Artificial limbs aren't just for humans. Near Washington, an orthotist who once made prosthetics for people is helping disabled animals around the world. VOA's Deborah Block visited a Virginia workshop where devices are built that improve the lives of pets and, in some cases, wild animals.
↧
Custom-Made Braces Help Animals Walk Again
↧
Wafugaji Waangua Kilio Mbele Ya Waziri Mpina Baada Ya Kuchomewa Nyumba Na Mazizi
Na Mwandishi Wetu, BabatiWAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesitisha operesheni ya kuwaondoa na kuwachomea nyumba, mazizi ya mifugo, makambi ya uvuvi Wananchi wa Kijiji cha Vilima vitatu Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara na kuunda timu ya wataalamu kutoka Wizara 8 kufuatilia utekelezaji wa operesheni hiyo na kuwasilisha ripoti hiyo serikalini kwa maamuzi zaidi. Operesheni hiyo iliyofanyika mwezi Julai mwaka huu imesababisha wananchi wengi kukosa mahali pa kuishi kutokana na nyumba zao kuchomwa moto ambapo sasa wanaishi chini ya miti hali iliyosababisha adha kubwa kwa wanawake wajawazito, watoto na wagonjwa. Pia mifugo yao kuvamiwa na wanyama wakali na mingine kupotea baada ya mazizi kuchomwa moto, shughuli za uvuvi kusimama baada ya makambi na zana za uvuvi kuteketezwa kwa moto hali ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi na kushindwa kujua la kufanya. Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Vilimavitatu na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu huku idadi kubwa ya wananchi wakiangua vilio mbele ya Waziri Mpina wakionesha masikitiko yao kuhusiana na unyama waliofanyiwa na Serikali ya wilaya hiyo na kumuomba kuwasaidia ili waweze kurudi katika maisha yao ya awali. Walisema mbali na madhara hayo pia akiba ya chakula walichokuwa nacho majumbani mwao nacho kimechomwa moto hivyo kukosa kabisa chakula na kumuomba afikishe kilio hicho kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ili wapatiwe msaada wa haraka chakula ili kunusuru wasife kwa njaa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia. Waziri Mpina alihoji iweje operesheni hiyo ifanyike huku kukiwa na katazo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la Januari 15 mwaka huu la kusitisha operesheni zote za kuwaondoa wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayodaiwa kuwa ni hifadhi hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo. Waziri Mpina pia ahoji iweje operesheni hiyo ifanyike kwenye eneo hilo huku kukiwa na Hukumu ya Mahakama iliyoliondoa eneo la Kijiji cha Vilima Vitatu kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyapori Burunge (Juhibu) ambapo hukumu hiyo haikukatiwa rufaa wala kutenguliwa na Mahakama. Pia Waziri Mpina alihoji iweje operesheni hiyo ya kuondoa mifugo ifanyike bila kushirikisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kama Sheria, Kanuni na miongozo inavyoelekeza hali iliyosababisha mifugo mingi kuteseka kwa kukosa huduma muhimu zikiwemo chanjo, dawa, maji na malisho na kusababisha mifugo kupotea na mingine kufa na kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji taifa. Kwa msingi huo, Waziri Mpina alisema operesheni imefanyika kinyume cha Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Namba 17 ya mwaka 2003, Sheria ya Ustawi wa Wanyama Namba 19 ya mwaka 2008, Sheria ya Nyanda za Malisho na Rasilimali za chakula cha Mifugo namba 13 ya mwaka 2010 na Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003. Hivyo alisema wote waliohusika kufanya operesheni hiyo walipaswa kukamatwa na kushtakiwa kutokana na makosa ya kuvunja sheria hizo za mifugo kwani wanalo jukumu la kuzisimamia ili zisivunjwe kwakuwa mifugo ni rasilimali muhimu kwa Taifa kama zilivyo rasilimali nyingine nchini. Waziri Mpina alieleza kasoro nyingine za operesheni hiyo kuwa pamoja na kutokufanya tathmini ya kina ya idadi ya wananchi, kaya, mifugo na mali zingine kabla ya operesheni kufanyika, kukosekana kwa nyaraka muhimu za kuendesha operesheni na mahusiano dhaifu baina ya wafugaji, JUHIBU na Mwekezaji Kampuni ya Chemchem Lorge ya nchini Ufaransa. Pia Waziri Mpina alisema kasoro nyingine ni kutokamilika kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwani kama ungekamilika ungekuwa ndio muarobaini wa migogoro katika Kijiji cha Vilima Vitatu na vijiji vingine 9 vinavyounda Hifadhi ya Wanyamapori Burunge. Pia Waziri Mpina aliwaonya viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania kutojihusisha na vitendo kuhamasisha uvunjifu wa sheria za nchi na kama kuna masuala muhimu yanayowahusu wafugaji wafuate njia sahihi za kukutana na mamlaka husika kutafuta suluhu, Pia amewataka wafugaji kote nchini kufuata Sheria. Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Babati Vijijini, Filbert Mdachi alisema CCM imesikia malalamiko ya wananchi wa kuwahakikishia kuwa haki itatendeka na kumshukuru Waziri Mpina kwa kufika eneo hilo ili kutafuta suluhu ya mgogoro huo ulisababisha adha kubwa kwa wananchi. Mkuu wa Wilaya ya Babati, Kitundu alisema alisema operesheni hiyo ilifanyika baada ya kudaiwa kuwepo viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo hayo na kukiri kupokea maelekezo kutoka mkoani .
