HUENDA klabu za Simba, Azam na Yanga zikaendelea kutamba katika Ligi Kuu Bara msimu ujao kutokana na kukosekana kwa mdhamini mpaka Agosti 22 wiki ijayo ambapo itaanza.
↧
Simba, Yanga kutamba Ligi Kuu
↧
Italy's populists dismiss Genoa bridge fears as 'fairytale'
Italy's Five Star Movement, now in government, claimed in 2013 that an imminent collapse was a "fairytale." Resignation calls in the wake of Genoa's bridge collapse are being resisted by road operator Autostrade.
↧
↧
Waziri Mkuu aagiza kukomeshwa vitendo vya ubambikizaji kesi wananchi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza ofisi za masuala ya sheria kuhakikisha kuwa vitendo vya ubambikizaji wa kesi vinakoma na mashauri yanayofikishwa mahakamani yanakuwa na ushahidi wa kutosha.
↧
Dk Mwakyembe apendekeza walimbwende waajiriwe ATCL
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harisson Mwakyembe amesema wizara yake inafanya majadiliano na Shirika la Ndege nchini (ATCL) ili kuwatumia wasichana wanaoshinda kwenye mashindano mbalimbali ya ulimbwende wafanye kazi kwenye shirika hilo.
↧
Mtoto wa Lowassa ajiondoa kinyang’anyiro cha ubunge Monduli
Kada wa Chadema, Fred Lowassa amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha wanaowania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge katika Jimbo la Monduli mkoani hapa.
↧
↧
Man who ‘wanted to bribe’ Lukuvi probed
Investigations in the case facing businessman Mohamed Kiluwa, who allegedly attempted to bribe the Lands, Housing and Human Settlements Development Minister William Lukuvi with $40,000 (Sh90 million) is yet to be completed.
↧
Africa’s weather forecast to go online
The African continent will be integrated to the global weather forecast system in an effort to improve its capability in meteorological observations. The online Observing Systems Capability Analysis and Review (Oscar) has more accurancy in weather predictions compared to the existing facilities at the poorly equiped meteorological stations.
↧
Data-based solution lab launched
A new solutions-driven research platform has been created to support financial service market actors using data.
↧
Retirees set to earn 5 per cent of delayed benefits, says regulator
Are you worried that it is it taking too long for you to get your social security benefits?
↧
↧
US voices concern about by-elections
The United States embassy in Dar es Salaam yesterday voiced its concern about how last Sunday’s parliamentary and civic by-elections were conducted in various parts of the country.
↧
ZAHERA ACHIMBA MKWARA
*Ataka wachezaji wanaowaza kufungwa na Simba wabaki nyumbani
*Tshishimbi amjibu kibabe
NA ZAITUNI KIBWANA, MOROGORO
BAADA ya kufanya mazoezi ya nguvu na kucheza mechi tatu za kujipima nguvu, kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewachimba mkwara wachezaji wake akiwataka wanaodhani watafungwa na Simba wabaki nyumbani.
Tayari Yanga imecheza mechi dhidi ya Mawezi Market na kushinda bao 1-0, Kilosa Kombaini ikashinda tena 1-0 na jana ilijitupa uwanjani dhidi ya Mkamba Rangers Morogoro.
Kocha huyo mwenye ‘confidence zake mjini’, ametamba kuwa hatishiki na majina makubwa ya wachezaji wa Simba waliosajiliwa msimu huu, kwani mpira hauchezwi na majina.
Simba imemsajili nyota wa Rwanda mwenye asili ya Kiganda, Meddie Kagere, ambaye alikuwa moto wa kuotea mbali katika michuano ya Sportpesa Super Cup akiwa na Gor Mahia ya Kenya, mwingine ni nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Zambia, Cletus Chama Chota, Hassan Dilunga, Paschal Wawa, Adam Salamba na Mohamed Rashid.
Lakini Zahera akizungumza na BINGWA jana kwenye kambi ya Yanga iliyopo Morogoro na kusema kuwa kikosi hicho kipo tayari kucheza na timu yoyote ile.
