Quantcast
Channel: Magazeti ya Tanzania - Tanzania Newspapers | Magazetini
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live

Mastaa hawa kuzibeba timu michuano ya Caf

$
0
0
KIPUTE cha michuano ya kimataifa kinatarajia kuanza mwishoni mwa wiki hii kwa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa wawakilishi wetu wanne kuanza kutupa karata zao uwanjani huku Yanga pekee ikianzia nyumbani.

Mechi hizi sio za kukosa FDL

$
0
0
Ni moto! Msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) unatarajiwa kuanza kurindima Septemba 14, ambapo timu 24 zilizopangwa katika makundi mawili zitakinukisha katika michuano hiyo kuwania nafasi ya kupanda Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020-2021.

Ukuta wa chuma Man United

$
0
0
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amewapongeza mahasimu wao wa mji mmoja, Manchester United kwa kufanikisha dili la usajili wa Harry Maguire, huku akisema klabu yake “ilishindwa kumudu bei” ya beki huyo wa Leicester City.

Madaktari wa Cuba waliotekwa Kenya na al-Shabab walazimishwa kusilimu

$
0
0
Vyanzo vya kiintelijensia nchini Kenya vinaashiria madaktari wawili wa Cuba waliotekwa nchini Kenya wamesilimishwa kwa lazima.

Uhuru amweka Ruto kiporo urais 2022

$
0
0
ISIJI DOMINIC SIASA za kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2022 zinazidi kumchefua Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye amekuwa akisisitiza wanasiasa kuwatumikia wananchi na kuacha kupiga siasa hadi muda wa kampeni utakapofika. Hata hivyo, ushauri huu wa Rais Uhuru ni kama unapuuzwa na wanasiasa tena wale kutoka chama tawala cha Jubilee ambao wanadai ni vigumu kutenganisha siasa na kuwatumikia wananchi. Kundi hili ambalo wengi wanamuunga mkono Naibu Rais, William Ruto katika mbio za kuwania urais 2022 wanasema jukumu la kwanza la mwanasiasa ni kupiga siasa kwa kisingizio kuwa unaweza ukasahaulika kama hujihusishi na siasa ukisubiri muda wa kampeni. Hii ni hoja ambayo wananchi wanapinga na kusisitiza mwanasiasa au kiongozi anayewatumikia waliompigia kura kwa kuhakikisha anasimamia miradi ya maendeleo ndiye atakayepata kura kutokana na kazi yake kuonekana kwa vitendo. Rais Uhuru ambaye anakerwa na baadhi ya wanasiasa ndani ya Jubilee wanaomshinikiza atamke kumuunga mkono Ruto kama mrithi wake, hivi karibuni alitoa maneno ambayo yanaashiria huenda asimuunge mkono naibu wake 2022. Akizungumza Ruto katika Kaunti ya Kiambu wakati anafungua kiwanda cha Bidco, Uhuru alisema ni Mungu pekee ambaye ataamua nani atakuwa Rais ajaye hivyo kuwataka viongozi kuacha kuweweseka na badala yake kuwahudumia Wakenya. “Uchaguzi utakuja na Mungu ndiye hupeana uongozi. Tufanye kazi,” alisema na kauli yake ilitafsiriwa kumlenga Ruto ambaye amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali nchini Kenya, ikitajwa ni lengo la kujitambulisha huku wafuasi wake wakisema Rais Uhuru anatakiwa kutimiza ahadi aliyotoa 2013 ambayo ni kumuunga mkono Naibu Rais. Moja wa wafuasi sugu wa Ruto, Oscar Sudi ambaye ni Mbunge wa Kapseret, alinukuliwa akimtaka Rais Uhuru kujiuzulu akijigamba anaweza kuongoza nchi vizuri endapo Rais atamuachia kwa miezi mitatu tu. “Ukiona Rais hawezi kukutana na viongozi, magavana na maseneta ambao wanalazimika kuandamana barabarani, ujue iko shida,” alisema Sudi akiwa nyumbani kwake Kapseret, Kaunti ya Uasin Gishu. Kelele za baadhi ya wanasiasa wa Jubilee zinazolenga kumpigia debe Naibu Rais Ruto hususan baada ya kitendo cha Machi 9 mwaka jana, Rais Uhuru alipokutana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na kuzika tofauti zao za kisiasa, zimekuwa zikizimwa na Uhuru ambaye amepania kutimiza ajenda nne kuu ikiwemo kupambana na ufisadi. Kauli ya Rais Uhuru ya hivi karibuni kwamba Mungu ndiye hupeana uongozi ikionekana kukwepa kumpigia debe Ruto inakinzana kwa kiasi fulani na ile aliyowahi kusema mwaka jana akiwa ziarani Nyeri kufungua soko la Karatina. Rais aliyeonekana kukasirishwa na wabunge wanaoteka eneo lake la ubunge muda mwingi kutumia kujadili siasa za 2022 badala ya kufanya mambo ya msingi yanayogusa wananchi, alisema chaguo la mrithi wake litawashangaza wengi.   “Wanafikiri kwa sababu Uhuru ataenda nyumbani 2022, hatakuwa na neno la kusema kuhusu nini kitakachotokea. Ninawaambia wakati muda muafaka ukifika, nitakuwa na kitu cha kuzungumza,”alisema Rais Uhuru katika mkutano wa hadhara. “Wengine wanafikiri nimenyamaza kwasababu siwezi kuongea kuhusu siasa. Mimi bado ni mwanasiasa. Watashangaa chaguo langu muda huo utakapofika, lakini kwa sasa nataka nijihusishe na kutekeleza ahadi nilizotoa kwa Wakenya.”

