Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

THE ROCK MCHEZA MIELEKA ALIYEPANIA KUGOMBEA URAIS MAREKANI

$
0
0
NA ALEX VULIVER, TSJ KWA wale wapenzi wa filamu za mapigano za kizungu na mchezo wa mieleka, ni wazi watakuwa wakimfahamu vizuri. Anajulikana kama The Rock ila kwa majina yake halisi anaitwa Dwayne Douglas Johnson, aliyezaliwa Mei 2, 1972 katika Mji wa Hayward, jijini California, nchini Marekani. The Rock ni mwigizaji, mtayarishaji, mwanamuziki na mwanamieleka. Mkali huyo kwa sasa ni baba wa familia ya watoto wawili ambao ni Jasmine na Semone, aliowapata baada ya kufunga ndoa na Dayn Garcia mwaka 1997. Hata hivyo, alitengana na mkewe huyo mwaka 2007 na kujikuta akianzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo Lauren Hashian ambaye yupo naye mpaka sasa. Baba wa mkali huyo, aliyejulikana kama Rock Johnson, ndiye aliyemfanya mwanawe kujikita katika mchezo huo kwa kumjengea misingi akiwa kama mwalimu wake akishirikiana na Pat Patterson na Tom Richard kwenye chuo cha mieleka kinachojulikana kama USWA (United States Wrestling Association) kilichopo Miami, Florida, nchini Marekani. Mafunzo hayo aliyapata mwaka 1995, mwaka 1996 alijiunga rasmi na Shirikisho la Mieleka Ulimwenguni (WWF) kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2002 na WWE (World Wrestling Entertainment). The Rock amepata mafanikio makubwa na kujijengea jina kupitia mchezo wa mieleka ambapo amewahi kuwa bingwa kwa kutwaa taji la dunia la uzito wa juu mara 11, mkanda unaojulikana kama WHC (World Heavy Weight Champion), huku akitumika kwenye matangazo mbalimbali na kumfanya kuwa mwanamieleka tajiri duniani. Mwaka 1999 aliingia rasmi kwenye tasnia ya filamu, hapo ndipo alijijengea jina zaidi Marekani na duniani kwa ujumla. Filamu zake kama Scorpion King, Fast and Furious, San Adreas na nyingine nyingi, zilimfanya kuwa mmoja wa waigizaji matajiri ulimwenguni. Nimekujuza kwa kifupi kuhusu huyu jamaa, pamoja na hayo yote kuna jambo linamuumiza kichwa, jambo gani? Wahenga walishawahi kusema: “Ndoto sio ile unayoota ukiwa umelala, bali ni ile inayokukosesha usingizi.” The Rock anatamani siku moja aliongoze taifa kubwa ulimwenguni, bila hata kutaja linajulikana nalo ni Taifa la Marekani. Hiyo ndiyo dhamira yake kubwa, kuona siku moja anakuwa Rais wa Marekani ambapo alishawahi kunukuliwa akisema: “Nitakapokua kiongozi nitakua na nafasi kubwa ya kuwasaidia watu, nafikiri itakuwa rahisi sana kwa sababu uchaguzi uliopita umeonesha chochote kinaweza kutokea.” Mkali huyo aliyasema hayo wakati Donald Trump alipotangazwa kama Rais mteule wa Taifa hilo kubwa duniani. Japo inaonekana kama ni ndoto, lakini ukweli ni kwamba hicho ni kama kitendawili ambacho The Rock anaweza kukitegua kwasababu muda wa kujipanga anao, sababu na sifa za kugombea anazo na uwezo wa kushinda anao pia kama alivyoweza Trump ambaye leo hii ndiye anayeishi White House ya Marekani. The post THE ROCK MCHEZA MIELEKA ALIYEPANIA KUGOMBEA URAIS MAREKANI appeared first on Bingwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 132783

Latest Images

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>