“Mpira ungekuwa unachezwa na majina basi Brazil ingebeba Kombe la Dunia, ila majina hayachezi mpira hata uwe na nani na nani ukishaingia uwanjani tu wote wanakuwa ni wachezaji, hivyo hatuhofii majina yao tupo tayari kucheza na yeyote yule,” alisema.
“Kuna wachezaji wameanza kujilalamisha eti Simba sijui nini wazuri, mara watatufunga, sasa nawaambia ikifika hiyo siku ni bora wabaki nyumbani na wasiangalie mpira kwenye televisheni wasubiri dakika 90 za mchezo,” alisema Zahera.
“Si wachezaji pekee, hata shabiki anayewaza kuwa tutafungwa nawaambiwa wabaki nyumbani, wasije kabisa uwanjani kwani sisi hatuangalii tunacheza na nani,” alisema.
Zahera alisema kikosi hicho kwa sasa kina ujasiri wa hali ya juu wa kupambana na timu yoyote.
“Si Simba tu, tupo tayari kucheza na yeyote yule, awe mkubwa au mdogo kwa sababu tunajiamini kutokana na mazoezi tuliyofanya,” alisema.
Yanga inatarajia kurejea Dar es Salaam kesho kwa ajili ya mchezo wao dhidi USM Alger, utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakuwa ni wa kukamilisha ratiba kutokana na kuburuza mkia katika Kundi D la michuano hiyo wakiwa na pointi moja, huku Gor Mahia wakiongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao wakiwa sawa kwa pointi nane na USM Alger na Rayon Sports wakishika nafasi ya tatu kwa pointi tatu.
The post ZAHERA ACHIMBA MKWARA appeared first on Bingwa.
↧
Mwl. Nyerere: Najua mtapata shida
MANENO ya mwisho ya Mwalimu Julius Nyerere ambapo yaliyopata kuandikwa ni pamoja na haya, “Najua ugonjwa huu sitapona, Watanzania watapata shida, lakini nitawaombea kwa Mungu.” Anaandika Mchambuzi Wetu … (endelea). Maneno haya ya Mwalimu yanaonesha alivyoelewa vyema viongozi wajao. Wasiwasi wake ni uwezo mdogo wa viongozi kukabiliana na changamoto hizo bila ya ushauri makini. Miaka ya bila mwalimu ...
↧
MAREKANI YSTOA TAMKO ZITO UCHAGUZI MDOGO
Na Waandishi wetu – dar es salaam
UBALOZI wa Marekani nchini, umeeleza kusikitishwa na vurugu na ukiukwaji wa sheria, vilivyojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita Jimbo la Buyungu na katika kata 36.
Taarifa iliyotolewa jana na ubalozi huo, ilisema; “Marekani imesikitishwa na uendeshaji wa chaguzi ndogo zilizofanyika nchini Tanzania Agosti 12, 2018.
“Taarifa za kuaminika zinaonyesha kuwa chaguzi ziligubikwa na vurugu zilizohusiana na uchaguzi, ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kukataa kwa baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwasajili wagombea kutoka vyama vya upinzani, vitisho vya polisi dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani, watu kukamatwa kiholela bila kuwepo vibali vya ukamataji na kukandamizwa kwa uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni katika kipindi chote kuelekea chaguzi hizo.
“Mambo haya yanakwaza haki ambazo Katiba ya Tanzania imewapa raia wake na kuhatarisha amani, utulivu na usalama nchini na katika eneo lote la kanda.”
Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Athuman Kihamia, alisema bado hajaliona tamko hilo ila wanajipanga kuelezea hali ya uchaguzi huo wa marudio ikiwamo kulijibu tamko hilo.
“Naomba uvute subira, bado sijaliona hilo tamko, na suala la uchaguzi, tutaeleza vyote ikiwa ni pamoja na kujibu tamko hilo la Marekani,” alisema Kihamia.
MTANZANIA lilimtafuta bila mafanikio Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Suzan Kolimba, kupata ufafanuzi wa wizara kuhusu masikito hayo ya Marekani.
Licha ya kupigiwa simu mara kadhaa hakupokea, na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakuujibu.
