NA MALIMA LUBASHA -SERENGETI
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara limewalalamikia askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa) kwa kukamata mifugo ya wananchi, kuwalipisha faini kubwa kisha kuhukumiwa kifungo jela.
Hali hiyo imesababisha uhusiano mzuri kati ya wananchi wanaopakana na Senapa kulegalega jambo linaloelezwa kuhatarisha jitihada za uhifadhi wanyamapori zinazochulikuwa kulinda rasilimali hiyo.
Hoja hiyo iliibuliwa mjini hapa juzi na Diwani wa Kata ya Mbalibali, John Ng’oina, alipowasilisha taarifa ya kata ya robo tatu ya ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Januari hadi Machi, mwaka huu katika kikao cha baraza hilo.
Ng’oina alisema askari hao wanakamata mifugo hiyo kwa madai ya kuingia hifadhini kinyume cha sheria.
Alisema walinzi wa rasilimali hiyo ni wananchi wenyewe, ndiyo maana Tanapa walianzisha Kitengo cha Ujirani Mwema mwaka 1985 lengo likiwa ni kuwataka wananchi hao kuwalinda wanyama pori, kuendeleza uhusiano kwa kuwajengea uwezo kufahamu umuhimu wa uhifadhi na kudhibiti vitendo vya ujangili huku wakichangia miradi vijijini katika sekta za elimu, afya na maji.
Pia madiwani wengine waliwalalamikia askari hao kwa kukamata mifugo na walisema ipo haja ya kukutana na uongozi wa Senapa kujadili changamoto hiyo ili kuondoa tofauti hizo.
Naye Diwani wa Kata ya Nagusi, Jackson Manyeresa, aliwalalamikia askari wanyamapori wa Grumeti Reserves kuwa wanavamia kaya na kufanya upekuzi na kuwafanya wananchi kuwa na hofu.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu, alisema ataitisha kikao kati ya madiwani na mhifadhi mkuu wa Senapa kujadiliana juu ya changamoto hiyo ili kukomesha tabia ya wananchi kuingiza mifugo yao ndani ya hifadhi kutafuta malisho huku wakijua hilo ni kosa kisheria.
Aliwataka wananchi wa vijiji vyote wanaoishi kando ya hifadhi na kufanya shughuli za ufugaji na kilimo kuacha tabia ya kuingiza mifugo yao hifadhini na alishauri endapo wataingiza ng’ombe hifadhini askari hao wanatakiwa kuwaonya na si kuwakamata kama ilivyo sasa na endapo watarudia ndipo wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
↧
Askari Senapa lawamani Serengeti
↧
Askofu mkuu mteule Nyaisonga asimikwa
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amemsimika Askofu Mkuu Mteule, Gervas Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya.
↧
↧
Pengo awataka waumini watafakari juu cha vyeo vyao
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema waumini wa Mbeya wanapaswa kutafakari nini maana ya cheo walichokipata ndani ya kanisa na majukumu yao yanayotokana na jambo hilo.
↧
JKT JKT Queens yatetea ubingwa wa Ligi Kuu Wanawake kwa rekodi kibao
Pointi 51 ilizokusanya JKT Queens katika mechi zao 17 na kuwapa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo, ni pungufu ya moja tu dhidi ya pointi zote za timu tano zilizopo eneo la chini za Tanzanite SC(13), Baobao Queens(13), Evergreen(9), Marsh Queens (11) na Mapinduzi Queens(6) ambazo zikikusanywa zote zinafikia pointi 52.
↧
Mamilioni yatuliza mzuka wote Yanga, watinga kambini
Wachezaji wa Yanga walikuwa kwenye mgomo wa kutofanya mazoezi kwa siku mbili wakidai posho na malipo mbalimbali
↧
↧
Hawaachi kitu eti! Walahi Mo Salah, Mane watamtoa mtu damu!
Katika ile orodha ya mabao, Mo Salah ameweka kwenye kamba mara 21, akifuatiwa na Mane aliyefunga mara 20, huku pacha wao mwingine, Firmino amefunga mabao 12.
↧
Ujerumani yasitisha maombi ya wakimbizi wa Syria
SERIKALI ya Ujerumani imetangaza kusimamisha mchakato wa kuyashughulikia maombi ya wakimbizi wa Syria wanaotafuta hifadhi. Hatua hiyo imechukuliwa hadi pale tathmini mpya itakapotolewa kuhusu hali ya usalama ya Syria.
Kwa mujibu wa kundi la vyombo vya habari vya nchini Ujerumani, Funke katika ripoti yake, limeinukuu taarifa ya wizara ya usalama wa ndani ikisema maamuzi hayo yamefikiwa hadi mwongozo mpya wa wizara hiyo utakapotolewa hivi karibuni.
Waandishi wa habari wa Funke wamesema kuna hofu kwamba Serikali ya Kansela Angela Merkel itayakataa maombi zaidi ya wakimbizi kutoka Syria iwapo itabainika hakuna machafuko nchini humo.
Kulingana na takwimu za serikali, Wasyria 17,411 walipewa hifadhi mwaka 2018. Baada ya uamuzi wa Merkel wa mwaka 2015 wa kuweka mipaka wazi kwa watu waliokuwa wanakimbia vita, kumekuwa na ongezeko la zaidi ya wakimbizi milioni moja wanaotafuta hifadhi, hasa kutoka Syria, Iraq na Afghanistan.