↧
↧
Serikali Ya Tanzania Na Uganda Zashirikiana Kutekeleza Ujenzi Wa Mradi Wa Umeme Wa Maji Kikagati-murongo
Serikali za Tanzania na Uganda zinatekeleza ujenzi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kufua umeme wa maji wa Kikagati-Murongo, uliopo kwenye mto Kagera mpakani mwa nchi hizo mbili utakaozalisha megawatts 14.Inakadiriwa kuwa kila nchi itapata megawatts saba kati ya hizo 14 zitakazozalishwa mara baada ya Mradi huo kukamilika.Mradi huo wa umeme wa unajengwa na kampuni ya kikandarasi ya PAC ya Italia unasimamiwa na kampuni Binafsi ya Uganda ya Kikagati-Murongo hydropower project ambayo ndio mjenzi wa Mradi huo ulioanza Mwezi Mei 2018 na kutarajia kukamilika Mei 2021 kwa gharama dola Milioni 90.Ujenzi wa Mradi huo ni makubaliano ya nchi mbili za Tanzania na Uganda ya matumizi bora ya maji ya mto Kagera ambao upo mpakani mwa nchi hizo.Bw.Geoffrey Mwambe ametembelea eneo la Ujenzi wa Mradi huo ili kukagua Maendeleo ya Ujenzi wake na kutaka maazimio ya Ujenzi wa Mradi huo ya asilimia 50 kila upande wa nchi hizo mbili za Tanzania na Uganda yazingatiwe.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti alisema kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika mkoani kwake.Mhandisi Mshauri wa Mradi huo kutoka Kampuni ya nguvu za Nishati ya Geni Mhandisi Dkt Juliana Pallangyo alisema watasimamia ipasavyo ili kufanikisha Ujenzi wa Mradi huo na kuongeza kuwa kila nchi itanufaika katika kila hatua za Ujenzi na uendelezaji wa Mradi huo.Mradi huo wa Kikagati-Murongo unajengwa kwenye Wilaya za Kyerwa Mkoani Kagera Tanzania na Wilaya ya Isingilo Nchini Uganda.
↧
Usichokijua kuhusu hali ya maisha Ujerumani
MWANDISHI WETU
UNAPOIZUNGUMZIA Ujerumani, inakujia taswira ya taifa tajiri
kabisa barani Ulaya, kwa maana linaloongoza kwa uchumi mkubwa.
Kiwango cha ukosefu wa ajira kiko chini ya asilimia sita,
bei za nishati na vyakula kwa wastani ziko chini kulinganisha na mataifa mengi
ya Ulaya.
Mwanachama huyo namba moja kwa nguvu na ushawishi katika
Umoja wa Ulaya (EU), mbali ya kuwa nchi yenye uchumi imara, pia ni ya pili
duniani kwa usafirishaji wa bidhaa ng’ambo na ya nne kwa ukubwa wa uchumi
duniani.
Wakati mdororo wa uchumi ulipoiathiri dunia ukianzia Marekani
katika miaka ya mwisho ya utawala wa Rais George Bush, kabla ya kusambaa hadi
Ulaya mwanzoni mwa mwongo huu, Ujerumani ilikuwa moja ya mataifa machache
duniani yaliyobakia imara.
Ilihali mataifa mengi kama vile Ugiriki, Ureno, Italia na
mengine mengi yakitikisika vibaya kiasi cha kukaribia kufilisika na kuufanya
Umoja wa Ulaya kuyumba na kuelekea kumeguka.