Naye Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Mindi Kasiga, alipotafutwa alisema yupo likizo, hivyo hawezi kuzungumza lolote.
CHADEMA
Juzi Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, ambaye alikuwa Buyungu kuendesha kampeni za uchaguzi huo, alisema wanaendelea kukusanya fomu za matokeo kutoka kwa mawakala wao.
Alisema hadi wakati huo walikuwa na matokeo ya kata tisa, ambayo alidai kuwa yalionyesha walipata kura zaidi ya 18,000, wakati zilizotangazwa ni 16,000.
“Matokeo haya ni tofauti kabisa na waliyotangaza, katika hizi kata tisa ambazo tulifanikiwa kupata matokeo yake, ukijumlisha kata tisa tu, sisi tuna zaidi ya kura 18,000 na CCM wana 19,000.
“Haya matokeo hayajumuishi kata ambazo ni ngome yetu, ambazo mawakala wetu walinyimwa fomu za matokeo, kwenye kata yetu ya Katanga, huko ofisi iliunguzwa, mtendaji akatokomea na fomu, sasa waambieni CCM wawaambie wawaonyeshe hizo fomu,” alisema Mrema.
CCM
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, alisema licha ya kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 58 Buyungu, lakini walishinda kwa tabu.
“Buyungu tulipata tabu kidogo kwa sababu mgombea aliyekuwapo alikuwa anapendwa sana na wananchi, alikuwa ni mwalimu, wanampenda tu na wamemtumia wale watu,” alisema.
Alisema wakati wa kampeni kila kata ilipangiwa mbunge maalumu wa CCM na wote walifanya kazi nzuri kwa kufanya mikutano zaidi ya 25, kuzungumza na viongozi wa dini zaidi ya 12, walimu wa sekondari na shule za msingi, bodaboda na wafanyabiashara wadogo wadogo.
UCHAGUZI ULIVYOKUWA
Uchaguzi wa udiwani katika Kata ya Kaloleni Jimbo la Arusha Mjini, uliingia dosari baada ya kuibuka vurugu huku baadhi ya watu wakiripotiwa kuchomwa visu.
Pamoja na vurugu hizo, gari la mgombea udiwani wa Kata ya Daraja Mbili, Masud Sungwa (Chadema), lilidaiwa kuchomolewa tairi, huku watu waliokuwa ndani walilazimika kushuka na kukimbia kunusuru maisha yao.
Katika vurugu hizo, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kaloleni, lddi Mussa, alidai kuchomwa kisu begani na kujeruhiwa maeneo ya mwili wake na mmoja wa watu aliyekuwa katika kundi la wafuasi wa Chadema waliokuwa wamemzingira.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi, alisema mgombea wa Chadema alishambuliwa na watu wasiojulikana.
“Amekwisha kufungua kesi tayari kituo cha polisi kwa ajili ya kuanza uchunguzi. Aliyechomwa kisu ni mwanachama wa CCM alikuwa eneo la Mianzini jijini hapa,” alisema.
ACT WATOA TAMKO
Katika hatua nyingine, jana Chama cha ACT-Wazalendo kimemvaa Dk. Bashiru, kikidai amepotosha umma kwa kusema CCM imeshinda uchaguzi huo.
Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Doroth Semu, alisema Agosti 13, mwaka huu katika mkutano na waandishi wa habari, Dk. Bashiru alifanya upotoshaji wa wazi ambao hawakudhani kama ungetolewa na mtu wa hadhi yake.
Aliyataja baadhi ya maeneo aliyodai kuwa yalipotoshwa na Dk. Bashiru kuwa ni pamoja na kuvurugwa kwa uchaguzi wa marudio, utekelezaji wa Ilani ya CCM.
“Katika taarifa yake, Dk. Bashiru alizungumzia aliouita ushindi wa ‘mia kwa mia’ wa CCM kwenye uchaguzi wa marudio. Ukweli wa mambo ni kwamba CCM haijashinda kwa haki Buyungu na kwenye kata nyingi katika uchaguzi huu.
“Mfano wa wazi ni wagombea wanane wa vyama vya upinzani kwenye kata za Tunduma kutangazwa kuwa si raia ili CCM iweze kupita bila kupingwa kwenye kata hizo.