Kumpongeza Magufuli sio kosa, ni haki yake

$
0
0
MHINA SEMWENDA KAMA kijana ninajiona nina deni kubwa sana kwa nchi yangu, mimi kama Mtanzania nimebahatika kushuhudia, ukuaji mkubwa wa nchi yetu katika awamu hii ya tano chini Rais Dk. John Magufuli. Nashukuru sana Mungu amenijalia uhai wa kuweza kuona maendeleo haya.  Miaka ya nyuma kabisa nikiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam, niliwahi kutamani kumwona Magufuli akiwa Rais, sidhani kama wakati huo yeye binafsi alikuwa na malengo ya kuwa Rais, hamasa niliipata kutoka kwenye wimbo wa msanii Roma Mkatoliki enzi hizo sikuwahi kuhisi kama Magufuli angekuwa Rais ila niliishia tu kutamani. Nashukuru ndoto yangu ilikuja kuwa kweli, na sasa yale niliyoyatamani ninayaona kwa macho yangu. Maeneo mengi ya nchi yetu sasa yanapitia katika mabadiliko makubwa ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, vituo vya kufua umeme, ujenzi wa shule na hospitali pamoja na mengine mengi. Kwa bahati mbaya, sijawahi kuwa mwanasiasa wala sijawahi kutamani kuwa mwanasiasa lakini ni ukweli usiopingika kwamba Rais Magufuli anafanya kazi nzuri. Kwa dhati ya moyo wangu nampongeza Rais Magufuli, hakika naamini na bado naamini kabisa kwa tulikopitia watanzania na maendeleo yanayofanyika sasa. Sisi Watanzania tulipaswa kuwa wasemaji wakuu wa huyu mzee na kupongeza jitihada zake. Lakini kwa siasa za Tanzania zilivyo, sasa Rais Magufuli anatumia nguvu kubwa kutueleza tena watanzania kile anachotufanyia nahisi labda kuna wakati anataka kukata tamaa na nahisi labda ndio namna siasa inavyomtaka afanye. Kiubinadamu hata kama unamfanyia mtu jambo kubwa na hakuelewi unaamua kuachana naye na kuendelea na mambo yako. Ni sawa na mzazi anayepambana na mtoto ambaye hataki shule mwisho wa siku mzazi akikata tamaa akamuacha mtoto ndio huwa anaharibikiwa. Mara nyingi ukimsikiliza Rais Magufuli anazungumza kuhusu Tanzania na maendeleo ya Tanzania kwa Watanzania wenyewe akiitakia mema Tanzania, sasa hata kama ni siasa ndio zilivyo ifike muda basi tumwelewe huyu mzee tumpe nafasi ya kuendelea kutufanyia kazi hii kubwa anayoifanya. Ninachokiona mimi sio sawa Rais kutumia nguvu kubwa kutufanyia kazi halafu bado tena atumie nguvu kubwa kutueleza kazi anayofanya kwa sababu anayoyafanya yanaonekana. Mimi kama kijana ninajiona nina deni kubwa kwa sababu sioni kama naitendea haki nchi yangu kwa kushindwa kusimama na kuisemea, tukiachana na itikadi za kisiasa. Vijana tunapaswa kuwa mstari wa mbele kuyasema haya na kupongeza na kuwa mstari wa mbele, kuilinda nchi yetu na rasilimali zetu huku tukiwaacha wanasiasa waendelee na siasa zao. Sio kweli kwamba kazi haifanyiki, inafanyika na tunaona sasa kwanini bado tena tunalaumu na kulalamika au wakati mwingine na kutukana kabisa. Mimi sio mwanasiasa kama nilivyosema, lakini kila kijana au mtu akisimama na kusema au kutoa pongezi kwa Serikali hii utasikia au utaambiwa unahitaji kupewa ukuu wa wilaya au ukurugenzi, kitu ambacho sio sawa. Lazima tujenge misingi ya kutofautisha uzalendo wa kusifia maendeleo na uzalendo wa kuipenda Tanzania na siasa au itikadi za chama kimoja au kingine. Kupongeza au kusifia sio kosa au sio dhambi, ni utashi tu wa kibinadamu. Sasa kama itikadi za kisiasa ndio zinafanya tushindwe kuona yanayofanywa hata kama yanaonekana basi kuna shida kwenye siasa zetu. Muda wote ninaposhuhudia siasa zetu nimejaribu kuwa muwazi ili nisiburuzwe na itikadi bali niwe katika mtazamo wa wazi.   