Wachezaji wa Chelsea, Ross Barkley na Antonio Rudiger, walishindwa kuungana na wenzao kurudi London kutoka Burnley kutokana na kushindwa kutoa kipimo cha mkojo baada ya mechi yao dhidi Burnley.
↧
Haja ndogo yawazuia wachezaji wa Chelsea kupanda ndege
↧
Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha
Wachezaji nyota wa kutoka Afrika wa zamani na wa sasa wametoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha aliyefariki katika ajali ya ndege.
↧
↧
Ndege ya abiria Boeing 737 yathibitishwa kuanguka Indonesia
Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea na operesheni za uokoaji katika bahari karibu na mji wa Jakarta baada ya ndege ya Shirika la ndege Lion Air iliyokuwa na abiria 189 kuangukia baharini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa Jakarta.
↧
Wazee Wamfanyia Tambiko Dr Kigwangalla
NA ANDREW CHALE, NZEGA WAZIRI wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewashukuru viongozi mbalimbali wa dini Nchini kwa dua na maombi yao kwa kipindi chote alichopata ajali hadi sasa kupona na kurejea tena na majukumu yake.Akizungumza katika mkutano wake wa pili uliofanyika katika Kata ya Lusu Tarafa ya Nyasa iliyopo kwenye jimbo lake hilo la Nzega Vijijini, jana Oktoba 28, 2018, Dkt. Kigwangalla amewashukuru viongozi hao wa dini pamoja na Wazee wa Mila kwani wao wamekuwa chachu kwenye kupona kwake tokea alipolazwa Hospitali kwa zaidi ya miezi miwili kwa kuuguza majeraha ya mwili wake kutokana na ajali ya gari aliyopata Agosti 4, mwaka huu.Amesema viongozi wa hao wa dini pamoja na Wananchi kila mmoja kwa nafasi yake walikuwa ni wa kipekee na dua zao zimeweza kusaidia na kwa sasa amerejea kutoa shukrani na kupokea dua zao hizo kwani kwa sasa ameanza kufanya kazi.“Kwa sasa nimeanza kurudi kwenye majukumu yangu kama kawaida. Kwa hivyo nikaona kabla ya kuanza kuonekana nikiruka huku na kule kwenye majukumu ya kiwizara, nikasema hapana nirudi kwanza nyumbani nipate dua za wazazi wangu, dua za wazee na viongozi wa dini.Kwa tukio lile kwa sisi tunaoamini, ni mkono wa Mungu ulikuwa mahala pale” amesema Dkt. Kigwangalla.Aidha, Dkt. Kigwangalla amewatoa hofu wananchi wa jimbo lake juu ya watu waliokuwa wakipitapita jimboni kwa lengo la kulinyemelea na kutoa maneno ya kumkatisha tamaa.“Kwa waliokuwa wanatembea na wakikesha usiku kucha wakisubiri nife wameanguka. Mungu amesimama mbele yangu, mimi ni mzima naendelea kutekeleza majukumu yangu mdogomdogo mpaka nitakapokuwa imara kabisa. Sasa naanza upya” amesema Dkt. Kigwangalla.Pia amewahakikishia wananchi hao kuwa kazi za maendeleo ya jimbo hilo zinaendelea na wasaidizi wake wa ofisi ya Mbunge inaendelea kuratibu kwa ukaribu kabisa na milango ipo wazi.Katika hatua nyingine Wazee wa Mila na Watemi wakiongoza na Chifu Ng’wana Ng’washi wa Wasukuma walifanya tambiko la kichifu la kumtambikia ili akawe tayari kwa kazi za kulitumikia Taifa katika majukumu ya Kibunge na Uwaziri. Dkt. Kigwangalla yupo katika ziara ya kutoa shukrani na dua maalum kwa Wananchi wa jimbon lake hii ni tokea kurejea kutoka kuuguza majeraha ya mwili wake tokea kupata ajali Agosti 4, mwaka huu wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi Mkoani Manyara.