↧
Wanaharakati waandamana kulaani ukatili wa Saudia
LONDON, UINGEREZA
WANAHARAKATI na watetezi wa haki za binadamu wamefanya maandamano nje ya Ubalozi wa Saudi Arabia katika mji mkuu wa Uingereza, London, kulaani ukatili wa hivi karibuni wa watawala wa Saudi Arabia, baada ya kuwanyonga watu 37 ambao ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Mamia ya wanaharakati hao, wakiwamo wapinzani na wakosoaji wa utawala wa Saudia walifanya maandamano hayo jana nje ya ubalozi wa Saudia mjini London, wakitaka serikali ya Uingereza na nchi nyingine za Ulaya zivunje kimya chao kutokana na makosa ya jinai yanayofanywa na Saudi Arabia dhidi ya haki za binadamu.
Waandamanaji hao wamesema ukatili wa Saudia umevuka mipaka na kukanyaga sheria zote za kimataifa, na kwamba kitendo hicho cha kuwanyonga raia 37, wakiwamo watoto wadogo, mlemavu na wanazuoni, na kisha kuusulubisha mwili wa mmoja wa Waislamu hao hadharani hakikubaliki.
Duru za kisheria na haki za binadamu zinasema kuwa hii ni mara ya pili ndani ya wiki moja kwa watetezi hao wa haki za binadamu na wakosoaji wa utawala wa Saudi Arabia kuandamana mjini London.
Mashirika na taasisi za kimataifa pamoja na wanaharakati wa masuala ya kijamii wanaendelea kulaani jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Aal Saud wa Saudi Arabia ya kuwaua kwa umati raia 37 wa nchi hiyo.
Harakati za Mapambano ya Kiislamu za Hizbullah ya Lebanon na Hamas ya Palestina, shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa asasi za kimataifa zilizolaani hatua hiyo ya watawala wa Saudia kutumia kisingizio cha kupambana na ugaidi kuwanyonga kwa umati Waislamu wa Kishia, zikisisitiza kuwa utawala huo wa kifalme hauheshimu thamani ya utu.
↧
Mikakati ya China yawatisha Marekani
BEIJING, CHINA
RAIS wa China, Xi Jinping, ametangaza kuwa ni muhimu kwa nchi zaidi duniani kujiunga katika mipango ya mikakati ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inayosimamiwa na nchi yake, lakini kwa upande wao bado Marekani imeonyesha kuhofia hatua hiyo na kusisitiza kuwa inajenga ushawishi mkubwa zaidi wa kimkakati kwa manufaa ya China.
Akizungumza katika mkutano wa kilele wa miradi ya miundombinu na ujenzi mjini Beijing, Rais Xi Jinping, alitoa wito kuwa ni wakati mwafaka kwa mataifa zaidi kujiunga na kuyaondolea wasiwasi baadhi ya watu kwamba mradi huo wa China utazinasa nchi katika madeni makubwa ambayo yatahatarisha uhuru wao.
Xi amesema kwamba mradi huo umelenga kuziendeleza nchi za Afrika na za barani Asia ambazo zimejenga bandari na njia za reli kwa mikopo kutoka China, lakini pia umelenga kutanua wigo kwa mataifa mengine ya Bara la Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini. Katika hotuba yake, Rais Xi aliahidi kuwa nchi yake inadhamiria kuleta faida kwa wote duniani bila kujali nguvu ya mataifa yatakayonufaika.
Mkutano huo wa kilele unaoendelea mjini Beijing unahudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 40, ikiwa pamoja na viongozi kutoka nchi za Afrika.
Duru za kisiasa zimesema kuwa mkutano huo umetafsiriwa kuwa ni vita ya kibiashara kati ya China na Marekani. Vita ya kibiashara baina ya Marekani na China inaathiri pia uchumi wa Ujerumani na Bara la Ulaya kwa jumla.
Kwa mujibu wa Waziri wa Uchumi wa Ujerumani, Peter Altmaier, amesema kuwa mkutano wa kilele kuhusu mradi wa China wa ujenzi wa miundombinu ya kuyaunganisha mabara, unaofanyika mjini Beijing, Waziri Altmaier amekutana na Makamu wa Waziri Mkuu wa China, Liu He, anayeiwakilisha nchi yake kwenye mazungumzo na Marekani juu ya kuutatua mgogoro huo wa kibiashara.
Aidha, Altmaier amesema kuwa mgogoro huo wa mataifa makubwa kabisa mawili unazuia kasi ya ustawi wa uchumi wa dunia, vilevile mazungumzo mengine baina ya China na Marekani yamepangwa kuendelea wiki ijayo mjini Beijing.
↧
↧
Ufaransa ‘yafukuzwa’ Libya
TRIPOLI, LIBYA
MAELFU ya wananchi nchini Libya wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Tripoli wakiwa wamevalia vizibao vya njano kama wanavyofanya washiriki wa maandamano ya vizibao vya njano kupinga siasa za kiuchumi za serikali ya Ufaransa, ambapo nao wamelaani mienendo hasi ya Serikali ya Rais Emmanuel Macron dhidi ya nchi yao.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, washiriki wa maandamano hayo wamelaani vikali operesheni za Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi linalojiita ‘Jeshi la Kitaifa la Libya’ pamoja na uungaji mkono wa kijeshi wa Ufaransa dhidi ya nchi yao.
“Sisi wazawa wa Tripoli kama walivyo wakazi wa miji mingine ya Libya, tumekuja hapa kuonyesha upinzani wetu kwa utawala wa mtutu wa bunduki wa Haftar na mashambulizi yake,” amesema mmoja wa waandamanaji.