Kiubinadamu viongozi wanaweza kukosea wao sio malaika lakini sio baya moja lifute mazuri yote yaliyofanywa. Kila binadamu anafanya makosa hata mimi binafsi nimefanya makosa huko nyuma na bado nitafanya makosa. Iweje kila linalofanywa kwa maendeleo ya nchi yetu lionekane baya kisiasa wakati kiuhalisia sisi ndio tunaonufaika nalo? Nitatoa mfano midogo, ujenzi wa hospitali ni kwa manufaa yetu au wanasiasa? ujenzi wa barabara ni kwa manufaa yetu au, ujenzi wa madaraja ni kwa manufaa yetu au? Jibu ni ndio kwa sababu sisi ndio watumiaji wakuu wa miundombinu hiyo pamoja na mingine mingi. Ubora wa barabara ni kwa manufaa yetu pamoja na mengine mengi, sasa sijui watanzania tunatakiwa tufanyiwe nini na viongozi wanaokuwa madarakani ili tuweze kuelewa na kuwapongeza huku tukiweka itikadi zetu za kisiasa pembeni. Tukiachana na sifa za kisiasa au pongezi za kisiasa na wanasiasa, Watanzania tunapaswa kuwa wasemaji wakuu wa maendeleo yetu kwa nchi yetu. Na sio kuwaacha wanasiasa kuwa wasemaji wa midomo yetu, kuona kwa macho yetu  na kuhisi hisia zetu, kwamba kila atakayesifia anataka madaraka au anataka kiki au anataka kujionesha hii sio sawa kabisa.  Tujifunze kutengenisha siasa na maendeleo ya nchi yetu. Tuiangalie nchi yetu kwanza kisha siasa ndio zifuate. Siasa isiwe sehemu ya kukatisha tamaa, watendaji wa Serikali katika kutimiza majukumu yao au siasa isiwe sehemu ya kuwafanya watanzania wasiwe huru kusifia maendeleo wanayoyaona. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Rais Magufuli anafanya kazi kubwa kwa nchi hii. Tumuunge mkono na tuwe sehemu ya kumpa moyo na faraja ili apate moyo wa kufanya makubwa kwa nchi yetu. Kuna siku niliwahi kuwaza jambo moja. Hivi mtu anapokuwa kiongozi (Rais) na akafanya kazi yake vizuri ana lipi la kupoteza kati yetu sisi Watanzania au yeye kiongozi.  Nitatoa mfano, Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete au Rais wa awamu ya tatu, Benjami Mkapa na Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wana lipi la kupoteza? Baada ya kumaliza vipindi vyao na sasa wamepumzika. Hayo waliyoyafanya katika kipindi chao wasingeyafanya kwani wasingekuwa walivyo sasa? Wamefanya yao mengi mazuri na mengine mabaya, lakini sasa wamepumzika wamemuachia kijiti Rais Magufuli ambaye naye itafika siku yake atapumzika. Sasa kwanini kwa haya anayoyafanya kwetu sisi Watanzania tusimpongeze na kumpa moyo afanye zaidi maana mwisho wa siku, sisi ndio wanufaika wa haya yote. Vijana bado tuna deni kubwa kuisimamia nchi yetu na kuuweka uzalendo wetu mbele na kuachwa kuongozwa na itikadi za kisiasa, hata tukasahau mambo ya msingi katika kuijenga nchi yetu. Lazima tujenge utamaduni wa kujivunia vilivyo vya kwetu. Rais ni wetu tulimchagua wenyewe kwanini tusimuunge mkono na kumpa nguvu kuipeperusha bendera na nchi yetu vizuri? Popote duniani, ukitamka Tanzania lazima Magufuli ndio aonekane nyuma ya bendera yetu sasa kwanini tusimuunge mkono na kumsaidia kuipaisha nchi yetu kimaendeleo. Vijana tuna deni kubwa kwa nchi yetu tusipoliangalia hili sijui, watoto wetu siku zijazo watakuwa na hali gani. Mimi binafsi nimejitoa kukupongeza na kukusifia na zaidi kukutia moyo. Pambana. Nchi yetu itafika tunakotaka. Mengineyo yatafuata baadaye. Kwa sisi tusio wanasiasa hatufuati itikadi zetu, lakini tunamsemea mama Tanzania ambaye wewe leo ndio unamjenga na alama unazoweka zitabaki daima hata kama sio kwetu ni kwa watoto wetu na wajukuu zetu. mhina.semwenda@gmail.com