↧
Ngoma Africa Band ya Ujerumani Yaipongeza Bendi ya Twanga Pepeta Kutimiza Miaka 20
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inatuma salamu za pongezi kwa uongozi,wanamuziki na wapenzi wa bendi maarufu ya dansi Twanga Pepeta (African Stars) ya Dar-es-salaam kwa kutimiza miaka 20 katika medani ya muziki.Kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi ya Ngoma Africa band amemtaja mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Bi.Asha Baraka kuwa ni mfano wa kuigwa na ameudhiirishia ulimwengu kuwa ni "Iron Lady" aliyezalisha, kuibua nakulea vipaji vingi katika medani ya sanaa ya muziki, Ras Makunja pia alimtaja kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Bi.Luiza Mbutu ni mwanamuziki wa kuigwa ameweza kuishi katika bendi hiyo muda wote bila ya kuhama hama kama ilivyo tabia za wanamuziki wengi duniani,kwa kweli tunawapongeza sana sana Twanga Pepeta kwa kutimiza miaka 20 ya kuzaliwa kwake na kurudisha heshima ya muziki wa dansi nchini Tanzania alisema Ras Makunja mkuu wa Ngoma Africa Band yenye maskani nchini ujerumani
↧
↧
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Kalemani Awataka Wananchi Kuchangamkia Fursa ya Umeme Vijijini.
Waziri wa Nishati dk.Medard Kalemani akizindua umeme wa Rea katika kijiji cha Kikumbaitale wilayani chato kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Chato Msafiri Simion.Waziri wa Nishati Dkt .Medard Kalemani katika akipiga ngoma mara baada ya kuzindua umeme wa ReaMoja ya nyumba zilizowekewa umeme wakati wa uzinduzi huoWaziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani mara baada ya uzinduzi huo Waziri wa Nishati dk.Medard Kalemani amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya Umeme hasa vijijini ambapo gharama ya kuweka umeme ni shilingi 27000 katika vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi wa REA. Dkt Kalemani ameyasema hayo wakati wa akizindua umeme katika kijiji cha Kikumbaitale wilayani chato ambapo amesema serikali inakusudia kuipeleka Nchi katika uchumi wa Kati kupitia viwanda, hivyo amewataka wananchi Wa Chato kuanzisha mashine za kukoboa na kusaga sambamba na kufanya biashara mbalimbali ikiwemo biashara za saluni. Alisema uwepo wa umeme huo utakuwa fursa kubwa kwa wananchi kufungua biashara mbalimbali zitakazowaingizia kipato ikiwemo mashine za kusaga na kukoboa."Lakini pia niwaaambie pia fungueni na saluni kwani umeme huu muutumie kujiongezea kipato ambacho kitakuwa chachu ya kujiletea maendeleo katika eneo lenu “ alisema dkt kalemani na kuwapongeza viongozi wa TANESCO kwa kazi nzuri wanazofanya kwa kushirikiana na REA.Hata hivyo alisema wataendelea kufanya kazi bila kuchoka kwa kutembelea vijiji mbali mbali ambavyo miradi ya REA inapita ili kukagua maendeleo ya mradi na kuhakikisha vijiji vyote vilivyo ndan ya mradi vinapata umeme kwa wakati.
↧
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Chatoa Mkono wa Pole Kwa Uongozi wa Hoteli ya Uroa Bay.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Watoa Mkono wa Pole kwa Uongozi wa Hoteli ya Uroa Bay, kutokana na Ajali iliotokea wiki iliopia na kufariki Wafanyakazi wa Hoteli hiyo, Ujumbe huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Ndg. Ramadhani Ali Kichupa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Ndg Haidar Haji Abdalla, akitowa maelezo Katibu wa CCM wa Mkoa Kusini Unguja, Ndg.Suleiman Mzee (Charas) na kuutambulisha Ujumbe huo kwa Uongozi wa Hoteli hiyo.kulia Mmiliki wa Hoteli Mr. Andrea Balladini.
↧
Woman Blows Herself up in Central Tunis: State Radio
A woman blew herself up in the center of the Tunisian capital Tunis on Monday, state radio said.
A witness reported an explosion on the central Habib Bourguiba avenue where police were cordoning off the area near the capital’s landmark Municipal Theatre.
Ambulances could be heard rushing to the scene.
“I was in front of the theater and heard a huge explosion and saw people fleeing,” witness Mohamed Ekbal bin Rajib told
↧
Rights Group Accuses E.Guinea Security Forces of Thrashing Leader
Activists in Equatorial Guinea alleged Monday that plainclothes security forces snatched and beat up the head of their human rights and development organization at the weekend.
Alfredo Okenve was "sequestered... [and] mistreated by security forces wearing civilian clothes", the Centre for Studies and Initiatives for the Development of Equatorial Guinea (CEID-GE) said in a statement.