Kwa kushirikiana na mataifa mengine wanachama, hasa yanayoifuatia
kwa ukubwa wa uchumi barani humo kama vile Ufaransa, Ujerumani ikachukua hatua
mbalimbali kujaribu kunusuru hali. Juhudi hizo zimeweza kulituliza jahazi la EU
lililiokuwa likienda mrama kiasi cha kuifanya Uingereza ambayo imekuwa haikikubali
chombo hicho kuchekelea hali hiyo, kwamba ilikuwa sahihi kukipinga.
Moja ya mamia kwa maelfu ya familia zinazoishi bila umeme Ujerumani
Lakini kwa sasa ni EU inayochekelea si Uingereza, ambayo
mwaka 2016 ilipiga kura ya kujiondoa kutoka chombo hicho, lakini baadae ikaonekana
kujuta kuchukua uamuzi huo.
Ndio maana haishangazi, kwa hili wimbi linaloitikisa dunia
kwa sasa la wahamiaji wanaojaribu kusaka maisha bora Ulaya limevuma zaidi Ujerumani
kuliko hata Italia, ambako ni lango kuu la kuwapokea wakitokea Afrika au Asia.
Wakimbizi hawa wengi wao huishia kufa kwa kuzama baharini
au kwa maradhi ama kuishia makambini wakiomba msaada au kuteseka utumwani huelekeza
macho Ujerumani.
Huvutiwa zaidi na Ujerumani kwa sababu ya utajiri, uimara
wa uchumi na ubora wa maisha walionao, kulinganisha na mataifa mengine
wanachama wa EU.
Lakini licha ya taswira hiyo njema inayoonesha neema na
ustawi wa taifa hilo, kuna upande wa pili wa shilingi wa taifa hilo.
Kwamba, umasikini upo nchini Ujerumani, licha ya kwamba
hakuna makazi duni au holela kama yale tunayoyaona hapa kwetu.
Ni upande hasi, ambao maelfu ya Wajerumani wanaishi maisha
ya udhalili, hushindwa kumudu kulipia bili za umeme na hata kupata mlo na
mahitaji mengine kutokana na umasikini.
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi ya Shirika la Misaada la
Caritas, maelfu ya Wajerumani wanaishi bila huduma ya umeme kwa sababu hawana
uwezo wa kuilipia licha ya kuwa hili ni taifa tajiri kabisa Ulaya.
Ripoti hiyo ilikuja huku Shirika la Watoto la Umoja wa
Mataifa (UNICEF) likisema kuna ongezeko la umasikini miongoni mwa watoto kwa
asilimia 2.7 nchini humo.
Aidha, inakuja huku Chama cha Kusaidia wasio na Makazi (BAG
W.) kikisema watu zaidi ya 800,000 wanaishi mitaani kwa kukosa makazi rasmi
nchini humo.
Kwa ushirikiano na Shirika la Utafiti wa Masuala ya
Kiuchumi Barani Ulaya (ZEW), Caritas limelivalia njuga suala hili na kulifanyia
utafiti wa kina.
Matokeo ya uchunguzi, ambayo yametolewa rasmi hadharani
yameonesha hali ilivyo ya kutisha.
Kwa mujibu wa utafiti huo, katika kipindi cha miaka mitatu
iliyopita, familia 328,000 zimelazimika kukatiwa huduma za umeme na nyingine
milioni 6.6 zikiwa hatarini kufungiwa huduma hiyo muhimu.
Kimsingi kukatiwa umeme ni jambo la mwisho kabisa linalofanywa
na kampuni ya kutoa huduma hizi ikiwa mtu anashindwa kulipia gharama hizo.
Kwanza, mtu hupewa muda wa kulipia gharama ya umeme
aliotumia endapo alibakisha deni la zaidi ya Euro 100 sawa na zaidi ya Sh
300,000 za Tanzania.
Kwa kawaida, hutumiwa mara kadhaa barua ya kumpa onyo na
baadaye kutahadharishwa kwamba atakatiwa umeme.
Kwa wengi waliokutwa na hali hiyo, walifungiwa huduma hizi
pale tu gharama zilipokuwa zimefikia kiwango kikubwa mno.
Si tu wanatakiwa kulipia deni hilo kabla ya kurudishiwa
umeme, bali pia wanatakiwa kulipia tena gharama za kurudishiwa huduma hizo.
Ada ya kurudishiwa huduma ya umeme inaweza kufikia hadi
Euro 200 sawa na zaidi ya Sh 600,000.
Lakini kwa wengi ambao ni watu wanaopokea ruzuku kutoka serikalini
ya kuwasaidia kuishi na wale wenye kipato cha chini kabisa nchini Ujerumani,
hata kiwango hicho bado ni kikubwa kwao na mara nyingi hawawezi kukimudu.