Siku chache zilizopita, Shirika la Habari la Al Jazeera liliripoti kwamba, meli ndogo ya kivita mali ya Ufaransa ilituma silaha na zana za kijeshi kwa wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, boti ndogo za mwendo kasi zilitumika kupakua shehena ya silaha kutoka kwenye meli hiyo ya kivita ya Ufaransa.
Aidha wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Tunisia, Abdelkrim Zbidi alinukuliwa akisema kuwa maofisa wa usalama wa nchi hiyo waliwatia mbaroni watu 13 wakiwa na pasi za kusafiria za Ufaransa kwenye kivuko cha Ra’s Ajdir katika mpaka wa Libya.
Wiki iliyopita, Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya ilitangaza kukata ushirikiano wake wa kiusalama na serikali ya Ufaransa kutokana na hatua ya nchi hiyo kuliunga mkono kundi la wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar.
Wapiganaji wa kundi hilo walianzisha mashambulizi makali Aprili 4 mwaka huu, dhidi ya mji wa Tripoli sambamba na kushambulia makao makuu ya Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa mjini humo. Hujuma hizo hadi sasa zimepelekea karibu watu 270 kuuawa na wengine 1300 kujeruhiwa, sambamba na watu 35,000 kuwa wakimbizi.
↧
Kardinali Pengo: Msiwe waoga kutekeleza majukumu yenu
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka wananchi wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya wasiogope kutekeleza majukumu yao.
↧
Pengo asema ipo haja kwa kanisa kushirikiana na Serikali
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema ili Roho Mtakatifu asibezwe na kusahaulika kuwa ni Mungu wa pili linahitajika kanisa linaloshirikiana na Serikali katika kuweka mazingira yanayotakiwa.
↧
JKT Queens yatetea ubingwa wa Ligi Kuu Wanawake kwa rekodi kibao
Pointi 51 ilizokusanya JKT Queens katika mechi zao 17 na kuwapa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo, ni pungufu ya moja tu dhidi ya pointi zote za timu tano zilizopo eneo la chini za Tanzanite SC(13), Baobao Queens(13), Evergreen(9), Marsh Queens (11) na Mapinduzi Queens(6) ambazo zikikusanywa zote zinafikia pointi 52.
↧
↧
Putin kumzidi maarifa Trump?
NA MARKUS MPANGALA
WIKI hii kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na Rais wa Urusi, Vladimir Putin wamekutana mjini Vladivostok, Mashariki mwa Nchi ya Urusi. Mkutano huo ni wa kwanza kati ya viongozi hao wawili, wamejadiliana umuhimu wa kuimarisha uhusiano wao kisiasa na kidiplomasia kwa malengo ya kupata suluhisho la suala la silaha za nyukilia kwenye rasi ya Korea.
Aidha, viongozi hao wamejadili kudhoofika kwa uhusiano wa biashara kati ya nchi zao kwa asilimia 56 mwaka 2018 kutokana na vikwazo vilivyowekewa na Serikali ya Korea Kaskazini.
Nchi zote mbili yaani Urusi na Korea Kaskazini zinakabiliwa na vikwazo kutoka sehemu zinazofanana. Kwa msingi huo Urusi na Korea Kaskazini hazina chaguo jingine zaidi ya kuimarisha ushirikiano, huku zikitegemea zaidi mshikamano wao na Nchi ya China ambayo imekuwa ikihusiana nazo vizuri kidiplomasia, kiuchumi, ulinzi na usalama.
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov ameviambia vyombo vya habari kuwa mkutano baina ya viongozi hao umepangwa kwa minajili ya kubadilisha hali ya hewa ya uhusiano wao, huku mataifa yote yakikabiliwa na vikwazo. Korea Kaskazini imewekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa, mataifa ya Ulaya na Marekani. Wakati Urusi imewekewa vikwazo na Marekani pamoja na mataifa ya Ulaya.
Korea Kaskazini inawahitaji washirika wapya na wa zamani ili kuendeleza mshikamano katika kipindi ambacho imewekewa vikwazo. Urusi nayo inahitaji washirika ambao itakuwa nao bega kwa bega katika kujenga uchumi wa nchi yake pamoja na kuongeza ushawishi miongoni mwa mataifa.
Urusi imependekeza kuwa Korea Kaskazini na Marekani zinapaswa kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kuhakikisha suala lenye mgogoro mkubwa duniani yaani silaha za nyukilia linapatiwa ufumbuzi.
Korea Kaskazini nayo imekuwa ikitoa masharti yake ili kuhakikisha inatii masharti yanayotolewa na mataifa ya ulaya, Marekani na Umoja wa Mataifa kama njia ya kukomesha majaribio ya silaha za nyukilia.
Sharti la Marekani na ambalo limechangia vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ni kwamba lazima Serikali ya Kim Jong Un iachane kabisa na mpango wa kutengeneza silaha za Nyukilia.
Sharti hili limekuwa gumu kwa Korea Kaskazini kwani inahitaji kufanya biashara na mataifa ya kigeni pamoja na kuhakikisha vikwazo dhidi yake vinaondolewa.
Tangu Rais Donald Trump achukue madaraka nchini Marekani alianza kuwa na mvutano mkubwa na kurushiana maneno huku Kim Jong Un naye akiendeleza majaribio ya silaha za nyukilia na kukiuka ilani ya kimataifa. Hatua hiyo ilikuwa tishio kwa jirani zake Japan na Korea Kusini.
Trump aliapa kupambana ikiwa Kim Jong Un iwapo nchi yake itaendelea kutishia kuirushia makombora ya masafa marefu Marekani, wote wakipeana majina ya kukebehi.