A relative of Okenve's, Analeto Medja, told AFP: "He was taking his brother to the airport. Four people stopped his car and forced him at gunpoint to get into theirs. They took him to some wasteland and beat him hard until he was bleeding, then they left him there."
Residents close to the scene took Okenve to a hospital in Bata, Equatorial Guinea's economic capital on Africa's Atlantic seaboard, Medja and other family members said.
The oil-rich country's political capital is Malabo on the island of Bioko, lying off the coast of Cameroon to the northwest of the mainland and its dense tropical forests.
The identity of the men in civilian clothes who attacked Okenve was unclear on Monday, but carrying firearms is tightly controlled by the iron-fisted regime of President Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, in power since 1979.
The affair was being followed widely on social networks on Monday, but there was no official reaction.
CEID-GE said it would file a formal complaint, denouncing the harassment of civil society in the former Spanish colony.
Okenve was arrested and detained for several days in April 2017 for celebrating the 20th anniversary of the CEID-GE. He was released after a bail payment of two million CFA francs (about 3,000 euros, nearly $3,500).
Human rights groups have repeatedly denounced Obiang Nguema, 76, for his repression of political opposition, independent civil society organizations and the media.
In February 2018, the European Union expressed concern at the "serious deterioration in the human rights situation" in Equatorial Guinea, which is also known for the lavish spending of Obiang's son and vice president, Teodorin Nguema Obiang.
A French court in October 2017 gave Teodorin Obiang a suspended fine of 30 million euros and a suspended three-year jail term after convicting him of looting public funds from his country to pay for a rich playboy's lifestyle in Paris.
↧
↧
Entrepreneurship key to unlocking economic development in Africa, Elumelu tells forum
Lagos. A total 5,000 African entrepreneurs, private and public sector leaders and the broader entrepreneurship ecosystem convened in Lagos on Thursday, October 25, 2018, for the annual Tony Elumelu Foundation (TEF) Entrepreneurship Forum. The event, which is the largest gathering of African entrepreneurs in the world, is a unique opportunity for bringing together young business talent, creating dynamic networks and transmitting the message to policymakers that a vibrant and responsible private sector will deliver economic transformation.
↧
PATORANKING AKUMBUSHIA VANESSA MDEE KUMLISHA UGALI
NA CHRISTOPHER MSEKENA
STAA wa muziki nchini Nigeria, Patrick Okorie ‘Patoranking’, amemtaja msanii Vanessa Mdee kama mtu wa kwanza kumlisha ugali walipokuwa nchini Kenya mwaka jana.
Patoranking ambaye mwishoni mwa wiki alifanya bonge la shoo katika kiwanja kipya cha burudani Buckets, Masaki jijini Dar es Salaam, aliliambia Papaso la Burudani kuwa wakati yupo na Vanessa Mdee katika mradi wa Coke Studio Afrika, ndiyo alianza kuvutiwa na ugali.
“Nakumbuka wakati tunajiunga Coke Studio, mimi na Vanessa alinifanya nile ugali, nikaupenda,” alisema Patoranking.
The post PATORANKING AKUMBUSHIA VANESSA MDEE KUMLISHA UGALI appeared first on Bingwa.
↧
VIDEO: Wema aongezewa machungu
Chama cha waigizaji mkoa wa Kinondoni (TDFAA) kimemfungia mwanachama wake Wema Sepetu kujihusisha na masuala ya filamu kwa muda wa miaka miwili.
↧
Tanzania, China zasherehekea miaka 50 ya ushirikiano sekta ya afya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema katika kipindi cha miaka mitatu, uwezo wa madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika kufanya upasuaji umeongezeka hadi kufikia asilimia 80 kutoka 45.
↧
↧
Daktari: Hakuna miujiza uliookoa maisha ya Glenn Hoddle
Daktari bingwa wa sauti, Injinia Simon Daniels (41), amesema hakufanya miujiza yoyote katika kumzindua Kocha wa zamani wa England, Glenn Hoddle.
↧
Washindi mashindano ya Voda kushindana kimataifa
Kwa muda mrefu, Vodacom imekuwa ikishiriki katika sekta ya michezo kupitia udhamini ambao imekuwa ikitoa kama ule wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambao ulikoma mwishoni mwa msimu wa 2017/2018.
↧
Angela Merkel kung'atuka madarakani mwaka 2021
Uamuzi huo wa bi Merkel unakuja baada ya chama chake kufanya vibaya katika chaguzi.