Idadi ya watu waliofungiwa huduma ya umeme kwa kipindi cha
mwaka mmoja imebakia katika kiwango kile kile, ikimaanisha hawakuweza
kujikomboa kuilipia.
Lakini hadi sasa haijawa wazi ni kina nani hasa ndio waathirika
zaidi wa janga hili.
Suala la kufungiwa huduma za umeme nchini Ujerumani
linazitia hofu familia nyingi ambazo ziko hatarini.
Walio wengi kabisa wanaokabiliwa na kitisho hiki ni familia
zenye mzazi mmoja – nyingi zikiwa ni zile zenye kipato kidogo zikiishi chini ya
mpango wa ‘Herz Vier’, yaani posho kwa
watu wasio na ajira.
“Kundi kubwa kabisa lililoingia katika hali hiyo ni la watu
wenye elimu ndogo na ambao wanazongwa na mzigo mkubwa wa madeni na wameshindwa kuelewana
katika utatatuzi wa suala hilo na idara za serikali zinazohusika,” unasema
utafiti huo wa Caritas.
Kwa mujibu wa
utafiti huo, hata familia inayoishi na mtoto mchanga wa miezi sita inakatiwa
umeme na kusababisha malezi ya mtoto kuwa magumu.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba kwa wengine wanaoishi
katika hali hii hulazimika kuachia mtoto kama huyo kuchukuliwa na familia
nyingine itakayomudu kumlea.
Ushauri uliotolewa na ZEW ni kwamba watu wanaoandamwa na
madeni inawabidi kutafuta uwezekano wa haraka wa kupata usaidizi.
Inabidi kuanza kutafuta ushauri wa kupambana na madeni. Juu
ya yote, watu wanapaswa kujifunza kuanza kujisaidia wenyewe kabla ya kuomba
msaada.
Licha ya suala la umeme, kuna idadi kubwa ya watu wanaoshindwa
kula vizuri kwa sababu ya umasikini wao, wakiwamo wastaafu, wazee, wakimbizi,
wasiokuwa na ajira za kudumu na wasio na kazi kwa muda mrefu.
Kanisa Katoliki la Mtaa wa Holweide mjini Bonn ni miongoni
mwa vituo vingi vinavyotoa msaada wa chakula, matunda na hata nguo kwa wenye uhitaji.
Kituo hicho hukusanya mabaki ya vyakula kutoka katika
maduka ya vyakula na masoko ya bidhaa nyingine za jumla na rejareja.
Mchungaji Michael Mombartz anasema hali ya umasikini
imekuwa ikiongezeka katika miaka ya hivi karibuni, jambo linalopunguza kasi ya
ugawaji wa chakula.
“Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, watu hawa wenye
uhitaji walipata chakula kila Jumatatu, lakini kutokana na ongezeko la idadi
yao, hivi sasa hupata mara moja kila baada ya siku 10,” anasema Mchungaji
Mombartz, ambaye amekuwa akisimamia ugawaji wa chakula kwa muda wa miaka 20
sasa.
Watu wengi wanashindwa kupata mlo kamili kwa siku kutokana
na kutokuwa na ajira za kudumu na wengine wakiwa hawana ajira kwa muda mrefu.
Kituo hicho huandaa pia mikutano kwa watu wasiokuwa na
makazi maalumu na kuwagawia mavazi pamoja na vyakula.
Kituo cha Holweide hutumia kiwango cha pato la mtu mwenye
uhitaji ili kufanya mgawo huo kuwa sawa.
Kwa mujibu wa maelezo yake, kulikuwa na ongezeko kubwa la
wahitaji mwaka 2014, tangu wakati huo hali haijabadilika ikimaanisha imeendelea
kubaki palepale au kukua zaidi.
Kituo hicho kilianza kugawa misaada ya chakula mwaka 2014
kikiwa na watu 10 tu, lakini hadi kufikia mwaka 2017 walifika 120, wengi wa
walioandikishwa ni kina mama wanaoishi peke yao, wastaafu na wale wasiokuwa na
ajira kwa muda mrefu.
“Lakini sasa kuna wakimbizi wanaoishi kwenye vyumba vya
kupangisha, ambao nao huchukua chakula na kwenda kupika kwenye makazi yao,”
anasema Mchungaji Mombartz.
Naye Vesna Tomic, anayesaidia shughuli ya ugawaji chakula
kituoni hapo anasema: “Kuongezeka kwa wakimbizi hao hakujaleta shida yoyote ya
msaada. Wote wanaelewa kwamba sasa na hawa wapo, tunajua kwamba hawaji hapa
kujifurahisha bali kwa sababu wanahitaji msaada.”