Korea Kaskazini ilikaidi na kufanya jaribio la nyukilia la sita mwezi Septemba mwaka 2017. Baadaye Kim alitangaza kuwa nchi yake imefanikiwa mpango wake wa kua taifa la nyukilia, ikiwa na silaha zinazoweza kuifikia ardhi ya Marekani.
Kim Jong Un na Trump wamekutana mara mbili katika mikutano yenye nia ya kuondokana na msuguano pamoja na vikwazo vilivyopo baina ya mataifa hayo. Mkutano wa kwanza ulifanyika nchini Singapore Juni mwaka jana, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Marekani viongozi hao wawili walikutana kwanza kwa dakika 41 na walikuwa wawili na wakalimani wao wakati wakijadiliana juu ya makubaliano waliyopaswa kufanyika kwa masilahi ya nchi zote mbili.
Mkutano wa mjini Hanoi nchini Vietnam, hakukuwa na makubaliano yoyote kwani kila upande ulishikilia msimamo wake. Korea Kaskazini iliambiwa iache matumizi na urutubishaji wa silaha za nyukilia kama sharti la kufikia mwafaka wa mgogoro baina yake na mataifa makubwa.
Kwa upande wake Kim Jong Un alisisitiza kuwa ili atekeleze masharti aliyopewa ni muhimu kwa Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo vyote dhidi ya Korea Kaskazini ambavyo vinahusiana na mipango ya kutengeneza silaha eneo la Yongbyon.
Hoja ya pili iliyosababisha Marekani ione kikao hicho hakikuwa na manufaa hivyo kuondoka mezani ni msimamo wa Korea kaskazini kuwa ipo tayari kuondoa vinu vya Yongbyon pekee na si vinu vyote vya nyukilia vya Korea Kaskazini. Marekani imekataa matakwa ya Korea Kaskazini ya kutaka kuondolewa kwa vikwazo vyote.
Mwaka 2011 Urusi ilishirikishwa katika mazungumza ya mpango wa nyukilia wa Korea Kaskazini. Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Kim Jong-il, alikutana na rais wa Urusi wa wakati huo Dmitry Medvedev.
Korea Kaskazini imekuwa ikiendelea na shughuli zake za nyukilia. Mapema Aprili mwaka huu taifa hilo lilidai kuwa limefanyia majaribio silaha yake mpya, ambayo duru za kisiasa inadhani ni kombora la masafa mafupi.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov, mazungumzo ya mgogoro katika rasi ya Korea yalianza rasmi mwaka 2002, ambapo yalihusisha Korea kaskazini, Korea kusini, China, Japan, Urusi na Marekani.
“Hakuna mpangilio rasmi wa mazungumzo hadi kipindi hiki. Lakini kwa upande mwingine, hatua zilizofikiwa zimefanywa na nchi nyingine. Manufaa yaliyopo ni kuungwa mkono kutatua mgogoro, lengo likiwa ni kusitisha michakato yote ya utengenezaji wa silaha za nyukilia, na kuhakikisha msuguano baina ya nchi mbili za Korea unamalizika,” alisema Peskov alipozungumza na vyombo vya habari.
Mkutano wa Kim Jong Un na Vladimir Putin umetafsiriwa kuwa ni fursa kwa Korea Kaskazini kuonyesha nguvu zake pamoja na kuwa na nchi zinazounga mkono juhudi zake kwenye mazungumzo yake ya Marekani.
Korea Kaskazini imemlaumu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, kutokana na kuvunjika mazungumzo ya Februari mwaka huu mjini Hanoi. Pia imependekeza waziri huyo aondolewe kwenye kamati ya majadiliano kuhusu nyukilia kwa madai anaongeza mambo mengi ya kipuuzi. Vilevile imependekeza kuteuliwa mtu makini na mwangalifu kwenye mazungumzo yao.
Mkutano huo pia ni fursa kwa Korea Kaskazini katika kutengeneza mwelekeo wa uchumi wake bila kutegemea Marekani. Kim Jong Un ameripotiwa kumwambia Putin juu ya umuhimu wa kuondolewa vikwazo dhidi ya nchi yake.
Wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia wanasema mkutano huo pia ni fursa kwa Urusi kuonyesha umuhimu na ushawishi wake katika utatuzi wa mgogoro wa rasi ya Korea. Urusi kama zilivyo Marekani na China hazina furaha kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya Korea kusini na Korea kaskazini.
Katika kipindi cha vita baridi, Muungano wa Sovieti (Urusi ya sasa) ilikuwa rafiki mkubwa wa Korea Kaskazini ambapo ilitoa misaada ya kijeshi pamoja na kushirikiana kibiashara. Korea Kaskazini inafuata itikadi ya kikomunisti kama ilivyokuwa Urusi, wakati Korea Kusini inafuata itikadi ya kibepari inayopo Marekani na washirika wake. Kufuata itikadi zinazofanana kulitengeneza urafiki mkubwa baina ya mataifa hayo.
Baada ya kuvunjika muungano wa Sovieti mwaka 1991, biashara kati ya mataifa hayo ilidorora ambapo Korea Kaskazini iliamua kuelekeza nguvu zake katika uhusiano wake na China, ambayo ni rafiki mwaminifu hadi sasa.
Chini ya uongozi wa Rais Putin, Urusi ilijikwamua kiuchumi na mwaka 2014 alifuta madeni yote ya nchi yake kwa Korea Kaskazini ikiwa ni ishara ya kuanza upya uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo.