↧
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Afungua Maonyesho ya Wiki ya Viwanda Mkoani Pwani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosamara baada ya kutembelea banda la kampuni inayotengeneza reli mpya ya kisasa ya YAPI MERKEZ wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya Viwanda mkoani Pwani.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela Tuzo ya Udhamini Mkuu wa maonyesho ya Viwanda mkoani PwaniMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela cheti ya Udhamini Mkuu wa maonyesho ya Viwanda mkoani Pwani.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi maalum ya kumpongeza kwa kufanya ziara yenye mafanikio mkoani Pwani toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) mara baada ya ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya Viwanda mkoaniMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wadhamini wa maonyesho ya Wiki ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
↧
↧
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Akabidhi Zawadi Kwa Wanafunzi Waliopasi Michipuo Skuli ya Fuoni, Katika Sherehe ya Kuwaaga Iliofanyika Katika Viwanja Vya Skuli Hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita waliofanya vuzuri zaidi kwenye mitihani katika Sherehe ya kumaliza elimu msingi zilizofanyika katika skuli yao. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita waliofanya vuzuri zaidi kwenye mitihani katika Sherehe ya kumaliza elimu msingi zilizofanyika katika skuli yao.Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi ya mashine ya kufulia, feni na Jiko Walimu wastaafu wa skuli ya Fuoni msingi, Asha Khamis na Hemedi katika Sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliomaliza Darasa la sita zilizofanyika Skulini kwao.Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi ya mashine ya kufulia, feni na Jiko Walimu wastaafu wa skuli ya Fuoni msingi, Asha Khamis na Hemedi katika Sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliomaliza Darasa la sita zilizofanyika Skulini kwao.Baadhi ya Walimu wa Skuli ya Fuoni msing wakionyesha furaha yao katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliomaliza masomo ya darasa la Sita yaliyofanyika katika Skuli yao.Wanafunzi wa Skuli ya Fuoni msingi wakifuatilia Sherehe ya kuwaaga wanafunzi wenzao waliomaliza elimu ya msingi katika sherehe zilizofanyika katika skuli yao.Na Mwashungi Tahir Maelezo 29-10-2018Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alisema maendeleo ya elimu nchini yataendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ili kufikia matarajio yaliyokusudiwa katika muendelezo wa elimu.Hayo aliyasema huko katika Skuli ya Fuoni ya msingi A na B wakati alipokuwa akizungumza na walimu wazazi na wanafunzi kwenye uwanja wa skuli hizo katika sherehe ya kuwaaga na kuwazawadia zawadi wanafunzi wa skuli hizo waliofaulu michipuo darasa la sita 2017 pamoja na walimu waliostaafu.Alisema ushirikiano ni lazima kati ya walimu ,wazazi na wanafunzi katika kupatikana maendeleo na mafanikio ili yaweze kupatikana kama Serikali inavyokusudia na kuweza kufikia kiwango kinachotakiwa juu ya elimu.Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi baada ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 imechukuwa juhudi ya kuweka elimu bure ili lengo wanafunzi wafaidike nayo kwa wenye uwezo na wasio na uwezo .Aliwataka wanafunzi waliofaulu mchipuo kuingia kidato cha kwanza waongeze bidii wapasi vizuri katika kidato cha nne hadi kufikia cha sita na kuendelea na elimu ya juu zaidi ili waweze kuwa wataalamu wazuri Serikalini.“Jitahidini muendelee vizuri katika masomo yenu hadi kumaliza katika vyuo ili muweze kuwa wataalamu wazuri katika Serikali “.Alisema Mkuu huyo.Pia aliushukuru uongozi unaotoa mafunzo maalum ya kuwasaidia wanafunzi wanaofanya mtihani SSP Special Study Program na kuwajengea uwezo kuwaletea ufaulu watoto wengi kwa jitihada zao wanazozichukua na faida zinaonekana.Akitoa rai kwa walimu wa Skuli ya Fuoni msingi A na B kwa wale vijana wanaosoma mbali uongozi SSP irudishe twisheni hapa skuli ya karibu badala ya kuifatia Kiembe samaki kwa lengo la kupunguza gharama kwa wazazi na wao wanafunzi kwenda masafa marefu.Hata hivyo alisema Serikali inafanya juhudi za kila mara katika kuongeza madarasa na idadi ya walimu itaongezeka ili ifikie malengo yanayotarajiwa hapo baadae ya kupunguza idadi ya wanafunzi wengi katika madarasa.Nae Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Silima Haji wa Haji aliwahimiza walimu na wazazi pamoja na wanafunzi kuongeza mashirikiano katika kukuza elimu ili lengo linalotarajiwa liweze kufikiwa kwa ufaulu wa wanafunzi kwa wingi.Pia aliupongeza uongozi wa program SSP kwa jitihada wanazozifanya na kufanikiwa kuweza kupasisha wanafunzi wengi na kuwataka kuongeza bidii zaidi.Jumla ya wanafunzi 42 wa Skuli za Fuoni msingi A na B na wamepata zawadi za uniform sare za Skuli na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amewahidi kuwapa pesa za ushoni.Kwa upande wa walimu waliostaafu Asha Khamis Suleiman ambaye alizawadiwa mashine ya kufuliya aliwataka walimu wawe na mashirikiano katika utendaji wao wa kazi na kuwataka wajiepuswhe na majungu.Pia aliwaomba waache kufanya kazi kwa mazowea na wafuate miongozo ya kazi ili kwa lengo la kuifanikisha suala zima la ellimu.