Mchungaji Mombartz anaona hali ni tofauti kidogo kwa sasa.
Awali watu waliona aibu kufika kituoni hapo, kitu kilichomtia uchungu hasa
akiwaona wazee waliofanya kazi kwa muda mrefu na sasa wanahitaji msaada lakini
wanaogopa kujitokeza.
Maisha ya ugenini bila kuwa na elimu nzuri ya kukupatia
ajira, ni mateso makubwa. Wakati kukiwa na wenyeji wanaoishi katika udhalili,
inakuaje kwa mgeni asiye na mbele wala nyuma kumfanya atoke kimaisha?
↧
Riyad Mahrez: Concerns over medicine taken by Man City winger a 'non-event', says Algerian FA
Concerns over medicine Riyad Mahrez took while on duty with Algeria is a "problem for Manchester City", says the Algerian Football Federation.
↧
↧
US urges Japan to join Persian Gulf naval mission
The US defense secretary said it's time for Tokyo to "strongly consider" joining the US-led mission. Some US allies have rejected the call, saying a European approach is the only way to tackle the unfolding crisis.
↧
US slams 'intolerable' support for Venezuela's Maduro
National Security Adviser John Bolton said Venezuela was now part of an "exclusive club of rogue states," and issued a stark warning to any countries wanting to do business with Caracas.
↧
Michael Job aka ‘Fake Jesus’ is not dead, spotted in Nakuru Kenya
American actor and preacher Michael Job, aka ‘Fake Jesus’ who hit the headlines early this week is not dead as several news outlets in Tanzania and Kenya reported.
↧
Why attitudes towards sex may change rapidly in future
Many of our answers probably include a reference to reproduction. Sex is the primary way that babies are made.
↧
↧
Aibu 20 za Wanaume Endapo akifanya Haya
AIBU 20 ZA WANAUME:1. Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume kulishwa na mkewe.2. Ni aibu na fedheha mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mkeo ukakala ukakoroma na taulo ukafunga..3. Ni aibu na fedheha kuendesha gari la mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki gari alafu unawaka wivu juu yake.4. Ni aibu na fedheha kuishi na mwanamke ambaye wakwe zako wanajua kuwa anakuzidi uwezo.5. Ni aibu na fedheha kumuoa mwanamke ambaye anamiliki uchumi wa familia hata watoto anasomesha yeye wewe unajivunia urefu wa kimo6. Ni aibu na fedheha kila likizo unaenda kijijini kwa mkeo na watoto wote kisa yeye anazohela7. Ni aibu na fedheha kukaa miaka mingi unamlaumu mkeo kuwa hazai wakati wewe huna hata mtoto wa kusingiziwa8. Ni aibu na fedheha kumrudia mwanamke aliye kuacha yeye mwenyewe kipindi kirefu na akaamua kukurudia yeye mwenyewe tena kwa masharti kutoka kwake.????9. Ni aibu na fedheha kupewa zawadi ya kiwanja na wakwe zako siku ya send off.????10. Ni aibu na fedheha kujenga kwenye kiwanja cha mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki kiwanja11. Ni aibu na fedheha kulelewa mtoto wako na baba wa kambo wakati wewe upo unaishi na unajiita kidume12. Ni aibu na fedheha kukaa kwenye nyumba yenye fenicha zoote kanunua mkeo????13. Ni aibu na fedheha kusimamia ujenzi wa nyumba ya mkeo wakati wewe huchangii hata shilingi mia14. Ni aibu na fedheha kulea mtoto ambaye sio wa kwako kwa kisingizio cha kitanda hakizai haramu wakati mkeo anajua mtoto yule sio wa kwako.15. Ni aibu na fedheha kulala kimapenzi na mwanamke ambaye anajua kuwa wewe unajua na unaushahidi wa michepuko yake16. Ni aibu na fedheha kumbembeleza mwanamke anayejua kuwa anakukosea kwa makusudi17. Ni aibu na fedheha kumaliza makanisa ukiwahadithia wachungaji tabia mbaya na usaliti wa mkeo18. Ni aibu na fedheha mkeo kukunyima unyumba ukaenda kumshitaki kwa wazazi wake wakati unajua cha kufanya19. Ni aibu na fedheha mara kukopakopa kwa wakwe zako tena waliostaafu kazi..ni aibu ni aibu kubwa.20. Ni aibuu na fedheha kwenda baa na mke baa au sehemu za starehe kila siku ikija bili unapewa wewe nawe unampa mkeo alipe kazi kukuna tu kidevu na kwenye wallet umejaza business card na viwembe vya kugushi nyaraka mitaani????Hizo ni baadhi tu ya aibu za wanaume waliowengi karne ya leo. Sambaza kwenye ma group wajijue na wamuombe Mungu awafungulie milango nao wawe wanaume katika nyumba zao
