Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

HISTORIA, REKODI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA

$
0
0
LONDON, England MICHUANO ya Ligi ya Mbingwa Ulaya ilianzishwa mwaka 1952. Mwanzoni ni mabingwa wa nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) ndio waliokuwa wakishiriki, tena walikuwa wakianzia katika hatua ya mtoano. Mfungaji wa kwanza wa michuano hiyo Bao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya lilifungwa na Joao Baptista Martins wa klabu ya Sporting CP. Klabu inayoongoza kwa kulichukua Real Madrid ndiyo timu yenye mafanikio makubwa kwenye historia ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa imechukua taji hilo mara 11. Wanaofuata ni wakali wa Seria A, AC Milan, ambao wamelifungia kabatini mara saba.  Fainali iliyotazamwa na mashabiki wengi Ni mchezo wa fainali wa msimu wa 2012-13 ambao ulizikutanisha Borussia Dortmund dhidi ya Bayern Munich kwenye Uwanja wa Wembley, London, Uingereza. Mtanange huo unatajwa kutazamwa na mashabiki milioni 360 duniani kote. Hispania kidume Ligi ya Mabingwa Ulaya Klabu za Hispania zinaongoza kwa kutwaa taji la mashindano hayo zikiwa zimefanya hivyo mara 16. Ubingwa wa mashindano hayo umeshatua katika nchi 22 na 12 kati ya hizo zimechukua zaidi ya mara moja. Timu ya kwanza kuchukua ubingwa Real Madrid ndio timu ya kwanza kutwaa taji hilo na hiyo ilikuwa baada ya kuifunga Stade de Reims mabao 4–3. Wimbo wa michuano hiyo Kuna wimbo huwa unasikika kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Uliandikwa na Tony Britten na kiitikio chake kina maneno ya lugha tatu; Kiingereza, Kijerumani na Kifaransa, ambazo ndizo lugha rasmi zinazotambuliwa na shirikisho hilo. Wimbo huo una urefu wa dakika tatu na una beti mbili na kiitikio.  Mpunga wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Kwa ushindi wa kila mchezo wa kuwania kutinga hatua ya makundi, timu hupokea Euro milioni 2. Zinazopoteza mchezo wa kufuzu hatua hiyo, hulipwa Euro milioni 3. Kwa kila timu inayoingia hatua ya makundi, huweka mfukoni Euro milioni 12. Kushinda mechi moja ya hatua ya makundi kunaipa timu Euro milioni 1.5 na sare itaipa Euro 500,000. Pia, UEFA hutoa Euro milioni 5.5 kwa timu zilizoingia mtoano, Euro miloni 6 kwa zilizofika robo fainali na Euro milioni 7 hutolewa kwa zilizotinga nusu fainali. Mshindi wa pili huweka mfukoni Euro milioni 10.5 huku bingwa akikinga pauni milioni 15. Mchezaji aliyecheza mechi nyingi Mlinda mlango Iker Casillas ndiye mwanasoka aliyeingia uwanjani mara nyingi katika mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kipa huyo raia wa Hispania ameshacheza michezo 166 ya michuano hiyo. Anayefuata katika nafasi ya pili ni kiungo wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez, ambaye amecheza mechi 157. Mfungaji wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Akiwa amepasia nyavu mara 96, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, ndiye mfungaji wa muda wote wa mashindano hayo makubwa barani Ulaya. Nafasi ya pili inakamatiwa na hasimu wake Lionel Messi aliyefunga mabao 93. Kwa msimu huu, Messi ndiye kinara wa mabao akiwa amewatesa walinda mlango mara 10.  Anayeshika nafasi ya pili ni Edinson Cavani mwenye mabao. Mkali wa ‘asisti’ msimu huu Mpaka sasa ni Mbrazil Neymar ndiye anayeongoza kwa pasi za mabao asisti akiwa amefanya kazi hiyo mara saba.  Bingwa wa kucheza faulo msimu huu Franco Vazquez wa Sevilla anaongoza kwa kucheza rafu akiwa amefanya hivyo mara 19 sawa na Aleksandr Gatskan wa Rostov Rostov. Kadi za njano Anayeongoza kwa kulimwa kadi za njano msimu huu ni Marco Verratti wa PSG ambaye amekumbana na adhabu hiyo mara nne. Kadi nyekundu Hakuna mchezaji aliyelimwa kadi nyekundu zaidi ya moja tangu kuanza kwa msimu huu. Mastaa wafuatao wamepata adhabu hiyo mara moja kila mmoja: Jeremy Mathieu (Barca), Jan Gregus (Kobenhavn), Olivier Giroud (Arsenal), Mario Lemina (Juventus) na Geoffroy Serey Die (Basel). Leicester, Rostov zaweka rekodi msimu huu Kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Leicester City na Rostov ziliweza kuingia hatua ya makundi. Itakumbukwa kuwa hii ni mara ya kwanza pia kwa Leicester kucheza michuano hii mikubwa barani Ulaya na waliipata nafasi hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita wa 2015-16. The post HISTORIA, REKODI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA appeared first on Bingwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Trending Articles