“Wapinzani tulibughudhiwa na mikutano yetu kuvamiwa na polisi. Mfano halisi ni wa wagombea wote wa vyama vya upinzani katika Kata ya Turwa wilayani Tarime kuzuiwa kufanya kampeni siku mbili za mwisho ili kutoa mwanya kwa CCM kushinda,” alisema Doroth.
Alisema pia katika uchaguzi huo wa Agosti 12, licha ya mgombea wa upinzani katika Jimbo la Buyungu kushinda, matokeo yaliyotangazwa na tume yalimpa ushindi mgombea wa CCM.
Doroth alisema kutokana na hali hiyo, yanapaswa kufanyika mabadiliko kwenye mfumo wa siasa na vyombo vya dola, ikiwamo kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
“Tunasisitiza mapendekezo haya yafanyiwe kazi kwa salama ya nchi yetu. Vinginevyo nchi inakwenda kupata tabu sana kuelekea 2020,” alisema Doroth.
Katika uchaguzi wa Buyungu, mgombea wa CCM, Christopher Chiza alitangazwa mshindi, huku chama hicho kikishinda udiwani katika kata 36 na nyingine 41 kikipita bila kupingwa baada ya wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.
MSEMAJI WA SERIKALI
Baada ya taarifa hiyo ya Marekani kuanza kusambaa mitandaoni, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi, kupitia ukurasa wa Twitter, alisema wanajiridhisha juu ya uhalali wa tamko hilo kisha watatoa tamko.
Maelezo hayo ambayo Dk. Abbasi aliyasambaza mwenyewe kwenye makundi mbalimbali ya mtandao wa Whatsapp, yalisema; “kuna taarifa inasambaa kuhusu kinachodaiwa ni taarifa ya ubalozi mmoja kuhusu masuala ya ndani ya nchi. Tunajiridhisha, tutatoa tamko punde.”
Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni, Dk. Abbasi alikuwa hajatoa tamko lolote.
Habari hii imendaliwa na GABRIEL MUSHI, ZAKIA NDULUTE (UOI), FRANK KAMUGISHA (SAUT) NA LEONARD MANG’OHA
↧
↧
BASHIRU AWAJIBU WANAODAI USTAHIMILIVU UMEMUISHA
NA ANDREW MSECHU-Dar es Salaam
SIKU mbili baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, kufanya mkutano na waandishi wa habari na baadhi ya watu kudai kwamba sifa ya kuibua mijadala aliyonayo imeingia dosari kutokana na namna alivyojibu maswali ya wanahabari, mwanazuoni huyo ameibuka na kusema hajutii.
Katika mahojiano kwenye kipindi cha televisheni cha 360 kinachorushwa na Clouds Tv, Dk. Bashiru alisema alionyesha ukali na hajutii jambo hilo.
“Kuna yule (anataja chombo chake) alinikera kwa kuhoji elimu yangu, akisema kwamba sijaitumia vizuri kukidhi matarajio na kwamba mimejibu rojorojo, huko ni kuwatukana Watanzania ambao wamenisomesha.
“Anapohoji uwezo wangu kielimu anawahoji walionisomesha kwa vipesa vyao, kwa kuwa nimesoma katika shule za umma tangu mwanzo,” alisema.
Alisema yeye ni mwanataaluma ambaye hakuwahi kununua mtihani wala kushindwa popote, akiwa na maandiko yake ambayo mtu anaweza kuyakosoa, lakini yanakubalika ubora wake.
Dk. Bashiru alisema huenda sehemu ya maarifa hayo ndiyo yaliyompa nafasi aliyonayo sasa, kwahiyo si sahihi kuhoji rejareja kwa kuanza na swali linalokera.
Alisema Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, alimpigia simu na kumweleza kuwa alipoulizwa swali hilo alipaswa kushuka badala ya kupanda na yeye akamjibu aliamua kupanda naye (mwandishi) na angepata nafasi angepanda naye zaidi.
“Lengo lilikuwa ni kutuma ujumbe kwamba wanapokusanyika kuzungumza, waheshimiane kwa sababu masuala ya mijadala yanahitaji kusikilizana,” alisema.
