ambaye alibubujikwa na machozi wakati msanii Rihanna aliyepewa nafasi ya kumkabidhi tuzo hiyo akimshukuru na kumtaja kama mwanamke shupavu na kuchangia uthubutu kwa wanawake wengi. Tuzo hizo zilitolewa Juni 23, Los Angeles, Marekani na mwanadada Card B aliibuka mshindi wa tuzo mbili, ambapo alishinda tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka (Invasion of Privacy) na Msanii Bora wa Hiphop wa Kike na alikuwa akiwaniakatika vipengele saba tofauti. Msanii Burna Boy kutoka nchini Nigeria, alishinda tuzo ya  Best International Act huku tuzo ya Best New international Act ikichukuliwa na Sho Madjozi wa Afrika Kusini Tuzo za Filamu zilienda kwa Michael Jordan kama Muigizaji Bora wa Kiume na Muigizaji Bora wa Kike ilichukuliwa na Regina King wakati  BlacKkKlansman ikichukua tuzo ya ilamu Bora. Katika tuzo za BET pia kulikuwa na kipengele cha michezo ambapo Mwanamichezo Bora wa Kike alichukua Serena William na Mwanamichezo Bora wa Kiume imechukuliwa na Stephen Curry. Katika kumuenzi msanii Nipsey Hussle  aliyefariki kwa kupigwa risasi Machi 31 mwaka huu, alipewa tuzo ya  Mwanamuziki Bora wa Hiphop marehemu ambapo aliwabwaga 21 Savage, Drake, J. Cole, Meek Mill na Travis Scott. Mwanamuziki Bruno Mars allibuka mshindi wa tuzo ya Msanii Bora wa Kiume  wa Pop na R&B na Msanii Bora wa Kike wa Pop na R&B ilichukuliwa na Beyonce. Aidha tuzo ya Kundi bora la Mwaka ilichukuliwa na Migos ambalo linaunfwa na wasanii watatu Quavious Keyate Marshall (Quavo), Kiari Kendrell Cephus (Offset) na Kirshnik Khari Ball (TakeOff). Tuzo ya Video Bora ya Mwaka ilichukuliwa na This is America ya msanii Childish Gambino huku Muongozaji Bora wa Video ikichukuliwa na Karena Evans. BET pia hutolewa kwa wasanii wacahanga manpo kwa mwaka huu tuzo ya Msanii anayechipukia ilichukuliwa na Lil Baby na tuzo msanii mdogo zaidi ilichukuliwa na Marsai Martin. Msanii Snoop Dogg alishinda tuzo ya Wimbo Bora wa Dini Na Unaohamasisha kupitia wimbo wake wa  ‘Blessing Me Again’ aliomshirikisha Rance Allan huku tuzo ya Wimbo Bora wa kushirikiana ikichukuliwa na Travis Scott kupitia wimbo wake ‘ wa ‘Sicko Mode’ aliomshirikisha Drake.  BET pia hutoa mafasi kwa watazamaji kuchagua video bora na kwa mwaka huu tuzo ya Chaguo la Watazamaji inayodhaminiwa na Coca Cola imechukuliwa na Ella Mai na wimbo wake wa ‘Trip’ na tuzo ya ‘BET HER’ imechukuliwa na wimbo wa ‘Hard Place’ ya H.E.R. Aidha tuzo hizo ziliongozwa na muigizaji Regina Hall na wasanii waliotumbuiza usiku huo ni Card B, Meek Mill, Mary J Blige, Migos, John Legend, Lil Bbaby, DJ Khalled ambaye alipanda jukwaan na timu yake kuimba wimbo wa Higher wakiwa wamevalia mavazi meupe kama ishara ya kumkumbuka marehemu Nipsey Hussle aliyeshirikiana naye katika wimbo huo.

Dkt. Migiro apokea vifaa vya mafunzo ya utabibu vyenye thamani ya Tsh. milioni 130

$
0
0
Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ulipokea kifaa muhimu cha kufundishia madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa sekta ya afya, pamoja na vitabu vya kitabibu kutoka katika Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza wanaofanya kazi katika sekta ya afya (Tanzania United Kingdom Health Diaspora Association - TUHEDA). Makabidhiano hayo yalifanyika jijini London tarehe 22 Juni 2019. Kifaa hicho ni sanamu ya binadamu ambayo inaendeshwa na programu maalumu za kompyuta zinazowezesha wataalamu mbalimbali wa afya kupata uhalisia wa hali ya magonjwa kama ambavyo wangeupata kutoka kwa mgonjwa aliye hai. Sanamu hiyo iliyopewa jina la ‘Msafiri’ na Ubalozi, ina uwezo wa kupumua, kutoa sauti ya mapafu kama mtu mwenye pumu, homa ya mapafu, au mapigo ya moyo yanayoweza kuashiria shinikizo la juu au la chini la damu, sawa na mgonjwa halisi. Upatikanaji wa sanamu hiyo umefanikishwa na mwanachama wa TUHEDA, Dkt. Nasibu Mwande, mtaalamu wa masuala ya ajali na magonjwa ya dharura (Accidents and Emergency), anayefanya kazi ya udaktari hapa Uingereza. ‘Msafiri’ ana thamani ya pauni za Uingereza zisizopungua 30,000 (sawa na shilingi za Tanzania zipatazo milioni mia moja), ana umbo la kawaida la binadamu na uzito wa kilo 60. Ubalozi umetaarifiwa kuwa sanamu hiyo ni ya kwanza nchini Tanzania katika ufundishaji wa kitabibu.Kupatikana kwa ‘Msafiri’ kutasaidia sana kupunguza makosa ya kibinadamu yanayoweza kufanywa na madaktari, wauguzi na wataalamu wengine kwani ‘Msafiri’ anaweza kutumika kutoa mafunzo ya kitabibu kwa mfano halisi wa magonjwa mbalimbali bila ya madhara ambayo yangetokea kama wataalamu wa utabibu wangetegemea kujifunza kupitia mgonjwa aliye hai. TUHEDA pia wamekabidhi vitabu muhimu mia tatu vinavyotumika kama rejea kwa madaktari wakati wa kuamua mgonjwa apewe dawa gani, dawa zipi zinaweza kutumika kwa pamoja bila madhara, na zitolewe kwa kiwango gani. Vitabu hivyo vina thamani inayokaribia pauni 9,000 sawa na shilingi za Tanzania zipatazo milioni 30.Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live