Duru za kisiasa zinasema, je ni kwa kiasi gani Urusi itafanikiwa kuwashawishi Korea Kaskazini ambayo wamefanya mkutano mmoja, kuliko Marekani iliyofanya mikutano miwili bila kupatikana mwafaka?
Makala haya yameandaliwa kwa msaada wa mashirika mbalimbali ya habari.
↧
Muungano utukumbushe fikra za waasisi wetu
Na LEONARD MANG’OHA
WIKI hii nchi yetu imesherehekea miaka 55 ya kuzaliwa kwake tangu Chama cha Tanganyika African Union (Tanu), kilichokuwa kikitawala Tanganyika na Afro Shiraz Party kilichokuwa kikiongoza Zanzibar kuungana na kuwa nchi moja.
Miaka 55 inatimia wakati kukiwa na ombwe kubwa la kisiasa nchini kutokana na vilio kuhusu kubanwa kwa demokrasia, kunakofanywa na Serikali dhidi ya vyama vya upinzani.
Vilio vingi vinahusu kukosa uhuru wa kukusanyika, kuandamana na kufanya mikutano ya hadhara ambayo imepigwa marufuku na ile ya ndani ambayo pia mara nyingi imekuwa ikivurugwa.
Kutokana na hali hiyo hakuna tena kujiamini miongoni mwa vyama hivyo kutokana na vitisho na kufikishwa mahakamani kwa viongozi wake. Mathalani wakati huu viongozi wengi waandamizi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaburutwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kinyume cha utaratibu.
Wadau mbalimbali wanaelezea hali hiyo kama njia ya kuvikandamiza vyama vya upinzani kwa makusudi.
Tunapoadhimisha miaka 55 ni vema tukarejea nyuma na kutazama mawazo na fikra za waasisi wa muungano huu Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.
Tukirejea maandiko ya Baba wa Taifa katika kitabu chake cha ‘Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania’, anaonyesha nia yake ya kutaka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Tamaa hiyo ya Mwalimu Nyerere inatokana na kile alichokiita ubovu wa uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndiyo uliofanya apendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
“Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.
“Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani, wala dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasiwasi!
“Wazalendo Watanzania hawana budi wapende kuona demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Hii ina sura mbili, Kwanza, ni lazima kurudisha tena uhuru na utaratibu wa kujadili masuala yote makubwa na kufikia uamuzi baada ya mjadala” inaeleza sehemu ya maandiko hayo.
Maneno ya Mwalimu katika kitabu hiki yanaonyesha ni kwa jinsi gani kama kiongozi wa chama na Taifa hakuwa na mawazo mgando ya kukumbatia chama chake tu hata pale alipoona kinaboronga, alifahamu wazi ili kuijenga CCM imara ni lazima kuwa na chama kingine chenye kutoa upinzani wa kweli kwa chama chake.
Zaidi ya miaka 25 sasa tangu Mwalimu alipoeleza hayo, lakini ni ukweli usiopingwa kuwa bado hakuna chama imara cha kukiondoa CCM madarakani. Nasema hivi kwa kuangalia hali ilivyo katika vyama vingi vya siasa vya upinzani nchini. Vyama vingi havina nguvu ya kisiasa kama ile ya CCM, kwa sababu havina mtaji mkubwa wa wanachama na hata nguvu ya kifedha ya kuweza kujiimarisha.
Vile vilivyojaribu kujitanua misuli yake vimejikuta katika migogoro ya ndani na kujikuta vinamaliza muda mwingi kupigania fito ndani ya vyama badala ya kuvijenga vyama vyao viweze kutoa upinzani wa kweli kwa CCM, huku baadhi ya vyama kama vile Chadema vimekumbwa na mkwamo wa kisiasa ambapo viongozi wake mara kwa mara wamejikuta matatani wanapofanya shughuli za kisiasa.
Mwalimu hakuwa mwoga wa changamoto bali alizitumia kama kipimo cha uongozi bora na alichukia uongozi wa kutumia vitisho bali wenye kutumia hoja zaidi katika kufanya maamuzi.
“Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kutoa maamuzi muhimu. Kwa sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja; vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha ya kutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala. Viongozi hawa wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; na hawatakuwa na haja ya kutumia akili.
“Kichini chini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho. Na kama tukiacha utamaduni wa woga ukazagaa tutakuwa tunakaribisha udikteta. Uhuru hauji wala haudumishwi ila kwa kuwa tayari kulipa gharama zake; na vitu vyote vyenye thamani kubwa gharama yake ni kubwa,”
Mwalimu alipendelea CCM iendelee kujenga utaratibu na utamaduni wa kuchambua masuaIa makubwa katika mijadala, na kufikia uamuzi baada ya uchambuzi na mijadala ya kidemokrasia na ya wazi wazi. Na wanachama wake kwa vitendo vyao lazima wapige vita utamaduni wa woga na fidhuli ya viongozi.
Kwa mtazamo wake kwa wakati huo Mwalimu aliamini kwamba demokrasia peke yake ambayo ingeendelea kuwa na maana kwa nchi hii wakati wanasubiri kupata mpinzani mzuri na makini nje ya CCM, ni demokrasia ndani ya CCM. Hapa aliwasihi wanachama wa CCM kukitazama upya chama chao na kuona jinsi ya kuongeza demokrasia ndani yake kwa manufaa ya Tanzania nzima.