Ukosefu wa shule ulivyoharibu ndoto za watoto Bagamoyo

$
0
0
*Dk. Kawambwa aomba wadau wa maendeleo kujitokeza AVELINE KITOMARY  NI ukweli usiopingika kuwa elimu ni msingi wa ustawi mzuri wa kutambua, kuelewa na kufanya vitu mbalimbali katika kila jamii yoyote ile inayohitaji kusonga mbele kimaendeleo.  Katika jamii yetu, zamani ilikuwa ikitolewa elimu ya mila,utamaduni na desturi mbalimbali ambapo wazee au wazazi walijihusisha kuwapatia elimu watoto na vijana. Lakini kwa ulimwengu wa sasa wa ushindani ili nchi au sehemu yoyote iweze kufanikiwa kiuchumi,kisiasa, kilimo, ufugaji na mengine kuna haja ya kupitia darasani kupata elimu. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi chake cha uongozi alipata kuwataja maadui watatu wa maendeleo kuwa ni ujinga,maradhi na umasikini.  Muonekano wa kijiji cha Fuyosi, kitongoji cha Kalimeni, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Kutokana na hilo, Rais wa awamu ya tano, John Magufuli amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupambana na maadui hao. Pamoja na mafanikio hayo, lakini kwa baadhi ya sehemu kumekuwa na changamoto kubwa ya elimu,afya na umasikini.  Mwandishi wa makala hii ataelezea jinsi ukosefu wa huduma za kijamii kama elimu unavyoangamiza ndoto za watoto wengi katika Kijiji cha Fuyosi iliyopo Kitongoji cha Kalimeni wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani. Kitongoji hicho cha Kalimeni kina jumla ya kaya 268 ambapo kati yao kuna wanaume 144 na wanawake 124 takwimu hizo ni za mwaka 2017 lakini bado kunaongezeko la watu. Shughuli kubwa inayofanywa katika kitongoji hicho ni kilimo cha mahindi na mihogo, hata hivyo wanakijiji hao bado wako katika umasikini uliokithiri. Asilimia kubwa ya wanakijiji hawajui kusoma wala kuandika, kuanzia wakubwa mpaka wadogo, naweza kusema hawaendani kabisa na dunia ya sasa ni kama watu waliosahaulika gizani.  Umasikini na ukosefu wa huduma za shule, afya,maji, migogoro ya wakulima na wafugaji na barabara, umekuwa ukizunguka kingo za Kitongoji hicho tangu nchi ipate uhuru. Kizazi hadi kizazi wamekuwa hawana desturi ya kupata elimu, watoto wengi sasa wako kijijini bila hatima yao kujulikana. Kutokana na kukosekana kwa huduma ya elimu kwa watoto katika kijiji hicho, hali hiyo imesababisha watoto wengi kujiingiza katika vitendo visivyoendana na wao kama ndoa za utoto,mimba katika umri mdogo na wizi kwa watoto wa kiume. Sababu kubwa ya watoto wengi waliofikisha umri wa kwenda shule kutokwenda ni umbali wa shule iliyopo katika kijiji mama cha Fukayosi.  Ni takribani kilometa 12 huduma ya elimu inapatikana hivyo kusababisha watoto kushindwa kwenda shule na kubaki nyumbani na wazazi wao.  Watoto wengi walijaribu kwenda shule lakini wameishia njiani kutokana na changamoto za umbali wa kilometa hizo nyingi, huku wazazi wakiwa hawana uwezo wa kuwalipa gharama za usafiri wa kwenda shule kila siku. MADHARA YA BAADAYE YA KUKOSA ELIMU Subira Fikiri ni mtoto mwenye umri wa miaka 15, anasema aliwahi kusoma shule ya awali kwa miaka minne baada ya kupona akaamua kuacha na kubaki nyumbani na mama yake,hakuweza kwenda shule ya msingi kwa sababu ya umbali.  “Nimebaki na mama yangu,baba alishafariki nilipelekwa kusoma chekechea kwa miaka minne 20012-2015, kwani hii ndio ipo hapa kijijini kwetu baada ya miaka yote nikaamua kuacha na sasa nakaa tu nyumbani. “Sijui kusoma wala kuandika kwani  nilishindwa kusoma shule ya msingi kwasababu ya umbali wa shule, hata hivyo mama yangu hana uwezo wa kugharamia nauli hata uwezo wakunipangishia chumba hana,”alisema Subira. Subira ambaye tayari ana mtoto aliyetimiza mwezi mmoja na siku 20, anasema amekata tamaa kabisa ya kupata elimu kutokana na hali yake ya sasa. “Baada ya kukaa nyumbani muda mrefu sikuwa na la kufanya niliingia katika vishawishi vya kingono baada ya hapo nikapata mimba na sasa nina mtoto mmoja katika umri huu mdogo sijui hata nifanyeje,”anasimulia kwa masikitiko. Kuhusu ndoto ya kupata elimu, Subira anasema alitamani siku moja awe daktari ili aweze kuisaidia jamii ya Kitanzania.  “Ndoto yangu kielimu nilikuwa nataka nisome ili niwe daktari nitibu watu hasa jamii yangu lakini sasa niko tu hapa kijijini ndoto zangu, zimeishia njiani sasa nina mtoto ananitegemea, mama yangu kama unvyomuona hana uwezo,nyumba yenyewe ndio hii inakaribia kuanguka,”anaelezea Subira. Subira anasema hata sasa anatamani kusoma ili atimize malengo yake endapo kama atapata mtu wa kumsomesha. “Natamani hata sasa ningesoma,napenda kupata elimu, nikipata nafasi ya kusoma naamini nitafanya vizuri na ninaweza kutimiza ndoto yangu,”anasema. Mtoto mwingine, Salum Kindamba mwenye umri wa miaka 14, licha ya umri wake wa kusoma kufika lakini bado hajaanza hata darasa la kwanza na hajui kusoma wala kuandika.  “Wazazi wangu hawana uwezo wa kumlipia nauli ya pikipiki ili niende shule hapa nina wadogo zangu watano wote waliofikia umri wa kwenda shule hawaendi pia,naomba Serikali itujengee shule,”anasema Kindamba. Mmoja wa watoto anayesoma akitokea kijijini hapo, Husen Saleh mwenye umri wa miaka 12 anasema anasoma darasa la pili lakini kutokana na kuchelewa kufika shule imesababisha afanye vibaya katika mitihani. “Tuko wawili tu tunaokwenda shule, tunapata shida ya usafiri wakati mwingine huwa tunaenda kwa miguu,wakati mwingine tunavizia lift na wakati mwingine hatuendi kabisa shule. “Tunaweza kufika darasani saa nne au tano tukifika mwalimu ameshafundisha tunachukua madaftari ya wenzetu tunaandika,mwalimu yeye hatuchapi kwasababu anajua tunatoka mbali lakini darasani hatufanyi vizuri na hatusomi vizuri,”anaelezea Husen. UMASKINI UNACHELEWESHA UJENZI Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kalimeni, Amos Rungwa anasema usaili walioufanya Novemba mwaka jana watoto 120 wanatakiwa waende shule. Kwa mujibu wa Rungwa, eneo la ujenzi wa shule tayari limeshatengwa na kupimwa hivyo kilichobaki