Alisema mijadala ni tofauti na porojo, kelele na mizaha katika mazungumzo, lakini mkutano wake na waandishi wa habari ulikuwa ni fursa muhimu kwao na yeye pia katika kuwasiliana na umma.
“Lakini mimi sikuridhika na naamini waandishi pia hawakuridhika,” alisema.
Kuhusu swali aliloulizwa kwamba kama CCM imeshindwa kuheshimu katiba yao ni vipi kitaheshimu ya nchi, alisema anamfahamu mwandishi aliyemuuliza swali hilo kuwa ni mwanachama wa Chama cha CUF na kwamba swali lake lilikuwa na mwelekeo wa kiitikadi.
“Hawa wanahabari walichukua mwelekeo wa kiitikadi na kuwakosesha watazamaji wasaa wa kupata ufafanuzi mzuri kwa namna swali linavyoundwa,” alisema.
Akizungumzia ustahimilivu wake kisiasa, Dk. Bashiru alisema anaweza kuvumilia jambo ambalo halimuui, lakini hawezi kuvumilia lile analoona linamuua na kwamba atakapoona anauawa atajitetea ili aendelee na mijadala.
SIASA ZA MATUSI
Akizungumzia siasa za matusi, Dk. Bashiru alisema tatizo hilo la siasa za ugomvi, liliibuka katika vyama vyote wakati wa uchaguzi mkuu, lakini tatizo lilikuwa kubwa zaidi CCM.
Alisema pia wanachama wengi wa chama hicho waliondoka kwa sababu kilitengeneza mfumo ambao bila kuwa na fedha ni vigumu kupata uongozi na kwamba baadhi walitaka vyeo ili wapange safu zao.
HAMAHAMA VYAMA
Kuhusu kuhama kwa wabunge, madiwani na viongozi wengine wa upinzani na kujiunga na CCM, alisema vyama husika vijitathimini kwanini watu hao waondoke kwao.
“Iweje ndani ya muda mfupi vinakimbiwa na wanachama na kukimbilia mahala pengine?” alihoji.
Dk. Bashiru alipoulizwa kama anadhani ni muhimu nchi ikarudi kwenye mfumo wa chama kimoja, alisema; “wingi wa vyama siyo demokrasia, umadhubuti wa mfumo wa vyama vingi ndiyo suala muhimu.
“Bado mfumo wetu wa vyama vingi ni legelege na vyama havijakua kitaasisi, hata CCM bado inabidi kuimarishwa kuwa chama madhubuti.”
Alisema hata kama vyama vitapukutika na kubaki viwili, haoni kama ni faida au hasara kwa kuwa itategemea vinavyobaki vinatoa mchango gani na kwamba kinachohitajika ni wananchi kuamua.
KUWA KATIBU MKUU CCM
Alipoulizwa kama anadhani CCM itambadilisha kutoka kwenye umahiri wake wa hoja na uadilifu ama yeye ndiye atakayekibadili, alisema alipokubali kutumikia nafasi aliyopewa, alikuwa amejiridhisha chama hicho kilikuwa kimeanza kubadili mwelekeo wake.
Alisema kama kingekuwa hakijabadili mwelekeo wake, aidha asingekubali kutumikia nafasi hiyo ama angekubali kwa shingo upande.
Dk. Bashiru alisema kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, alikuwa amekutana mara moja tu na Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli, siku alipokuwa akizindua mabweni mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Kabla ya hapo sikuwa nimewahi kukutana naye na pia baada ya pale sikukutana naye tena, mpaka alipotumia njia zake kuona nafaa na kunichomoa huko nilipokuwa,” alisema Dk. Bashiru.
↧
PROFESA KABUDI ATANGAZA MABADILIKO MFUMO MAWAKILI
Mwandishi wetu
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kuanzia sasa mawakili walioko kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wanasheria wote katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi za Serikali watakuwa ni Mawakili wa Serikali.
Alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dodoma jana.
“Kwa miaka mingi kumekuwa na ombwe la usimamizi wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma. maamuzi mengi yamekuwa yakifanyika pasipo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuwa na taarifa. Mambo yanapoharibika ndio Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inataarifiwa ili kuokoa jahazi,” alisema.