↧
Taarifa ya Hali ya Mafuta Zanzibar
Na Mwashungi Tahir Maelezo. 29-10-2018.Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imewajuilisha wananchi kuhusu Meli ya MT East Wind inayotumiwa na kampuni ya Zanzibar Petrolium Limited (ZP) imewasili nchini ikiwa na Tani 900 sawa na lita 1,695,632. Ambapo taratibu za mafuta kusambazwa kwenye vituo tayari zimeanza kufanyika .Akitoa taarifa kuhusu hali ya mafuta Zanzibar kwa waandishi wa habari huko kwenye ofisi zao ziliopo maisara Mkurugenzi Mkuu ( ZURA) Haji Kali Haji akitoa ufafanuzi alisema hali halisi ya uwepo wa mafuta hapa nchini kuanzia Jumapili tarehe 28-10-2018 inaonyesha kwamba upande wa kisiwa cha Unguja kutakuwa na mafuta ya Petroli lita 1,295,632 yanayoweza kutumika kwa muda wa siku 7.Mafuta ya dizeli lita 2,047,914 yanayoweza kutumika kwa muda wa siku kumi na tatu na Mafuta ya Taa lita 362,517 yanayoweza kutumika kwa muda wa siku saba 7 .Aidha alisema meli hiyo baada ya kushusha mafuta inategemea kupeleka mafuta Pemba ambapo mafuta ya Petrol lita 400,000 yanayoweza kutumika kwa muda wa siku kumi na moja (11) , Mafuta ya Dizeli lita 250, 000 yanayoweza kutumika kweam muda wa siku kumi na moja (11).Alieleza kuwa meli hiyo inatarajiwa kurudi tena katika Bandari ya Mombasa kupakia Tani 1500 sawa na lita 2,000,000 za Mafuta ya Petroli itawasili trehe 04/11/2018.Alisema ZURA imesikitishwa na hali ya uhaba wa mafuta uliojitokeza ambayo imewasababishia wananchi kukosa huduma kikawaida , kutokana na hali hiyo ZURA inayaagiza Makampuni ya Mafuta kuhakikisha ya kwamba yanasambaza mafuta kwa haraka na kurejesha huduma hiyo kwa wananchi na kuhakikisha inapatikana bila ya usumbufu.Pia ZURA inawaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kueleza kwamba inafuatilia kwa karibu matengenezo ya Meli mbili zilizoharibika ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa mafuta nchini inarejea kama kawaida.Vile vile Mamlaka inawasisitiza wananchi kutosikiliza taarifa zisizo rasmi ambazo zinazopelekea taharuki, matarajio ya ZURA ni kuwa hali ya upatikanaji wa Mafuta Zanzibar itaendelea kuwa nzuri ZURA pia inawashukuru wananchi kwa kuwa wastahamilivu na kuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kuimarisha huduma ya nishati.MwishoImetolewa na Idara ya Habari maelezo.
↧
Muonekano wa Uwanja wa Kimataifa wa Kisiwani Pemba Baada ya Ujenzi Wake.
Mandhari na Muonekano wa Uwanja Mpya wa Kisiwani Pemba Baada ya Kukamilika Ujenzi wake kukamilika ndivyo utakavyoonekana.Picha Kwa Hisani ya Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafiri -Pemba.
↧