↧
Mwanamke Staha na Lugha Nzuri Ndio Silaha
Hata Uwe Mwanamke mzuri kiasi,mwenye rangi ya udongo wa fedha na kiuno kinachozuia upepo usivume, na una hela na kazi nzuri sana,Kama una KIBURI, LUGHA MBOVU, MAJIBU MABAYA.Hakuna Mwanaume atakaa na weweWakati mwingine mnaachwa mnajiuliza,'Amewezaje kuniacha na mi ni mzuri hivi', Jifanyie Internal Scanning kuhusu TONE yako unapoongea na Mwanaume, Mafahali wawili hawawezi kukaa zizi moja.Yaani wewe Afande KIBESI, na Mmeo Koplo KIBESI, Huo sio Uhusiano ila ni kikosi cha Askari wa Kiwango Security.A woman should be tender.Soft-tonned.Alistener.Huwa mnazidiwa vitu vidogo tu, we unajifanya kidume, wakati MCHEPUKO unaongelea puani hata kama mwanaume ndo kakosea, Shoga usimtafute mchawi wa ndoa/yako mahusiano yako n wewe mwenyewe na kibesi chako, wataka jitia jabali haki sawa, kama haki sawa KOJOA UMESIMAMA NA USIJIKOJOLEE!
↧
Haji Manara aburuzwa mahakamani
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara na wenzake watatu wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Haji ManaraImeelezwa kuwa wanadaiwa deni na fidia ya Tsh. milioni 83.3 baada ya kupokea bidhaa zenye nembo ya Dela Boss Perfume bila kuzilipia.Mbali na fedha hizo, Mlalamikaji aliyejitambulisha kwa majina ya Abu Masoud Al Jahdhamy, Ameiomba mahakama kuwaamuru washtakiwa hao watatu ambao ni, Haji Manara, Beatrice Ndungu na Palm General Supply kumlipa fidia nyingine itakayoona zinafaa ikiwemo gharama za mawakili.Kesi hiyo ya madai yenye namba 128/2019 ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mwandamizi, Wanjah Hamza, Imeahirishwa mpaka tarehe 29 Agosti Mwaka huu itakapotajwa tena.Katika madai ya msingi, mlalamikaji amefungua kesi hiyo akiwadai walalamikiwa fedha hizo baada ya kuwasambazia bidhaa zenye nembo ya “De La Boss Perfume” Tanzania na bidhaa hizo zimetengenezwa Dubai.
↧
Bora Niuze Bikira Yangu Kuliko Niitoe Bure Halafu Baadae Nijute
Watu wamekuwa waongo sana , Utasikia ooohh mi ntakuoa ukinipa, siku akishapa tu anachokitaka anakula kona, Marafiki zangu wote zao zimeshatolewa ukiwauliza walio watoa hata hawajulikani walipo..Wamewatenda na kusepa ...Mie bora tu niuze yangu Bei poa kabisaa laki tano za kibongo..hayo ni maneno ya Msichana mmoja kutoka Kenya Alivyoandika kwenye Facebook page yake!!
↧
↧
Msanii Tekno akamatwa na Polisi
Polisi wa Jiji la Logos nchini Nigeria, wamemkamata msanii na mtayarishaji wa muziki nchini humo Tekno Miles pamoja na wasichana wawili.Polisi wamesema wamemkamata staa huyo kwa sababu ya kumuuliza maswali na kumfanyia uchunguzi kwa tukio ambalo amelifanya wikiendi iliyopita.Wikiendi iliyopita zilienea video katika mitandao ya kijamii zikionyesha Tekno akiwarekodi wasichana watatu wakiwa wanacheza huku nusu ya maungo ya miili yao yakiwa wazi na yeye akiwatunza pesa.Siku ya Jumapili Tekno aliomba msamaha kwa kutumia barua baada ya kufanya tukio hilo na amesema wasichana hao amewatumia katika video yake mpya itakayotoka siku za hivi karibuni, na wala hakuwa na nia mbaya kuwarekodi video hizo.
↧
SIMBA Day Noma.... Uwanja wa Taifa umejaa, Mo Dewji aagiza zifungwe TV nje ya uwanja mashabiki waendelee kuburudika
Katika kuadhimisha kilele cha Simba Day Jana, Mashabiki wa klabu ya Simba wamefanikiwa kujaza uwanja wa Taifa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mo Dewji.Mo Dewji akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja huo, Amesema kuwa uwanja umejaa na ameshaagiza zifungwe TV nje ya uwanja huo ili mashabiki waliokosa nafasi ya kuingia watazame tukio hilo Live.