Alisema hali hiyo kwa miaka mingi imekuwa ikiisababishia Serikali kuingia kwenye migogoro na kuingia hasara.
“Baada ya mabadiliko haya, wanasheria wote walioajiriwa katika utumishi wa umma wanakuwa wanafanya kazi na kutumia mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndani ya wizara zao, taasisi zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa,” alisema.
“Vilevile wanasheria hao watakuwa chini ya uangalizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nia ya mabadiliko haya ni kumuwezesha Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe na usimamizi juu yao na kuwazuia kufanya kazi bila kufuata maelekezo yake.”
Prof. Kabudi alisema mashirika yote ya kimkakati kama vile Bandari, Tanesco nayo pia yataletwa chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuepuka kuitia Serikali hasara.
“Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye mashirika haya, lakini kuna maamuzi yanafanyika wakati Ofisi ya Mwanasheria Mkuu haina taarifa,” amesema.
“Kutokana na marekebisho hayo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaratibu na kusimamia mawakili wa Serikali walio katika ofisi hiyo na wanasheria wote katika wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi za Serikali ambao sasa watakuwa ni mawakili wa Serikali.
Aidha, mawakili wa Serikali walio katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali watakuwa chini ya uratibu na usimamizi wa Mkurugenzi wa Mashtaka na Wakili Mkuu wa Serikali,” amesema.
Alisema marekebisho hayo yanakusudia kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa mashtaka ya jinai nchini hususani utekelezaji wa azma ya Serikali ya kutenganisha shughuli za upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.
“Kuanzishwa kwa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kunalenga kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa mashauri ya madai na kuiwezesha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuimarika katika weledi na ubobezi wa kitaalamu katika kuishauri Serikali na kuandika miswada ya sheria kwa kuzingatia mabadiliko makubwa katika tasnia ya sheria kitaifa, kikanda na kimataifa,” ameongeza.
Hata hivyo, Prof. Kabudi alisema mabadiliko yoyote hayawezi kuleta matokeo yaliyokusudiwa kama watendaji hawatabadili mtizamo wao. Ni kweli muundo uliobadilishwa ulikaa kwa miaka mingi na inawezekana mambo mengi yalikuwa yanafanyika kwa mazoea.
“Kutokana na mabadiliko haya, tunakiri kuwa mitizamo yetu na ya watumishi wenzetu lazima ibadilike. tumejipanga kuhakikisha kuwa watumishi hawafanyi kazi kwa mazoea ili wasiwe na tashwishwi wala ajizi katika kutekeleza majukumu ya umma,” alisema.
↧
MTIBWA KUANZA KUPUNGUZA DENI WIKI HII
NA SALMA MPELI
UONGOZI wa Mtibwa Sugar, kupitia Mkurugenzi wake Mkuu, Jamal Bayser, unatarajiwa kuanza kulipa deni lao kwa timu ya Santos ya Afrika Kusini wiki hii.
Akizungumza na BINGWA jana, Bayser alisema wamekubaliana kulilipa deni hilo kwa awamu tatu tofauti na kulimaliza, kabla ya kuanza kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mtibwa ilifungiwa kushiriki michuano hiyo baada ya kushindwa kukipeleka kikosi chao mwaka 2003 kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ni baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 kwenye mechi ya awali jijini Dar es Salaam.
“Tunatarajia wiki hii kuanza kulipa awamu ya kwanza ya deni letu, ili kulimaliza mapema kabla ya michuano ya Shirikisho haijaanza,” alisema Bayser.
Mtibwa wanatakiwa kulipa Dola 15,000, ambazo ni sawa na Sh milioni 34 za Kitanzania, kwa ajili ya fidia dhidi ya timu ya Santos.
Katika hatua nyingine, Bayser alisema kikosi cha Mtibwa kinatarajiwa kuondoka leo kwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
Mtibwa, ambao ni mabingwa wa kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) na Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara, zinatarajiwa kushuka dimbani Jumamosi hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo, katika mchezo wa kuashiria kufunguliwa rasmi kwa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, inayotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.