ni ujenzi wa madarasa kuanza. “Takwimu za mwaka jana tulivyoanza kupata kibali cha kuanzisha shule, tuna watoto wako mtaani 120 ambao wamefikisha umri wa kwenda shule ni miaka mitano sasa tangu kijiji kimetenga eneo kwaajili ya ujenzi wa shule lakini mpaka sasa bado hatujafanikisha. “Tangu tumefanya takwimu wengine wameshazaliwa na wengine muda wao wa kuanza shule umeshapita, mfano mtoto wa miaka 7 anatakiwa aende shule sasa tunapobaki naye mpaka anafika miaka 14 hata akipelekwa darasa la kwanza wenzake watamshangaa,”anasema Rungwa. Anaeleza kuwa watoto wengi mpaka sasa hawasomi na wako kijijini, huku wengine walioanza kusoma wakiishia katikati kwa sasabu ya umbali wa shule kwani gharama za kupeleka mtoto shule nauli ya pikipiki kila siku ni Sh 10,000. “Wengi wako mitaani wengine wameshaoa wengine wamepewa mimba wakiwa watoto,vijana wengine wamekuwa wezi hata juzi tunatoka kuwafunga wawili miaka mitano mitano kwaajili ya wizi hali hii inasikitisha,usafiri ni pikipiki ambapo gharama zake ni Sh 5000 kwenda na Sh 5000 kurudi wazazi maisha duni hawamudu.  Anasema hali ya umasikni uliokithiri katika kijiji hicho, unakwamisha kuanza ujenzi wa shule hiyo wanaendelea kuwahamasisha wanakijiji waendelee kuchanga. “Kama unavyoona ndugu mwandishi hali ya hapa ni mbaya hata nyumba zetu unaziona hapa, wote masikini na darasa moja linagharimu Sh milioni 15 huo uwezo wa kufikia hizo fedha ni ngumu ingawa nitaendelea kuwahamasisha wanakijiji kuchanga na tumepanga kila kaya katika kijiji watoe Sh 5000.  “Hivi karibuni tulipata barua kutoka Ofisi ya Mratibu Elimu wa Kata ya Fukayosi ya kuanza kujenga shule kuanzia la kwanza mpaka darasa la saba lakini bado hatujafanikisha zoezi la uchangishaji. Anawaomba wadau mbalimbali wa maendeleo na Serikali,kujitokeza kuungana na wao katika kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ili watoto wapate elimu. “Tunaomba wadau mbalimbali, taasisi za kidini na Serikali waungane pamoja na sisi kuchangia gharama za ujenzi wa shule ili watoto wetu wasiendelee kukaa mtaani na wao wanapata elimu kama watoto wengine. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkecha anasema changamoto ya elimu ipo kwa vitongoji vyake hasa Kalimeni ambayo ndio iko mbali zaidi kuliko vitongoji vingine. “Vitongoji vinaumbali mrefu kutoka kijiji mama cha Fukayosi tunaendelea kufanya juhudi ili shule hiyo ijengwe,tunaendelea kuchangisha wanakijiji japo wana hali mbaya, tutajitahidi kupita vitongoji vyote tisa kwaajili ya kupata mchango wa Sh 5000,”anaelezea Mkecha.  HALI YA HUDUMA ZINGINE  Mwenyekiti huyo nasema hata huduma zingine za afya,maji na barabara bado ni changamoto kwao.  Anasema katika kipindi cha mwaka 2008 na 2017 akina mama takribani sita walijifungulia barabarani, huku watu watatu wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya uzazi. “Ukiacha elimu hata huduma zingine bado zinachangamoto kama huduma ya afya hatuna, hapa akinamama wakati mwingine wanajifungulia njiani hata ukisema utakodisha gari barabara haipitiki.  “Hali hii imesababisha akinamama kujifungulia barabarani kwamfano tangu mwaka 2008 hadi 2017, akinamama kama sita wamejifungulia barabarani na pia watu watatu wamepoteza maisha mwaka 2017 mama na mtoto wote walipoteza maisha mwaka 2012 mtoto alipoteza maisha kwasababu ya kukosa huduma,”anaelezea Rungwa. Kwa mujibu wa Rungwa hata upatikanaji wa maji katika kitongoji hicho ni changamoto kubwa. Anasema maji yanaletwa kutoka sehemu nyingine na wanalazimika kununua kwa dumu Sh 1500 hadi 2000 kwa dumu moja. “Tulikuwa tumeshaanza kuletewa huduma ya maji kwa mradi wa maji Wami Makurange tangu mwaka juzi, mipira imechimbwa chini bomba ipo na tanki la maji lipo lakini hayatoi maji. “Sisi tunategemea kuletewa dumu ni Sh 1500 mpaka 2000 na sio watu wote wanamudu kununua maji kwa gharama hiyo kubwa tunaomba Serikali pia iingilie hili maana hata mkandarasi wa mradi huu wa maji hatumwelewi,”anabainisha Rungwa.  MBUNGE AAHIDI KUTOA MATOFALI  Mbunge wa Bagamoyo, Dk.Shukuru Kawambwa anakiri kuwepo kwa changamoto ya huduma za jamii katika kitongoji hicho ikiwemo ile ya kupata elimu. Anasema kutokana na hali ya umasikini ya wananchi wake amechangia matofali 5,000, hivyo anaahidi kuwa atafuatilia suala la ujenzi hadi utakapokamilika.  “Yote hayo nayajua na tunahangaikia na tayari nimeshawachangia matofali,wananchi wangu ni masikini lakini nawaomba waunge mkono juhudi za ujenzi wa shule. “Nitaenda Kalimeni wiki ijayo nijue wamefikia wapi na katika kikao changu nahamasisha sana hilo ni kweli watoto kule hawasomi na sio jambo zuri pia naelewa umbali wa shule ni mrefu nalifuatilia kwa ukaribu,”anaeleza Dk Kawambwa. Dk. Kawambwa aliyepata kuwa Waziri wa Elimu wakati wa Serikali ya awamu ya nne, anawaomba wadau wa maendeleo waweze kuwasaidia ili kufanikisha huduma za jamii katika eneo hilo. “Tunaomba wadau wa maendeleo wajitokeze, ndugu mwandishi hata mimi nahangaika kuzungumza na wadau wengine ili kufanikisha suala hilo la ujenzi wa shule,”anabainisha Dk. Kawambwa. Kuhusu maji anasema yako katika hatua ya kufika huko na muda sio mrefu watapata huduma hiyo na tayari mradi umeshaanza. Anasema pia atahakikisha barabara inayoelekea katika kitongoji hicho itachongwa ili kurahisisha usafiri. “Kuna mradi wa maji imeshaanza kule hivyo wananchi wangu wasijali watapata maji na pia barabara inayoelekea huko itachongwa ili iweze kupitika,”anaahidi Dk. Kawambwa.  UTARATIBU WA SERIKALI Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa anasema kwa utaratibu wa Serikali wananchi wanatakiwa waanze kujenga baada ya hapo ndio wanaweza kupata msaada wa halmshauri.  Anasema hata hivyo baada ya kusikia hali ya elimu atalifikisha suala hilo halmashauri.  “Kwa utaratibu wananchi wanatakiwa kuanza wao wenyewe halafu halmashauri itawasaidi lakini kwasasabu umeniambia nitalifikisaha suala hilo halmashauri,”anasema Kawawa.