Ni wazi kuwa CCM kama chama mama katika siasa za Taifa hili ambalo sasa linafikisha umri wa mtumishi wa umma aliye katika umri wa kustaafu, kinawajibika kuimarisha demokrasia nchini. Kinao wajibu wa kuvionesha njia vyama vingeni nini wanapaswa kufanya ili kufikia mafanikio ya kisiasa yenye kulenga maendeo kwa Taifa na si kuendelea kukaa madarakani bila kuwa na tija.
Naamini bado CCM haijakamilisha kazi hii ya kukuza demokrasia ya vyama vingi kwa sababu ni ukweli usiopingwa kuwa vyama vingi bado ni dhaifu kupambana na CCM. Kwa hiyo tunapoadhimisha miaka 55 ya muungano tuyakumbuke maono ya waasisi wake.
↧
Mazito yamkabili mchekeshaji aliyeukwaa Urais Ukraine
HASSAN DAUDI NA MITANDAO
AWALI, alifahamika kwa kipaji chake cha uchekeshaji lakini sasa rasmi Volodymyr Zelensky ndiye Rais wa Ukraine, akimwacha mbali mpinzani wake, Petro Poroshenko, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, Zelensky alizoa asilimia 73 ya kura zilizopigwa.
Si tu ushindi, pia Zelensky ameandika historia ya kuwa Rais wa kwanza kuingia Ikulu akiwa na tofauti kubwa ya kura dhidi ya mpinzani wake tangu nchi hiyo ilipopata uhuru miaka 30 iliyopita.
Pia, kasi yake kueleka katika ushindi huo imekuwa gumzo kwani baada ya kutangaza nia mapema mwaka huu, ilimchukua miezi miwili tu kushinda kwa asilimia 30 raundi ya kwanza ya uchaguzi huo, na kisha wiki tatu kutangazwa mshindi dhidi ya Petro Poroshenko aliyetaka kurejea madarakani.
Akiwa hana uzoefu wa masuala ya kisiasa, umaarufu wa ‘bwana mdogo’ huyo mwenye umri wa miaka 41 umetokana na uchekeshaji wake katika igizo lake la televisheni la ‘Servant of the People’ (Mtumishi wa Watu), ambalo lina wapenzi wengi katika Taifa hilo lenye watu milioni 45.
Kwa faida ya wengi, katika tamthilia hiyo, Zelensky ameigiza nafasi ya mwalimu aliyegombea na kushinda urais kwa lengo la kuwakaba koo viongozi ‘wapigaji’. Hivyo, igizo lake hilo limeakisi safari yake halisi ya Ikulu.
Huku akitumia mitandao ya kijamii kuwafikia wapiga kura wake, wengi wao wakiwa ni vijana, wapo waliolichukulia hilo kuwa ni udhaifu mkubwa wa Zelensky katika kuzungumza hoja za msingi.
Mmoja kati ya hao ni Profesa wa siasa katika Chuo Kikuu cha Kyiv-Mohyla Academy, Oleksiy Haran, alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha Al Jazeera, amesema “Watu walivutiwa na rais wa uongo waliomtazama kwenye ‘muvi’ yake, wakiamini ni ukweli. Ni suala la kisaikolojia. Zelensky anapozungumza, huwa ana makosa mengi. Ndiyo maana upande wa timu yake ulikuwa ukiepuka mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Zelensky na waandishi wa habari au wataalamu.”
Ni kweli hiyo ya kukosa uzoefu inaweza kuwa hoja yenye mantiki lakini haitakuwa mara ya kwanza kwa wananchi wa Taifa hilo kumchagua mgombea nje ya ulingo wa siasa, mfano mzuri ukiwa ni pale bingwa wa zamani wa uzito wa juu, Vitali Klitschko, aliposhinda kuwa Meya wa Kyiv mwaka 2014.
Madai yaliyopingwa vikali na Zelensky aliyesema kukwepa midahalo na mahojiano ilikuwa moja kati ya mbinu zake za kushinda uchaguzi na tayari ameshapokea pongezi nyingi kutoka kwa mataifa mbalimbali, yakiwamo Marekani na Ufaransa.
Je, ni changamoto zipi zinazomkabili Zelensky kueleka safari yake ya miaka mitano Ikulu ya Ukraine? Kwa maana nyingi, yapi matarajio ya wachambuzi wa siasa na wananchi wa taifa hilo kwake?
Kibarua cha wazi kinachoweza kuonekana ni kuwathibitisha wakosoaji wake kuwa si kibaraka wa mfanyabiashara anayeshika nafasi ya tatu kwa utajiri nchini humo, Ihor Kolomoyskyi.
Kutokana na tuhuma za rushwa, akaunti za benki za Poroshenko zilitaifishwa mwaka 2016 zikiwa na zaidi ya Dola za Marekani bilioni 5.5 na ndipo alipokimbilia Israel.
Kwa kuwa hata tamthilia yake ya ‘Servant of the People’ ilikuwa ikirushwa na kituo cha televisheni kinachomilikiwa na bilionea huyo, basi kuna shaka kuwa Zelensky ni mtu wa karibu wa Kolomoyskyi.
Rais aliyemaliza muda wake, Poroshenko, ni mmoja kati ya wanaoamini hivyo, kwamba ushindi wa Zelensky ni kicheko ambaye hana uhusiano mzuri na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Kama hiyo haitoshi, inaaminika kuwa hata walinzi wa Zelensky ni wale waliokuwa wakifanya kazi na Kolomoisky, ikielezwa pia alimtumia hata mshahuri wa zamani wa tajiri huyo wakati wa kampeni.