The post MTIBWA KUANZA KUPUNGUZA DENI WIKI HII appeared first on Bingwa.
↧
TPLB YATOA UFAFANUZI MDHAMINI LIGI KUU
NA WINFRIDA MTOI
BODI ya Ligi Tanzania (TPLB), imeweka wazi kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao itaanza bila kuwa na mdhamini mkuu wakati wakiendelea na mazungumzo na makampuni kadhaa ili yaidhamini ligi hiyo.
Awali ligi hiyo ilikuwa ikidhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo mkataba wake umemalizika na tayari wameanza mazungumzo, lakini hadi sasa hawajafikia makubaliano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura, alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na kalenda yao ya mashindano kuwabana.
Alisema kalenda ya ligi kulingana na mashindano mengine inatakiwa kuanza kuanza Agosti 22, mwaka huu na wameshawasiliana na klabu kuwa wanaendelea na mazungumzo na mdhamini mkuu.
Aidha, Wambura alisema kati ya kampuni wanazozungumza nazo ni pamoja na mdhamini aliyemaliza mkataba wake, Vodacom na watakapofikia makubaliano muda wowote watatoa taarifa kwa klabu.
“Tunaanza ligi, lakini ifahamike kuwa mdhamini mkuu hatakuwapo, pia kampuni tunazofanya nazo mazungumzo tumekubaliana wataingia katikati mara tutakapofikia mwafaka, waliopo kwa sasa, Benki ya KCB na Azam TV ni wadhamini wenza,” alisema Wambura.
Hata hivyo, alikiri kwamba ligi kuanza bila kuwa na mdhamini mkuu itakuwa na changamoto, lakini tayari wamezipa taarifa klabu kutokana na hali hiyo, hivyo hata vifaa zitajigharamia zenyewe.
“Kwa sasa ligi itaitwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na hata jezi za timu pale inapokaa nembo ya mdhamini mkuu patabaki wazi, tunajua kuna changamoto ya kifedha, lakini tunazihakikishia klabu mdhamini mkuu atapatikana,” alisema Wambura.
Katika hatua nyingine, TFF kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi imerejesha mfumo wa tiketi za wanafunzi katika mechi za Ligi Kuu msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.
Akizungumzia uamuzi huo, Wambura alisema unalenga kutoa nafasi kwa vijana kuangalia mpira na wamefanya hivyo kutokana na programu zao za kuwahamasisha kwa kuwapa nafasi za kushuhudia ligi kwa kulipa nusu kiingilio.
Aidha, alisema tiketi hizo zinawalenga hasa wanafunzi wa shule za sekondari kwa sababu ili kuzitumia lazima uwe na kitambulisho cha shule unayosoma.
“Hizi tiketi zilikuwapo kipindi cha FAT (Chama cha Soka Tanzania) zikaondolewa, lakini msimu ujao zitarudishwa, mfumo huu pia utaepusha usumbufu kwa wale wanaokuja na watoto uwanjani, kwani watakuwa na jukwaa lao maalumu,” alisema Wambura.
The post TPLB YATOA UFAFANUZI MDHAMINI LIGI KUU appeared first on Bingwa.
↧
↧
Ma-DC wadaiwa kuitumia vibaya sheria ya kifungo saa 48
Amri ya wakuu wa wilaya kuwaweka ndani, baad-hi ya viongozi wa serikali na wale wa kisiasa imeendelea kujitokeza huku wadau wakikosoa suala hilo na kutaka wakuu hao watumie njia ya kuwaonya na si kuwakamata.
↧
SSRA: Serikali ilifikia ukomo kukopa mifuko ya hifadhi za jamii 2014
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema Serikali ilifikia kikomo cha ukopaji mwaka 2014 baada ya kukopa zaidi ya kiwango kinachotakiwa.
↧
Mabadiliko Polisi yamhamisha RPC Msangi Mwanza
Baada ya miezi 28 ya kulitumikia Jeshi la Polisi mkoani Mwanza akiwa mkuu wake, Kamanda Ahmed Msangi amehamishiwa makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.
↧