↧
Mashabiki wa SIMBA Wavunja Record Kwa Kununua Viti Vyote 60,000 Uwanja wa Taifa
Mashabiki wa Simba wakomba tiketi zote za SportPesa Simba WikiMashabiki wa klabu ya Simba wamedhihirisha ubingwa wao leo na kuweka rekodi ya kujaza uwanja wa Taifa kwa kuuza tiketi zote 60,000 za SportPesa Simba Wiki ambayo imekamilika siku ya leo.Zilianza kumalizika tiketi za mzunguko ambazo zilikuwa zinauzwa 5,000 (buku tano) kabla ya nyingine ambazo zilikuwa zinauzwa 150,000 kwa Platinum, 100,000 Platinum, VIP A 30,000, VIP B na C 15,000 nazo pia zikaisha.Hivyo Simba wameweka rekodi ya kuuza tiketi zote ambazo waliziandaa kwenye mchezo wa leo wa kimataifa dhidi ya Power Dynamo ambapo wameibuka na ushindi wa mabao 3-1.
↧
Yajue Madhara ya Kuingiza Vitu Ukeni au Kuuosha Kwa Kuusugua
Hivi karibuni kumekua na malalamiko mengi toka kwa wasichana kutopata ujauzito na wengine kutofurahia pale wanaposhiriki tendo la ndoa.Wanawake wengi hasa wenye umri kati ya miaka 18-45 wamekua wakikumbwa na matatizo mbalimbali ya uzazi bila kujua kwamba kwa namna moja ama nyingine wao wenyewe ndio chanzo cha matatizo hayo.Leo nimekuja na taarifa na tahadhari zilizotolewa na madaktari wakubwa nchini marekani ambao wameeleza mambo gani ya kuzingatia na kutothubutu hata kujaribu kwa kulinda afya ya uzazi na kutoharibu uke wako.Mtaalamu wa Constance Young Daktari na profesa katika chuo cha Columbia University anatueleza mambo ya kuzingatia kutoharibu uke wako.1.VAGINAL DOUCHINGHii ile tabia ya kuosha sehemu za ndani ya uke kwa kutumia viosheo maalumu vinavyopatikana madukani au supermarket mbali mbali, Hapana hii ni tofauti na ule unawaji wa kawaida au uoshaji wa kawaida unapokwenda kuoga, haijakatazwa kuosha uke wako kwa maji ya uvuguvugu kwa kuwa hiyo ni salama na haina matatizo kiafya.Vagina douching ni kule kutumia sabuni za maji au maji maalumu ambayo yanakua yamechanganywa na iodine,vinegar na magadi na kuyaingiza ndani ya uke, hii ni hatari kwa afya ya uke wako.Njia bora ya kujisafisha ni kutumia maji ya uvuguvugu pale unapooga kwa kusafisha sehemu za nje na sio ndani ya uke kwakua inaelezwa kwamba uke hua unajisafisha wenyewe kwani hutoa kitu kinachoitwa mucous ambayo ina control damu na uchafu mbali mbali ndani ya uke.2. INSERTING UFOsNajua unafahamu kipi kinatakiwa kiingie na kipi kisiingie kwenye njia yako ya uzazi[ukeni],vidole,uume, na vifaa vya hedhi sio tatizo kiafya ila kumekua na tabia kwa baadhi ya wanawake kutumia ndizi na vitu vinavyofanana na hivo katika kile kinacho aminika kujiridhisha pale anapokua mbali na mwenzi wake.Kama hujawahi kufanya tafadhari usijaribu na kama unafanya acha mara moja vitu hivi husababisha vaginal irritation ni maumivu katika uke na michubuko ambayo itakufanya usifurahie tendo la ndoa.3.SELF MEDICATINGDk. Dardik ameeleza kuwa tabia ya kujitibu bila kuwaona madakta wa matatizo ya wanawake si jambo nzuri kwa kuwa imesababisha matatizo makubwa kwa wanawake wengi ameeleza kuwa kuna wanawake wanatumia vitunguu swaumu, limao na wengine hata sabuni bila ya kufuta utaratibu na ushauri wa daktari.Uke umejumuisha bakteria wabaya na wazuri wote hao wanakazi maalumu ya kufanya usawa wa homoni ukeni, matumizi ya madawa makali husababisha uwepo wa bakteria wabaya na hatimaye mwanamke anaweza kuona siku zake za hedhi haziendi sawa na wengine kutokwa damu nyingi na maumivu makali wanapokuwa katika mzunguko.4.VAGINAL STEAMINGHiki ni kitendo cha kujifukiza kwa marashi, kumekua kiaminika na baadhi ya matabibu wa asili kutokea nchi za uchina, korea na japani ambao wameambukiza hadi mataifa kama Marekani na Uingereza tendo hili huitwa vaginal steaming huchukuliwa marashi yanaitwa VAGI-STEAM na mwanamke hukaa juu ya kiti ambacho chini yake kuna bakuli yenye maji yamoto na mvuke huo huenda moja kwa moja kwenye sehemu za uke.Jambo hili hufanywa kwa nia ya kusafisha uke lakini imepigwa vita na madaktari wakieleza kwamba si sahihi kwani huwaondoa baadhi ya bakteria wanaotakiwa katika kurekebisha mfumo wa homoni na kusababisha madhara.