Bobi Wine: Tutaendelea kutetea haki ya wanyonge

$
0
0
Mahakama nchini Uganda imemfungulia mashtaka mbunge wa upinzani na mwanamuzi Muziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine na watu wengine zaidi ya 20 kwa kumkasirisha rais Yoweri Museveni.

Manara aburuzwa kortini, adaiwa Mil 83

$
0
0
HAJI Manara, Msemaji wa Klabu ya Simba na wenzake watatu, tarehe 6 Agosti 2019 wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kudaiwa Sh. 83.5 milioni. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Msemaji huyo na wenzake (Beatrice Ndungu na Palm General Supply), wamefikisha kwenye Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakidaiwa kupokea bidhaa zenye nembo ya Dela ...

Mchanga pekee ni kampeni ya mwaka mzima inayolenga kuhamasisha ukusanyaji wa chupa za plastiki na uhifadhi wa fukwe za bahari

$
0
0
MCHANGA PEKEE ni Kampeni ya miezi 12 iliyobuniwa, kuasisiwa na inayosimamiwa na Kampuni ya Coca-Cola Kwanza Kampuni Tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa ikiwa imeanza mwezi Februari mwaka 2019 yenye malengo na madhumuni ya kuelimisha, kufundisha, kushirikisha na kuhimiza uhifadhi wa plastiki taka (mazingira) katika jamii zetu ikiwa imejikita katika usafishaji wa fukwe zetu, ukusanyaji wa chupa za plastiki, uchakataji na njia bora ya uhifadhi wa chupa za Plastiki nchini Tanzania.

Familia yamrudisha Rooney England

$
0
0
Wayne Rooney amesema familia ndio imemuondoa DC United na kujiunga na Derby County.

Tottenham Spurs yatupa kete yake kwa Dybala

$
0
0
Tottenham imekubali kutoa Pauni69 milioni kunasa saini ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala majira ya kiangazi

Zoezi La Utayari Kukabiliana Na Ugonjwa Wa Ebola Katika Wilaya Ya Buhigwe Mkoani Kigoma

$
0
0
Kufuatia nchi ya jirani (DRC) kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka 2018. Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa iliyomo hatarini kuathiriwa na ugonjwa huo.Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa maendeleo; WHO, FAO, USAID, HRH2030, na USAID Global Health Supply Chain Programu, inaendelea na zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma.Zoezi hilo linalenga kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu, utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo atagundulika, matibabu ya wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kigoma.

Edouard Mendy: Senegal goalkeeper ready for Rennes adventure

$
0
0
Senegal goalkeeper Edouard Mendy is ready for a new adventure at French Ligue 1 club Rennes after joining from rivals Reims.

Brazil: Amazon deforestation rises rapidly

$
0
0
A government institute at loggerheads with Brazil's President Jair Bolsonaro has called the massive increase a "major setback." The right-wing administration's pro-agrobusiness policies are to blame, the agency claims.

Mfungwa aliyevaa nguo za kike ili atoroke jela ajinyonga

$
0
0
Mfungwa wa dawa za kulevya ambaye alikamatwa baada ya kujaribu kutoroka gerezani akiwa amevalia nguo za kike amefariki dunia.

Lowry atoboa siri ya Leonard kuondoka Toronto

$
0
0
Mlinzi wa timu ya Marekani ‘All Star’, Kyle Lowry amesema anajua kwanini Kawhi Leonard angeondoka kwenda Los Angeles Clippers, lakini kiongozi huyo wa muda mrefu wa Toronto Raptors hana mpango kuondoka Canada.

Bolton: US Ready to Sanction Those Who Do Business with Maduro Government

$
0
0
One day after the U.S. imposed a full economic embargo on Venezuela, National Security Advisor John Bolton says the U.S. can now sanction anyone who supports the government of President Nicolas Maduro. Maduro’s government denounced the sanctions as a "grave aggression" that will lead to "the failure of political dialogue." VOA’s Diplomatic Correspondent Cindy Saine has more from the State Department.

Volatility, Uncertainty as US-China Trade War Escalates

$
0
0
U.S. financial markets struggled to rebound Tuesday after their biggest drop since December. U.S. President Donald Trump’s top economic adviser says the White House has the upper hand in deepening trade and monetary disputes with China -- an assertion made after Beijing announced it will no longer buy U.S. agricultural products. VOA’s Arash Arabasadi reports.  

Jumping Like a Lemur, Flying Like a Dragonfly – Robots That Mimic Animal Movements May Be On Their Way

$
0
0
In a laboratory in California, engineers are working on pushing the boundaries of how robots move, imitating the ways some animals jump, fly or crawl. Michelle Quinn met Salto, a one-legged jumping robot to see the future of robots.
Viewing all 132783 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>