Hayo yanatajwa huku yakiwapo madai mengine kwamba magari mawili ya kifahari aliyokuwa akitumia Zelensky yanamilikiwa na watu wa karibu wa Kolomoisky, ingawa wawili hao wamekataa, wakisema uhusiano wao ni wa kibiashara tu na hauathiri maisha yao ya kisiasa.
Licha ya Zelenskiy kukanusha kuwa kibaraka, wanaomtaja wanatilia shaka uwezekano wa wafanyabiashara wakubwa kurejesha nguvu yao katika uendeshaji wa Serikali kwa masilahi yao.
Mbali ya hilo, Zelenskiy akabaliwa na mtihani mzito wa kuyamaliza machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Ukraine, ambayo yanachangiwa na vikundi vinavyoungwa mkono na Urusi, ikielezwa kuwa yameshagharimu maisha ya watu 13,000.
Tangu Urusi ilipolikalia eneo la Crimea mwaka 2014, Jeshi la Ukraine limekuwa likipambana kurejesha amani bila mafanikio. Hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya Serikali ya Moscow kuzishikilia meli tatu za kijeshi za Ukraine.
Tatizo ni kwamba mamlaka za Urusi hazijawahi kuamini kuwa Ukraine ni sehemu ya taifa lao na si nchi inayojitegemea, kama alivyowahi kusema Rais wa Urusi, Vladmir Putin, kuwa mataifa hayo ni kitu kimoja.
Ieleweke kuwa machoni mwa viongozi wa Urusi, Ukraine imekuwa ikitumiwa na mataifa ya Kibepari, ikiwamo Marekani. Utafiti uliowahi kufanywa na Kituo cha tafiti za kisaikolojia cha Levada, uliwahi kubaini kuwa asilimia 56 ya Warusi wanawachukia wenzao wa Ukraine.
Je, baada ya Poroshenko kuchemsha kwa kipindi chote cha uongozi wake, Zelensky ataweza? Katika hilo, mchambuzi wa siasa nchini Ukraine, Mykola Davydyuk, anasema: “Huenda Zelensky akatafuta mbinu za kidiplomasia na si kutumia jeshi.”
Kuonyesha ni kwa kiasi gani inaweza kuwa ngumu kwa Zelensky katika hilo la kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo, tayari Urusi wameshatangaza kuwa watasitisha kupeleka mafuta na makaa ya mawe nchini Ukraine kuanzia Juni mosi, mwaka huu.
Urusi wanatangaza hatua hiyo huku Ukraine ikiwa wateja wakubwa wa makaa ya mawe kutoka kwa jirani zao hao, ikiagiza asilimia 23 ya bidhaa hiyo. Kando ya hilo, wakati uchaguzi uliomweka madarakani Zelensky ukiendelea, Jeshi la Ukraine lilitangaza kuwa vikundi vinavyoungwa mkono na Urusi vinaendeleza machafuko.
Ahadi ya Zelensky juu ya mgogoro huo ni kauli yake ya kusema huu ni wakati mwafaka kwa serikali yake itakayoanza kazi Juni 3, mwaka huu kuipeleka Ukraine katika karne ya 21.
Ziara yake nchini Ufaransa alikokwenda kukutana na Rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron, hata kabla ya kuingia madarakani, imewapa matumanini ‘watu’ wake, ikiwaamisha kuwa huenda ukawa mwanzo wa uhusiano mzuri na mataifa mengine kama Urusi.
Wakati huo huo, Zelensky anaingia Ikulu akitambua kuwa ana mzigo mzito wa kumaliza kero za kiuchumi ambazo ameachiwa na serikali zilizopita, ikiwamo aliyoing’oa madarakani ikiwa imekaa muhula mmoja.
Hadi leo hii, Ukraine imeendelea kuteswa na deni la mwaka 2014, walipokopa Dola za Marekani bilioni 17.5 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Mbaya zaidi kwa Zelensky, Mtafiti wa Fedha mjini Kiev, Oleksandr Parashchiy, anasema:
“Miaka mitatu ijayo, Serikali ya Ukraine itakuwa na deni la Dola bilioni 20 na haifahamiki fedha hizo zitapatikana wapi. Anatakiwa kulifanyia kazi suala hilo.”
Naye mtaalamu wa deplomasia anayeishi Kiev, Andreas Umland, anasisitiza kuwa licha ya miaka 30 ya chaguzi, ikipitia mikononi mwa viongozi wenye utaalamu wa siasa na uchumi, bado Ukraine imeendelea kuwa nchi masikini zaidi barani Ulaya.
Hali mbaya kiuchumi inaungwa mkono na mchambuzi wa siasa za Ukraine, Melinda Haring, anayesema: “Wanachokitaka wananchi wa Ukraine ni maisha ya kawaida tu lakini nchi inakuwa masikini wakati (Rais) Poroshenko amejitajirisha. Ni wazi watu walitaka mtu asiye na makandokando na uhusiano na wanasiasa.”
Zaidi ya hayo, mtihani mwingine alionao Rais huyo ni namna atakavyoweza kupata uungwaji mkono wa Bunge, ikiwa sehemu kubwa ya viti inakaliwa na wapambe wa rais aliyetangulia, Poroshenko.
“Haitakuwa rahisi kupata sapoti ya Bunge. Ni wazi atakuwa na Bunge lenye chuki (dhidi yake),” anasema mchambuzi wa siasa mwenye makazi yake mjini Kiev, Anatoliy Oktysuk.
↧
NINI KINASABABISHA WAZAZI WA KIUME KUPOTEZA UPENDO, KUKATALIWA NA WATOTO KADIRI WANAVYOZEEKA?