↧
↧
Zari Hassan Afunguka Kuhusu TETESI za Kumcheat Diamond
Mzazi mwenza wa Daimond Platnumz Zarina Hassan ‘Zari The Boss lady’ amesema hajawahi kutembea na mwanaume yeyote mwingine wakati yuko kwenye uhusiano na mwanamuziki huyo.Katika mahojiano yake na mtandao wa Millard Ayo, Zari amesema tuhuma zilizotolewa na Diamond kuwa alitembea na moja ya wasanii mapacha kutoka P Square na aliyekuwa mkufunzi wake wa gym wakati yuko kwenye uhusiano na msanii huyo si za kweli.“P Square ndiyo alikuwa wa kwanza kumwambia Diamond tusiachane kwa sababu familia ni kitu bora kuliko chochote. Tulikuwa tunaingia karibu miaka minne, kwaajili ya maisha yangu, ya wanangu, nilikubali kupoteza kila kitu ikiwemo nafsi yangu kwaajili yake, Mungu ndiyo shahidi wangu. Sijawahi kutembea na mwanaume yeyote yule,” Zari amesema.“Nilizama katika penzi lake, na kwa sababu nilihisi kwamba nimetoka katika uhusiano mwingine, kwa hiyo nilitaka pia kuujenga uhusiano wangu uwe imara kama uliopita, na nilidhani hata ungekuwa ni wa milele, sijawahi kumdanganya Diamond.”Amesema Diamond alikuwa anatafuta sababu ya kuvunja uhuiano wao kwa sababu tayari alikuwa anajua amefanya kosa la kupata mtoto mwingine nje ya uhusiano wao, hali iliyosababisha kuongea maneno mengi ya uongo.
↧
Siwema Amwagia Sifa Nay wa Mitego
MREMBO ambaye ni mzazi mwenziye na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Siwema Edson amesema hawezi kuwa mchoyo wa kutoa pongezi kwa mzazi mwenziye huyo kwa jinsi anavyomlea mtoto wao, Curtis kwa sababu ni baba bora. Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Siwema alisema kuwa ,hata kama wana tofauti lakini kwa upande huo anampa hongera kwa sababu hata hivyo alimuacha mtoto akiwa mdogo kutokana na matatizo ya hapa na pale lakini Mungu ni mwema alijitahidi kumlea kwa mapenzi makubwa.“Unajua siwezi kumsema Nay kwa mabaya tu maana mambo yalishapita kitambo sana, il a ukweli najivunia ni baba bora kwa mtoto wetu na hata kama hatupo pamoja lakini mtoto ahisi tofauti kabisa kutokana na mapenzi makubwa anayopata kutoka kwa baba,” alisema Nay ambaye anaendelea na maisha yake jijini Mwanza.
↧
Mtoto wa Beyonce Avunja Rekodi
BLUE Ivy ambaye ni mtoto wa mastaa wanaokimbiza kwenye Muziki wa R&B na Hip Hop kutoka Marekani, Jay-Z na Beyonce, amefuata nyayo zao kwa kuvunja rekodi kwenye ‘chart’ za Billboard. Blue Ivy amevunja rekodi ya kuwa mdogo zaidi kuwahi kuingia katika chart za Billboard Hot 100 akiwa na miaka 7 tu jambo ambalo halijawahi kufikiwa na mtoto yeyote.Mtoto huyo ameingia katika chart hizo kupitia ngoma alioshirikishwa na mama yake, Brown Skin Girl ambayo pia wapo SAINt JHN na Wizkid. Ngoma hiyo kwa wiki hii imeshika namba 76 na inatabiriwa kuzidi kupanda zaidi ya hapo. Ikumbukwe kuwa wazazi wake wote wawili walishawahi kuingia kwenye chart hizo mara kibao
↧