NA ZAITUNI KIBWANA
MGOMBEA wa nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi mkuu
wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha, amesema ana sera sita alizozigawanya makundi
matatu lakini kubwa ni kufanya mabadiliko ndani ya klabu hiyo.
Tiboroha ni miongoni mwa wagombea watatu waliobaki kuwania
nafasi ya mwenyekiti katika kinyang’anyiro hicho baada ya kujitoa kwa Elias
Mwanjala aliyedai ana majukumu mengi.
Akizungumza na BINGWA jana, Tiboroha alisema, ili Yanga
iweze kushindana na klabu kubwa ni lazima ifanye mabadiliko ya mfumo.
“Ni lazima Yanga ibadili mfumo iwapo inataka
kushindana na klabu kubwa barani Afrika kama TP Mazembe na timu nyingine zenye
mafanikio.
“Si vibaya kuiga mambo mazuri kama walivyofanya
Simba, sisi tulikuwa waasisi wa mabadiliko kipindi cha Mwenyekiti, Abbas
Tarimba, lakini hatukufanikiwa na sasa tunataka kurudia sera hiyo,” alisema.
Aidha, alisema mbali na mabadiliko ya muundo pia
sera yake ni kuwaunganisha Wanayanga kuwa kitu kimoja ili kuondoa tofauti zao.
“Hii ni timu ya wananchi, tutaanza kuongeza
mashabiki mpaka wanachama ili kuwaweka karibu na timu yao,” alieleza Tiboroha.
Pia alisisitiza jambo jingine kuwa ni kuandaa
mpango wa muda mfupi ambao utaleta tija kwa manufaa ya klabu hiyo wakati
wakijiandaa kubadilisha mfumo
↧