Utangulizi.
LABDA wewe unaweza kuwa shahidi wa familia nyingi au hata familia unapotoka kwamba watoto wengi hupoteza ukaribu na baba zao na kuongeza ukaribu na mama zao hususani pale wazazi hawa wanapokuwa na umri mkubwa au kuanza kuzeeka.
Utakuta mara nyingi watoto wanawasiliana sana na mama, watapiga simu kwake na kutuma meseji mara kwa mara, mama ndiye atajua nini kinaendelea kwenye maisha ya watoto hata kama wako mbali na baba anabaki kupewa taarifa na mama.
Hata inapofika nyakati za watoto kuwasaidia wazazi basi mama husaidiwa zaidi kwa uwazi au hata kisirisiri wakati baba anaweza kutelekezwa au hata akisaidiwa basi ni kidogo. Je unadhani sababu kubwa ni nini? Tatizo hili mizizi yake ni ipi? Nimetamani tuliangalie kwa pamoja maana linatuhusu wote na labda wazazi wanaweza kujitambua na kubadilisha namna ya maisha ili kupunguza au kuliondoa kabisa.
Sababu:
Kwa kiasi kikubwa katika familia zetu za kiafrika hususani katika miaka 25 ya kwanza ya maisha ya watoto, wengi huwa mikononi mwa wazazi na labda baba ndio huwa mwenye nguvu kubwa katika familia, baba ndio mfalme wa familia, ndio atasema nini kifanywe na nini kisifanywe, ndio atasimamia muda wa kurudi nyumbani na hata kuadhibu kila lisilosawa kwa watoto.
Maamuzi ya mwisho huwa ni ya baba ambaye ndiye kiongozi wa familia na hali hizi huwafanya watoto kujenga hofu kubwa kwa baba yao badala ya kujenga upendo kwake. Sio tu kwenye ukali na kuadhibu lakini katika kipindi hiki baba ndiye anayelisha familia, yeye ndiye wakuhakikisha kila mtu amekula, ameshiba, amevaa nguo na analala salama.
Hii inamuongezea nguvu sio tu za kiuchumi bali hata za kihisia dhidi ya wale anaowatawala (watoto na mke) pale nyumbani, maana ukikiuka amri na sheria za nyumbani madhara yake yanaweza kuwa makubwa, unaweza kukosa chakula, au usilipiwe ada au hata kufukuzwa nyumbani. Kwahiyo utake au usitake ni lazima kuzingatia kila sheria hata kama hauzipendi.
Sio tu hofu kwa baba bali hata chuki inaweza kuota katika kipindi hiki. Baada ya kipindi hiki, watoto wanapoanza kupata kazi wakiwa bado nyumbani mama sasa huanza kupata nguvu na baadae wakianza kutawanyika na kuishi maisha yao wenyewe ndipo nguvu na mamlaka huamia mikononi mwa watoto wenyewe, sasa wanajipangia kila kitu kuhusu maisha yao, wafanye nini, waende wapi, wahusiane na nani, walale wapi n.k. Sio baba tena wala mama anayeweza kuwazuia au kuwapangia.
Watoto wanapoanza kupata fedha baada ya kuanza kazi au biashara zao binafsi, wanaanza kumjali zaidi mama kuliko baba. Wanaendeleza na kuuongeza ukaribu zaidi na mama zaidi ya baba. Bahati mbaya sana wakati baba akiwa ndio mfalme na mwenye mamlaka ya nyumba, wakati anahakikisha wote wanakula na kuishi vema alikuwa bize na kazi, alimezwa na majukumu na kusahau kuwa na muda na watoto wake.
Alikuwa amekamatwa na ajira yake kuhakikisha anapanda cheo na kupata mshahara mzuri ili watoto wasome vizuri na waishi vizuri, au alikuwa ameshikwa na biashara zake kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa ili familia isiyumbe kiiuchumi na watoto wasome. Muda wakuwa rafiki na watoto wake haukuwepo kabisa na kwahiyo kukaanza kutengenezwa mpasuko wa ukaribu wa kihisia baina ya baba na watoto wake na kwa upande mwingine wakajenga na kuongeza ukaribu wa kirafiki na kihisia na mama yao ambaye mara nyingine walimwona kama muathirika mwenzao wa ukali wa baba, maana labda watoto mara nyingine walimwona baba akiwa mkali au hata kumpiga mama mbele yao.
Hapa watoto wanajiona kama wao pamoja na mama walishiriki maumivu ya uongozi wa mabavu wa baba, na hali hiyo inawafanya kuongeza ukaribu wa kihisia zaidi, sio tu wanampenda mama bali wanasimama upande wake kumlinda na kumtetea pia dhidi ya baba na hata uhitaji na hatari nyinginezo.
↧
↧
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 28.04.2019: Pogba, De Gea, Van Dijk, Maguire, Bale, Hazard
Paul Pogba ameidokezea Manchester United mpango wake wa kujiunga na Real Madrid
↧
Simba yaipora Yanga taji kama utani vile
Kama Simba itapata ushindi kwenye mechi zake tano za viporo itavuna alama 15 ambazo zitaifanya kufikisha pointi 84 wakati Yanga itabaki na alama zake 74 huku zote zikiwa na mechi 32 na kubakiwa na tano za kumaliza msimu.
↧
London Marathon 2019: Kenya's Eliud Kipchoge wins as Mo Farah fifth
Kenya's Eliud Kipchoge runs the second fastest marathon in history to win the London Marathon as Britain's Mo Farah finishes fifth.
↧